Michael Ballack - Namba 13
Ballack alikuwa anamhusudu sana mshambuliaji wa zamani wa Ujerumani, Rudi Voller ambaye alikuwa anava jezi namba 13. Hivyo Ballack aliposajiliwa na Bayer Leverkusen, alimkuta Rudi Voller ndio mkurugenzi wa Michezo wa klabu hiyo, Ballack akashauriwa kuvaa namba 13. Kumbe alichagua namba ya mkosi bila kujijua.
Bayern Munich
Ujerumani
Bayer Levekusen
Chelsea
Aliposajiliwa Chelsea alikuta namba 13 inavaliwa na William Gallas, yeye akaomba namba 13 kama sehemu ya mkataba wake inavyosema.
Hivyo Gallas akanyang'anywa namba 13 ili apewe Ballack, kitendo hiko kilimchukiza Gallas akaomba kuhama na kutua Arsenal.