Makapuku Forum

Makapuku Forum

Derek Chauvin aliyekua Polisi wa Minnesota Marekani na baadaye kuhukumiwa kifungo cha miaka 22 jela baada ya kukutwa na hatia ya kumuua George Floyd May, 25 2020, amekata rufaa.

Derek ambaye anatajwa kuwa Polisi wa kwanza Mzungu kuwajibishwa kwa mauaji ya Mtu mweusi Minnesota, amekata rufaa hiyo katika Mahakama ya Rufaa Minnesota akipinga hukumu hiyo na kusema alionewa na hakupewa haki zake za msingi wakati wa maamuzi.
Screenshot_20210924-202620_Instagram.jpg
 
"Tunataka kuendelea kupata mafanikio na mwaka huu ligi itakua ngumu na kila mechi kwetu itakua ya muhimu"
.
"Hivyo basi itatubidi kuwa na nguvu ya ushindani ili kuweza kupata vikombe vilivyo mbele yetu ikiwemo Ngao ya Jamii na pia kombe la klabu bingwa Afrika"

- Mo Dewji, Mwenyekiti Bodi ya Wakurugenzi Simba.
Screenshot_20210924-203113_Instagram.jpg
 
Wanachama Yanga kumrejesha Nugaz
.
ZaChiniChini Kutoka Jangwani kuna mvutano mkali kwa baadhi ya mashabiki (Yanga Lialia) na wazee wa Baraza ambao wameutaka Uongozi wa klabu hiyo kumrejesha aliyekuwa afisa uhamasishaji Sheikh Antonio Nugaz Mr Wape salaaam mzee wa kuvimbaa !!
.
Wanachama hao wamedai Nugaz ameitendea haki kazi yake ya Uhamasishaji na hata kuibuka kinara kwa idara ya Uhamasishaji kwa msimu wa 2020/21
Screenshot_20210924-203222_Instagram.jpg
 
Wananchi mmesikia kocha Nabi anasema mpeni muda kama miezi miwili au mitatu timu ikipata MUUNGANIKO itakuwa tishio AFRIKA !!

nyieee hamna kocha hapa miezi 3 simba inamsubiria tu
Screenshot_20210924-203503_Instagram.jpg
 
Mourinho kumng’oa Dalot United
.
Kocha wa AS Roma, Jose Mourinho amependekeza jina la beki wa Manchester United na Ureno Diogo Dalot ili asajiliwe katika dirisha lijalo la majira ya baridi.
.
Dalot amekuwa hapati nafasi ya kutosha kwenye kikosi cha kwanza cha Man United tangu arejee kutoka AC Milan alipokuwa akicheza kwa mkopo.
Screenshot_20210924-203736_Instagram.jpg
 
"Nina imani tutaanza msimu vizuri kwa kushinda taji, tumefanya maandalizi ya kutosha wakati huu, tumejipanga kimbinu na tumeendelea kurekebisha makosa machache, pia tumeboresha maeneo tuliyokuwa bora ili kuhakikisha tunaanza msimu kwa kuchukua taji kama tulivyomaliza msimu kwa kushinda mataji.

- Didier Gomes, Kocha Mkuu Simba SC.

Nyieeee huyu ndio kocha sasa.
Screenshot_20210924-204747_Instagram.jpg
 
Sababu za Kaze Kurudi Yanga Zatajwa
.
“Leseni yake ya ukocha (leseni A ya CAF), ni sababu kubwa ya Kaze kurejeshwa Yanga. Viongozi wanaona hii itawasaidia Yanga kuwa chini ya makocha ambao wana leseni kubwa kutoka kwenye Shirikisho la Soka Afrika.
.
“Jambo lingine ni lugha, Kaze ni mzuri sana kwenye kuzungumza lugha nne kwa ufasaha ambazo ni Kiswahili, Kiingereza, Kifaransa na Kirundi, ndani ya timu kuna wachezaji wenye kutumia hizo lugha zote nne.
.
“Hivyo itakuwa rahisi kwa Kaze kuweka daraja kati ya kocha mkuu na wachezaji, pia itapunguza gharama za kuwa na mkalimani wa timu.
.
“Lakini Kaze ni mzuri kwenye mbinu na mikakati, ni rahisi kwa kocha mkuu kubadilisha mbinu na mipango ya timu, programu za mazoezi punde tu anapopewa ushauri na msaidizi wake ambaye naye ni kocha mzuri.
.
“Kaze ameishi Tanzania akiifundisha Yanga kwa takriban miezi sita, anavijua vizuri viwanja vya mikoani, hivyo ni rahisi kumsaidia mwalimu juu ya uchaguzi wa wachezaji sahihi kwenye viwanja tofauti.”
Screenshot_20210924-204909_Instagram.jpg
 
TAMBWE: VIGOGO WA TIMU WANAVURUGA DERBY
.
Straika wa zamani wa Yanga na Simba, Amissi Tambwe amesema licha ya kufanya maandalizi, lakini inapofika siku ya mechi ya dabi maisha huwa ni tofauti kabisa.
.
Anasema unapewa presha na viongozi kwa kuambiwa kuwa hii ni mechi muhimu kwetu na lazima tupate matokeo mazuri, hali inayompa presha mchezaji kiasi cha kutaka kujivunja ilimradi asiicheze kuepuka lawama.
.
Tambwe mbaye ni raia wa Burundi anayekipiga DTB ya Daraja la Kwanza, alisema mechi hiyo maisha yake ni tofauti kabisa na zingine kwenye maisha ya mchezaji.
Screenshot_20210924-205021_Instagram.jpg
 
Zlatan Ibrahimovic:

"Sio kweli kwa namna vyombo vya habari vinavyoripoti. Wachezaji wote Wanakula sana. Iwe wanafanya hivyo mbele ya wenzako au kwa kujificha wakiwa majumbani kwao, sisi sote tunakula sana.
.
"Wengine huchagua kuwa wakweli na kula mbele ya kila mtu sio kuigiza kama wana kula kidogo. Wakati huo huo tukiwa nyumbani tunarudia hadi sahani mbili za kila mlo kama watu wengine wa kawaida. Ninakula sana na ninacheza vizuri tu kama kila mchezaji mwingine.
.
"Tuache kuigiza kwa sababu sisi tunataka vyombo vya habari Vitusifu. Sote tunajua kuwa tunakula sana wakati vyombo vya habari vinapokuwa havipo. "

ujue Zlatan linaongeaga ukweli bwana kama mbongo mswahili huyu jamaa
Screenshot_20210924-205218_Instagram.jpg
 
Kayoko Pilato Ngao ya Jamii
.
Mwamuzi wa kimataifa wa Tanzania, Ramadhan Kayoko ndiye atachezesha mechi ya Ngao ya Jamii baina ya Simba na Yanga itakayochezwa katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam Jumamosi hii.
.
Kayoko atasaidiwa na refa msaidizi namba moja Frank Komba, refa msaidizi namba mbili Soud Lila na refa wa akiba Heri Sasii wote wakitokea Dar es Salaam.
Screenshot_20210924-205409_Instagram.jpg
 
Barcelona yajitosa Man United kumng’oa Martial
.
Straika wa Manchester United na Ufaransa, Anthony Martial anatarajiwa kuondoka katika dirisha lijalo la majira ya baridi baada ya Barcelona kuonyesha nia ya kutaka kumsajili.
.
Taarifa zinadai Man United ipo tayari kumuachia dirisha lijalo ikiwa timu yoyote itatoa ofa nono kwa sababu hayupo kwenye mipango ya Kocha Solskjaer.
.
Mchezaji huyo alitabiriwa kufanya mambo makubwa wakati anajiunga na Man United 2015, lakini siku hadi siku mambo yanaonekana kuwa magumu upande wake. Msimu huu amecheza mechi sita za michuano yote na hajafunga hata bao moja, huku mechi nyingi alizocheza aliingia akitokea benchi.
Screenshot_20210924-205542_Instagram.jpg
 
Farhan Jr

SIMBA SPORTS CLUB, EITHER HATE OR GET MOTIVATED

Ni siku nyingine tena klabu ya Simba imesaini dili na Kampuni ya Africarriers ambao wanatoa million 800 na mabasi matatu, jumlisha na matengenezo yake! Ni kama Real Madrid ana mabasi ya AUDI ardhini na ana ndege za EMIRATES angani

Hii inakuja baada ya wiki iliyopita kutangaza dili la Air Tanzania! Hii ni kusema Simba wana Mdhamini wa Ardhini (Africarriers) na Mdhamini wa angani (Air Tanzania)

Ngoja tupeane darasa kidogo! Kwenye wadhamini wa klabu wapo wa aina tatu! Kuna MAIN SPONSORS, GLOBAL SPONSORS na REGIONAL SPONSORS! Simba wanalifahamu vyema na wanabalance vyema

Kwenye Main Sponsors wanapimwa kwa pesa wanayoweka ndani ya klabu ndio hao wa kukaa mbele ya jezi kama Sportpesa, Co-Sponsors wakikaa pembeni au kwenye traveling kits!

Dili la Simba la leo limepelekwa kwenye jezi kifuani kwa timu ya vijana na sleeve sponsorship kwa timu ya Wanawake! Imagine! Hii ina maana kuwa rate card ya kuwekeza Simba ni kubwa, ina maana kibiashara klabu imepiga hatua

Unapata picha gani kusikia leo hii udhamini wa million 800 na mabasi matatu ila bado Kampuni haijakaa kifuani! That's business at its best! Hii ndio maana halisi ya kusema hizi timu zina pesa

Nadhani CEO Barbra aendelee kupambana kupata partners na Sponsors wengi zaidi kama hivi sasa! Zije partnership za hotel, klabu italala! Zije Partnership za hospital (klabu ipate matibabu)

Barbra aendelee kupambana zije partnership za suti rasmi za klabu, zije partnership rasmi za Perfume za klabu! Huku ndipo wanapoelekea na ndipo Simba wanapaswa kujivunia

Al Ahly hakufanikiwa kiuchumi kwa kujifungia bali kutoka na kuzifuata fursa! Leo hii ana wadhamini zaidi ya 13! Hana presha na ndio maana ana nguvu Afrika, ndipo anapoenda Simba

MO Dewji anaposema klabu inajiendesha kwa hasara nadhani tuwe tunaelewa! Timu inapaswa kuwa na madili mengi kama haya ili iingize faida ya kutosha sana! Ndivyo ilivyo! Bajeti ya Simba kwa siku ni zaidi ya Million 10! Piga hesabu!

Hongereni sana babra kwa kuendelea kupambana kuhakikisha klabu inasimama yenyewe
Screenshot_20210924-205730_Instagram.jpg
 
Farhan Jr

KOCHA NABI, KOCHA ZAHERA, KOCHA KAZE! HAKUNA MATATA

Upana wa bench la Ufundi imekuwa agenda duniani! Dunia imebadilika sana kwa Walimu! Benchi linataka Kocha wa mbinu, Kocha wa Man Management, Kocha wa Nature na nurturing

Ndio maana sasa hivi timu nyingi zinajaza benchi imara na pana sana! Ndio maana United walimuongeza Mike Phelan kwakuwa ni bora kwenye Man Management, ndio maana walimuongeza Carrick kwa kitu kama hicho

To me Yanga nawapongeza sana kuwa na Makocha watatu wa viwango vikubwa sana! CAF , CAF A na CAF A ni Quality kila eneo, hivyo kilichobaki ni muda kuamua! Hata Simba wana bench lao tena pana tu, and i like that

Mmoja kaniuliza swali kwanini walimfukuza Kaze na mbona wamemrudisha tena? Niwaambie tu kuwa Coaches are hired to be fired! Kumfukuza na kumrudisha Mwalimu inafanywa kwa SITUATIONAL ANALYSIS

SITUATIONAL ANALYSIS inasemaje? Ni kuwa malengo ya muda huu kayatimiza? Kama ndio kwa ukubwa gani? Kama sio ni kwa kiwango gani? Kisha wanafanya projection za WHAT IF? hapo ndipo duniani Kocha anaweza kurejea tena

Chelsea waliwahi kumtimua Jose Mourinho ila akarejea tena kufundisha! Real Madrid waliwahi kumtimua Carlo Ancelotti ila akarejea tena kufundisha! Huu ndio mpira kupitia SITUATIONAL ANALYSIS + WHAT IF ANALYSIS! Hivyo kumrejesha Kaze ni sahihi tu

Kuna Mtu akaniuliza Makocha wa viwango wote inawezekana vipi wakakubali kuwa Wasaidizi? Hapo nitamjibu kuwa Calvin Johnson alikuwa Head Coach pale Kaizer Chiefs ila ameenda kuwa Msaidizi wa Pitso Al Ahly, huu ndio mpira wa miguu

Mwisho, kuna Mtu akahoji hawa wataelewana? Niwaambie tu hii ni issue ya PERSONALITY tu! Mnaweza kupishana hata kama mna elimu tofauti na mnaweza kuendana hata kama mna elimu sawa!

Kwenye kazi hawa lazima waweke weledi na kusadiana! Jose Mourinho na Pep Guardiola waliwahi kuwa Wasaidizi wa Bobby Wiliamson pale Barcelona na Pep Guardiola aliwahi kuwa na Tito Vilanova kama Msaidizi na mambo yalienda! That's Football

Matola aliondoka Police Tanzania kwenda Simba kuwa Msaidizi ilhali kiutendaji alikuwa Mkuu pale Police! Hitimana alikubali kuwa Msaidizi Simba ilhali alitoka kuwa Mkuu kwingineko

THAT'S FOOTBALL
Screenshot_20210924-210035_Instagram.jpg
 
Farhan Jr

KOCHA NABI MOHAMED, KOCHA KAZE NA MWINYI ZAHERA = YANGA

Football duniani imepitia mabadiliko makubwa sana, hivi sasa unahitaji mwalimu mwenye vitu vingi sana haswa kwenye Man Management! Utofauti wa haiba unapelekea mabench kuwa na Makocha wengi

Ukiwatazama Mamelodi Sundowns wana Makocha watatu wakubwa ambao wana hadhi ya kuwa Makocha wakuu, Manchester United wana Makocha zaidi ya watatu, ni issue ya quality

Well Kocha Nabi hakuanza Pre Season na hata mechi za CAF hakuwa na Kocha Msaidizi baada ya wa awali kuondoka! Uongozi wa Yanga ulitaka kutumia muda kumpatia Mwalimu mtu sahihi

Katika majina mengi waliyotuma maombi, yakapatikana majina matatu ikiwemo Kocha Kaze! Mwalimu Nabi alipewa hiyo shortlist na kuchagua yule anaemtaka walimpa muda

Kupitia Network yake ya Walimu aliowahi kufanya nao kazi, mmoja aliwahi kufanya kazi na Kaze, hivyo ukijumlisha na CV yake basi Kocha Nabi mwenyewe akapendekeza jina lake kwa Viongozi, mwisho akaletewa

Ujio wa Kaze utasolve vitu viwili! Mosi changamoto ya lugha ambapo sasa Msaidizi atatafsiri moja kwa moja! Background Analysis ambapo Kaze amewahi kupita na pia analifahamu soka la ukanda huu

Nasikia Zahera kuna uwezekano wa kuwa Mkurugenzi ndani ya Yanga! Nadhani huyu ni Mtu muhimu zaidi kwenye hii klabu! Haswa kwenye kuunganisha mawazo ya kiufundi kwa watu wa Utawala

Haijawahi kuwa shida kwa Walimu kutoa mapendekezo lakini suala ni nani kwenye uongozi atadigest mawazo hayo kwenye mzani wa Utawala na Kiufundi? Bila shaka Mwinyi atawafaa hapa

Mwisho! Kinachotakiwa ni Viongozi na Mashabiki kuiamini na kuiheshimu project! Waipe MUDA bila presha then majibu yatapatikana kama kweli wanafanya haya kwa ajili ya kujenga

Yanga mmeshavuka kipindi cha TRIAL and ERROR na sasa ni actual investment! Kwenye MUDA
Screenshot_20210924-210333_Instagram.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom