Makapuku Forum

Ila akina Bush(Sr & Jr) hawajawahi kufungwa jela japo siku 3 tu pamoja na kuua watu wengi wakati wa utawala wao
ICC ipo kwaajili ya Waafrika tu
......
Hakuna haki hapa duniani!

Ila viongozi wa Kiafrika nao wamezidi. Tena wao wanaua raia wa nchi zao wenyewe. Akina Bush wanakwenda huko mbali wanaanzisha vurugu ambazo ukiangalia vizuri, japo kinadharia tu, in the long run zina lengo la kunufaisha nchi zao ama kiuchumi, kimkakati na hata kiusalama. Na historia inakiri kuwa hili limekuwa likifanyika miaka nenda miaka rudi. Watawala "mashuhuri" katika historia akina Genghis Khan, Napoleon, mafarao wa Misri, Wagriki na Waroma wa kale hata Hitler majuzi juzi hapa ni mifano dhahiri. Hawa angalau wakienda huko na kushinda vita vyao vya kujipanua basi himaya zao nzima zinakua na kujiimarisha. Viongozi wa Afrika wao wanaua watu wao wenyewe na lengo hasa ni wao kujitajirisha kupindukia. Hili ndiyo tofauti yao na akina Bush!
 
Kama nilivyoahidi jana kuwa ningeleta segment fupi kwa ajili ya kuangalia upakiaji mizigo kupita kiasi, jana sikufanikiwa ila leo nitaleta na itakuwa ya mtiririko kwa juma zima.

Karibuni.
 
Siyo Waafrika tu. Kiasili sisi ni wanyama na tuna ile instinct ya ubinafsi na umimi kwanza. Japo kwa juu juu tunaonekana kama tumestaarabika sana huko ndani tu wanyama tu. Ndiyo maana tumejiundia mavyombo mengi ya kiusalama ili kuhakikisha kuwa hatukiuki "ustaarabu" wetu. Imagine kama tusingekuwa na polisi, magereza na majeshi ya ulinzi na taasisi zinginezo za kiulinzi hali ingekuwaje. Tungebakia kuwa wastaarabu?

Na wakati mwingine ustaarabu na heshima vinakuja baada ya kupigana na kuuana kwanza. Wamarekani bila ile civil war yao majimbo ya kusini yakitaka kujitenga sidhani kama leo wangekuwa nchi moja. Wanaigeria nao Biafra hii ilishawafundisha somo muhimu. Hata Wakenya juzi juzi hapa walitunishiana misuli na nadhani leo hii kidogo wanaheshimiana heshimiana. Kupigana (wenyewe kwa wenyewe) kamwe si jambo jema lakini kuna wakati ndiyo njia pekee ya kuzungumza na kuheshimiana. Naamini Bongo hatutafika huko!
 
NUKUU YA LEO

Winning one league title at Roma to me is worth winning 10 at Juventus or Real Madrid.

Kushinda kombe moja la ligi nikiwa na Roma ni faida kubwa kwangu kuliko kushinda makombe 10 ukiwa na Juventus au Madrid

Haya maneno yalipata kusemwa na mwanasoka wa kimataifa ya Italia na klabu ya As Roma Bw. Francesco Totti. Totti alizaliwa sept. 27. 1976 mjini Roma-Itali

Francesco Totti anayevaa jezi namba 10 amedumu As Roma kwa miaka 24 na kuweka rekodi nyingi kuliko mtu yeyote.

Totti amecheza jumla ya mechi 786 na kufunga magoli na kufunga jumla ya magoli 307.

Juzi jumapili Totti alistaafu Rasmi kucheza soka ngazi ya Club wakati alistaafu team ya Taifa 2007 .

Nimefanya kwa ufupi tuu wakuu..ila week hii nitakuwa naleta matukio na nukuu za Francesco Totti.



Waitaliano wanasema


No Totti, No party
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…