1996 - Meli ya Mv Bukoba yazama katika Ziwa Viktoria na kuua watu zaidi ya 700.
Ilikuwa ikitoka Bukoba kwenda Mwanza, ilizama karibu na pwani ya Bwiru.
Rais wa kipindi hiko, Benjamin Mkapa alitangaza siku tatu za maombolezo na bendera kupepea nusu mlingoti.
Makaburi ya wahanga wa tukio hilo yapo Igoma, Mwanza ambapo walioshindwa kutambuliwa na ndugu zao walizikwa hapo.