

Farhan Jr
DIDIER GOMES NA SIMBA, KIPI NI KITUO KINACHOFUATA?
Pep Guardiola baada ya kubeba ubingwa wa UEFA 2009 mbele ya Manchester United alijifungia chumbani akawauliza maswali matatu Wasaidizi wake akiwemo Marehemu Tito Vilanova
Swali la kwanza! Mafanikio haya yatadumu kwa muda gani? Swali la pili! Tutaweza kutengeneza timu nyingine ya ushindi? Swali la tatu! Naweza kuwa na timu ya kutwaa tena UEFA? na mwisho! Tutaweza kumudu kwenye kiwango hiki?
Pep aliwahoji wenzie na alisema wazi kuwa ikitokea amepambana na amefeli na haoni njia mbadala basi ataaga na kuondoka Barcelona! Bila shaka mnakumbuka Pep baada ya miaka minne aliondoka Catalunya
Well nimeitazama Simba, nimeona kabisa Didier Gomes anajiuliza na kuwauliza wenzie maswali yale yale manne ambayo Pep aliwauliza wenzie pale Stade de Olimpico, Roma nchini Italia, Mei 27, 2009
Nimegundua kupitia mechi na TP MAZEMBE, Mwalimu analijibu swali la pili kwa namna gani ataendelea kuwa na kikosi cha ushindani! Kwanza alianza na Rally Bwalya akicheza juu ya Thadeo Lwanga na Saido Kanoute
Mwalimu alimtaka Rally awe huru na mpira acheze free role! Lakini baadae kwenye press alisema wazi kuwa kuna vitu Bwalya hakuvitimiza kwa ufasaha ila akasema hakuanza vibaya sana
Well wakiwa na Clatous Chama hii Simba ilikuwa inacheza mpira wa pass mpaka wafike golini kwa mpinzani! Bahati mbaya sasa Chama hayupo na ni wazi Mwalimu anaitaka Simba icheze soka la haraka kufika kwa mpinzani
Alipowaanzisha Chris Mugalu, Dennis Kibu na Bernard Morrison ni wazi anataka timu itembee, waondoke kwenye pass nyingi na kufika langoni mapema ndio maana hata Mugalu alikuwa anaenda pembeni na chini kuomba mipira
Mwalimu anataka kuyalinda mafanikio yake na tayari anajua watu alonao! Anajua Duncan Nyoni ni myumbufu na Peter Banda ni mnyumbufu pasi na kusahau Ousmane Sakho! Wote wanatembea kwenye chaki na timu lazima ikimbie
Naona Ousmane Sakho ataenda kuwa Mtu muhimu kwenye hii timu, naona Simba itaondoka kwenye pass nyingi na kuelekea mpira wa kasi na kufika langoni kwa haraka! Ndio njia ya kulinda mafanikio
Benchi linajua halina Chama tena, hivyo wameamua kuuvua mfumo ule na kuanza mfumo mpya