Biashara ya pembejeo za kilimo

MPSZX PAULO

Member
Mar 12, 2020
38
32
Habari zenu Wana JF,

Awali ya yote ningependa kumshukuru mwezi mungu Kwa kutujalia uzima na afya njema Kwa niaba ya wa JF wote.

Andiko langu ni kutaka msaada Kwa waliotangulia katika tasnia ya biashara ya pembejeo za kilimo katika mambo yafuatayo:

1. Ni mtaji kiasi gani kiwango Cha chini kabisa kinaweza anzisha biashara ya pembejeo
2. Mi ofisi gani napaswa kuanzia ili kupata kibali Cha kufanya biashara hiyo kihalali
3. Gharama za kupata kibali ni kiasi gani na wapi napaswa kulipia
4. Pia huwa nasikia kuna vyeti vya TPRI,TOSCI,TFRA utaratibu wa kutolewa upoje

Na changamoto za biashara ya pembejeo ni zipi?

Naomba kuwasilisha asanteni sana na karibuni wenye ujuzi na uzoefu tusaidiane
 
Back
Top Bottom