Makapuku Forum

Makapuku Forum

Tuwaombee hata maadui na washindani wetu!
bda82ec316dc380e7806af5bc23b805c.jpg
 
Kazi zingine unaziomba halafu ukiipata unakuta ni kinyume kabisa na ulivyotegemea. Inabidi tu uifanye kwa sababu hakuna namna. Shedede kazi ya ulinzi ipo kama ulivyotegemea itakuwa hasa yule bosi mwenye wivu akiwepo?
ed5f0f3f6c37a841f5546726d07cf83c.jpg
 
Gitaa hupendezesha muziki

Naimani tumeshinda salama wadau, tukiendelea na mapumziko ya wiki ya kutumia baada ya kuwa tumepokea haki yetu.

Leo tumwangalie mwanadada maarufu kwa jina la Tracy Chapman, mara ya kwanza nasikia nyimbo zake ni baada ya kuwa nimemsikia Karola Kinasha na nilijikuta navutiwa na nyimbo zake na zaidi upigaji wake wa gitaa, na kama unavyojua kijisegment hiki ni kwa ajili ya wacharaza gitaa tu.

Ni maarufu kwa nyimbo za kisiasa na kuelezea masuala ya kijamii na kutokana na kazi yake ameshinda tuzo 4 za Grammy na tuzo nyingine nyingi ndani na nje ya USA.

Keshafanya kazi na mashirika ya kimataifa ya kupigania haki za binadamu, Mwaka 1988 katika kuadhimisha miaka 40 ya Tamko la Umoja wa Mataifa la Haki za Binadamu (UDHR) alitumbuiza jijini London chini ya Amnesty International, na mwaka huo huo alitumbuiza katika kukumbukumbu ya kuzaliwa Nelson Mandela.

Nyimbo zake maarufu ni pamoja na ninaoupenda zaidi, 'talking about revolution', Fast Car, For My lover, Matters of the heart, let it rain na ambao nitaupandisha leo 'give me one reason'. Wimbo wa Fast Car ningependa uutafute na usikize gitaa linavyodonolewa kufuatisha maneno yenye kusisismua bongo.

Tracy keshatumbuiza na wapiga gitaa maarfufu duniani akiwemo BB King, Buddy Guy, Eric Clapton na pia kina Ziggy Marley pia na muitaliano Luciano Pavarroti.

...ana msemo wake ninaoupenda ' kama kuna watu wanadhani una nafasi ya kutoa mchango wako, basi toa, ni kitu kizuri kufanya.

Mwangalie hapa katika clip ya YouTube akicharaza gitaa na gwiji Eric Clapton.



Hadi wakati mwingine, twe na usiku mwema

Asante Obe, jamaa yuko vizuri aisee
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom