Makapuku Forum

Makapuku Forum

490562b4bf765a12847c38ae543c983c.jpg
28bf7e8ce17d1d8ec60a4690caf52124.jpg
Ila akina Bush(Sr & Jr) hawajawahi kufungwa jela japo siku 3 tu pamoja na kuua watu wengi wakati wa utawala wao
ICC ipo kwaajili ya Waafrika tu
......
Hakuna haki hapa duniani!

Ila viongozi wa Kiafrika nao wamezidi. Tena wao wanaua raia wa nchi zao wenyewe. Akina Bush wanakwenda huko mbali wanaanzisha vurugu ambazo ukiangalia vizuri, japo kinadharia tu, in the long run zina lengo la kunufaisha nchi zao ama kiuchumi, kimkakati na hata kiusalama. Na historia inakiri kuwa hili limekuwa likifanyika miaka nenda miaka rudi. Watawala "mashuhuri" katika historia akina Genghis Khan, Napoleon, mafarao wa Misri, Wagriki na Waroma wa kale hata Hitler majuzi juzi hapa ni mifano dhahiri. Hawa angalau wakienda huko na kushinda vita vyao vya kujipanua basi himaya zao nzima zinakua na kujiimarisha. Viongozi wa Afrika wao wanaua watu wao wenyewe na lengo hasa ni wao kujitajirisha kupindukia. Hili ndiyo tofauti yao na akina Bush!
 
2d6d8c99f8d52667f7d089cc39a74f59.jpg
459c1c2fb41003d4ac1e16e89366f50c.jpg
9fdb8894e3ff2ff1af4b29a0a72ee0d9.jpg
947bd6c3430aa4b7deaa14e0402cb963.jpg
Waafrika linapokuja suala la madaraka hatuwezi kuafikiana kwa njia za amani mfano ingeweza kuitishwa kura ya maoni lakini zisingeheshimika wajanja wangeiba kura tu
Hata Sudan sio kwamba wamekubaliana kiroho safi bali waneshinikizwa tu na Jumuiya za Kimataifa
.
Ingekuwepo demokrasia basi hata Wazenji wangeshaachana na Muungano muda mrefu tu
......
Siyo Waafrika tu. Kiasili sisi ni wanyama na tuna ile instinct ya ubinafsi na umimi kwanza. Japo kwa juu juu tunaonekana kama tumestaarabika sana huko ndani tu wanyama tu. Ndiyo maana tumejiundia mavyombo mengi ya kiusalama ili kuhakikisha kuwa hatukiuki "ustaarabu" wetu. Imagine kama tusingekuwa na polisi, magereza na majeshi ya ulinzi na taasisi zinginezo za kiulinzi hali ingekuwaje. Tungebakia kuwa wastaarabu?

Na wakati mwingine ustaarabu na heshima vinakuja baada ya kupigana na kuuana kwanza. Wamarekani bila ile civil war yao majimbo ya kusini yakitaka kujitenga sidhani kama leo wangekuwa nchi moja. Wanaigeria nao Biafra hii ilishawafundisha somo muhimu. Hata Wakenya juzi juzi hapa walitunishiana misuli na nadhani leo hii kidogo wanaheshimiana heshimiana. Kupigana (wenyewe kwa wenyewe) kamwe si jambo jema lakini kuna wakati ndiyo njia pekee ya kuzungumza na kuheshimiana. Naamini Bongo hatutafika huko!
 
NUKUU YA LEO

Winning one league title at Roma to me is worth winning 10 at Juventus or Real Madrid.

Kushinda kombe moja la ligi nikiwa na Roma ni faida kubwa kwangu kuliko kushinda makombe 10 ukiwa na Juventus au Madrid

Haya maneno yalipata kusemwa na mwanasoka wa kimataifa ya Italia na klabu ya As Roma Bw. Francesco Totti. Totti alizaliwa sept. 27. 1976 mjini Roma-Itali

Francesco Totti anayevaa jezi namba 10 amedumu As Roma kwa miaka 24 na kuweka rekodi nyingi kuliko mtu yeyote.

Totti amecheza jumla ya mechi 786 na kufunga magoli na kufunga jumla ya magoli 307.

Juzi jumapili Totti alistaafu Rasmi kucheza soka ngazi ya Club wakati alistaafu team ya Taifa 2007 .

Nimefanya kwa ufupi tuu wakuu..ila week hii nitakuwa naleta matukio na nukuu za Francesco Totti.
ea3bb64421f33f13ca066be1691a05d5.jpg

6482429eff93f41e8a4e14a4c6332806.jpg
1f333b0bce76f70ad1b7046dfdcfa25e.jpg


Waitaliano wanasema

No Totti, No party
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom