NUKUU YA LEO.
Muendelezo wa nukuu ya suicide note ya kevin Carter. Party 2
I am hunted by the vivid memories of killing and corpses and anger and pain of starving of wounded or children.
Ninafuatiliwa na kumbukumbu halisi za mauaji, maiti, hasira na maumivi ya watoto wenye njaa au waliojeruhiwa.
Kevin Carter ni mpiga picha/ mwandishi wa habari na mwanajeshi alezaliwa tar.13/9/1960 na kufariki tar. 27/07/1994 kwa kujifungia kwenye gari yake na kuvuta hewa ya carbonmonoxide.
Hiyo nukuu ilikuwa kwenye suicide note yake. Kevin alizaliwa na kuishi katika tabaka la watu wa kati nchini Afrika ya kusini. Kuna siku aliona polisi wakiwapiga watu weusi walioishi katika maeneo ya watu weupe.
Hii ilimuumiza, hakupenda hiki kitendo,
Mwaka 1980, aliona mhudumu wa mgahawani mwenye asili ya weusi akiteswa na kudhalilishwa, Kevin alizuia yule dada kupigwa, lakini ilipilekea kevin kupigwa na kusababishiwa majeraha mengi mwilini na wanajeshi wenzake weupe.
Baadaye tar 20 may 1983 kevin akashuhudia shambulio la bomu katika mtaa wa church jijini pretoria. Bumo hilo lililenga kusambulia kikosi cha anga (SAAF)ambacho alikimbilia baada ya kuondoka kikosi cha Ardhi. Kevin Cater anakimbia jeshini na kuanza kazi ya upigajia picha akiwa na kikundi cha Bang-Bang Club.
Kikundi cha Bang-Bang Kilikuwa ni kikundi cha waandishi wa habari na wapiga picha miaka ya 1990’s hasa kipindi cha kupigania uhuru wa Afrika ya Kusini.Bang Bang Club kiliundwa na kevin Carter mwenyewe, Jaoa silva, Ken Oosterbroek na Greg Marinovich.
Ken Oosterbroek aliuwawa wakati wa vurugu mjini Thokoza siku tisa (9) kabla ya uchaguzi wa kwanza Afrika ya kusini tar. 27/04/1994.
Jaoa silva mzaliwa wa ureno, anaishia Africa ya kunisi sasa hivi akiwa ni mtu ambaye bado anafanya kazi ya upigaji picha huku akiwa amepoteza mguu mmoja nchini Afghastan akiwa anapiga picha kwenye mapigano ya wanajeshi wa marekani na wapiganaji wa al-quida.
Greg Marinovich alikuwa wa kwanza kuchukua tuzo ya Pulitzer Prize baada ya kuchukua picha wakati wa mateso na mauaji ya mtu alieaminika kuwa jasusi3 wa kikundi cha kisiasa cha Inkatha mwaka 1991 nchini Afrika ya kusini. Sasa hivi anafundisha masuala ya habari chuo kikuu cha boston nchini marekani.
To be continued .....