Makapuku Forum

Makapuku Forum

UNAAMBIWA

Sio ajabu kusikia Mtu anasema akifa azikwe na kitu flani, hiyo ilitokea kwa Billy Standley wa Ohio Marekani ambae alipenda sana michezo ya kuendesha pikipiki na wakati wote alikuwa anawaambia Rafiki zake kuwa anatamani azikwe akiwa juu ya pikipiki yake aliyokuwa anaipenda sana.

Billy ambaye alizaliwa Mwaka 1931 alifariki Mwaka 2014 ambapo Rafiki na Ndugu zake walitimiza ahadi kwa kumuweka juu ya pikipiki ndani ya jeneza lenye kioo na kila Mtu akawa anamuona.
Screenshot_20210922-145833_Instagram.jpg
Screenshot_20210922-145851_Instagram.jpg
Screenshot_20210922-145913_Instagram.jpg
Screenshot_20210922-150018_Instagram.jpg
 
UNAAMBIWA

Mapacha wa Marekani Abigail Hensel (Abby) na Brittany Hensel wameungana hivi toka walipozaliwa March 07,1990 wakiwa na mwili mmoja lakini kila Mtu ana kichwa chake, moyo wake, tumbo lake , uti wa mgongo na hata mapafu yake pia.

Abby na Brittany kila mmoja ana mguu mmoja na mkono mmoja ambayo inafanya kazi kwa kushirikiana, kwahiyo hushirikiana kwenye kutembea, kupiga makofi, kuogelea, kukimbia, kuendesha Gari n.k ingawa wana uwezo wa kuongea, kula au kuandika kila Mtu kivyake.

Walizaliwa New Germany , Minnesota Marekani wakasoma hadi Elimu ya Chuo Kikuu, Bethel University na sasa wameajiriwa kama Walimu wakifundisha Sunnyside Elementary , New Brighton.

"Kwa sasa tunapata Mshahara mmoja kwakuwa tunafanya kazi ya Mtu mmoja kwa pamoja lakini katika siku zijazo tunafikiria kuongea na Maboss zetu watuongezee mshahara au kila Mtu apewe mshahara wake maana tuna Degree mbili kila Mtu yake na pia tunao uwezo wa kufundisha masomo tofauti kila mmoja au kufundisha kwa njia tofauti, mfano mmoja anaweza kuwa anafundisha huku mmoja anasimamia uelewa wa Wanafunzi na kujibu maswali Yao" ——— Abby
Screenshot_20210922-150446_Instagram.jpg
 
UNAAMBIWA:

Wanachuo wa The National Polytechnic Insitute huko Cambodia wamebuni Drone itakayosaidia kubeba Watu na kupaa kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine.

Wanafunzi hao wamefanikiwa kutengeneza Drone ambayo kwa sasa ina uwezo wa kubeba Mtu mmoja mwenye uzito usiozidi Kilo 60 ambaye anakaa kwenye kiti juu ya Drone, ikiwa na uwezo wa kuruka kwa Dakika 10 umbali wa 0.6 Miles

Vilevile wanafikiria pia Drone hizo zisaidie kwenye majanga kama kuzima moto ambao unawaka kwenye majengo marefu ———> “kwa sasa Drone ina uwezo wa kuruka urefu wa futi 13.1 kwenda juu lakini tunapambana ili kuboresha iende juu zaidi na ikiwezekana ibebe zaidi ya Mtu mmoja"

Gharama ya kutengeneza Drone hiyo ni USD 20,000 (Tsh. Milioni 46.3) ambapo wanafikiria kuzitengeneza nyingi zaidi ili waziuze,
Screenshot_20210922-150623_Instagram.jpg
 
Licha ya Tanzania kuwa na Sheria ya vileo na sheria nyingine ambatani, matumizi holela ya pombe zenye asilimia kubwa ya kilevi yamekithiri mitaani na kusababisha madhara makubwa kwa jamii.

Mwaka 2017 Serikali ilipiga marufuku matumizi ya pombe za pakti maarufu kama viroba baada ya kubaini kukithiri kwa tabia za ulevi na uchafuzi wa mazingira, hata hivyo imebainika kuwa wafanyabiashara wa pombe sasa wamegeukia kwenye chupa ndogo za plastiki mithili ya chupa za vitakasa mikono (sanitizer) zinazouzwa kwa bei nafuu ya kati ya Sh500 hadi Sh2000.

Pombe hizo zina vilevi kati ya asilimia 35 hadi 43 na zinapatikana kirahisi kwenye maduka ya mitaani, vibanda vya wamachinga na hata kwenye vituo vya daladala na kugeuka mbadala wa bia zenye ujazo wa mililita 350 zenye kilevi cha asilimia 4.5 hadi asilimia 5 zinazouzwa kati ya Sh1,500 hadi Sh2,500.
Screenshot_20210922-150800_Instagram.jpg
 
Inawezekana Azam FC wanajua nguvu waliyoitumia kuchukua ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara 2013/14, kila wakikumbuka hawatamani tena ubingwa wa Ligi Kuu.

- Alex Luambano
Screenshot_20210922-150946_Instagram.jpg
Screenshot_20210922-151012_Instagram.jpg
 
KIMEUMANA !! Wananchi mzee Magoma mmemsikia __!!
.
Mzee anasisitiza Manara HATAKIWI ndani ya Yanga, kwani anawagawanya wanachama na mashabiki.
Screenshot_20210922-151833_Instagram.jpg
 
James Rodriguez Al Rayyan
.
Hatimaye klabu ya Everton imemalizana na timu ya Al Rayyan ya nchini Qatar ili kuwauzia kiungo wao kutoka Colombia, James Rodriguez katika dirisha lijalo la majira ya baridi litakalofanyika Januari, mwakani.
.
James amekuwa hapati nafasi ya kutosha kucheza kwenye kikosi cha kwanza cha Everton ambapo msimu huu hajacheza michuano yoyote. Mkataba wake unamalizika 2022.
.
Supastaa huyu alitua kikosini Everton akitokea Real Madrid.
Screenshot_20210922-151943_Instagram.jpg
 
Kocha wa Al Ahly mambo magumu
.
Pitso Mosimane amekalia kuti kavu kwa kitendo chake cha kupoteza mchezo wa Fainali ya Super Cup japo jana dhidi ya El Geish na muda wowote anaweza fungashiwa vilago
Screenshot_20210922-152043_Instagram.jpg
 
Man United vitani kwa Kessie
.
Mabosi wa Manchester United wameamua kuingia kwenye vita dhidi ya Liverpool na PSG ili kuipata saini ya kiungo wa AC Milan na Ivory Coast, Franck Kessie, 24, katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi akawe mbadala wa Paul Pogba, 28, ambaye mkataba wake unamalizika mwakani.
.
Man United imekuwa kwenye sintofahamu ya muda kwa sababu hadi sasa Pogba amegoma kusaini mkataba mpya wa kuendelea kusalia kwenye viunga hivyo licha ya kuwekewa ofa mezani.
.
Kessie ni miongoni mwa wachezaji walioonyesha kiwango bora Milan tangu atue 2019 na msimu huu amecheza mechi tatu za michuano yote. Mkataba wake wa sasa unamalizika 2022.

Screenshot_20210922-152510_Instagram.jpg
 
Saka awindwa na vigogo Italia na Spain
.
Juventus na Atletico Madrid ni miongoni mwa timu zilizoonyesha nia ya kumsainisha mkataba winga wa Arsenal na England, Bukayo Saka, 20, katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi.
.
Saka ni miongoni mwa wachezaji vijana walioonyesha viwango bora katika msimu uliopita akiwa na Arsenal na timu ya taifa ya England. Mkataba wake unamalizika 2024. Saka amejihakikishia namba ya kudumu kikosini Arsenal.
Screenshot_20210922-152602_Instagram.jpg
 
Kocha wa Al Ahly mambo magumu
.
Pitso Mosimane amekalia kuti kavu kwa kitendo chake cha kupoteza mchezo wa Fainali ya Super Cup japo jana dhidi ya El Geish na muda wowote anaweza fungashiwa vilago
View attachment 1948417
Kufanya kazi na timu kama al ahly ni tabu tupu, hawajui matokeo matatu, hawajui kuteleza, ni ngumu coach kushinda kila game, kila kombe pasina kupoteza hata kimoja, haiweezekani.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom