Mtumishi. Majaribio ya aina hii ni unethical kwa sababu implications zake ni hatari mno. Cross-breeding, DNA crossing/splicing na uhamishaji huu wa seli za ubongo hautakiwi kuachiwa tu ufanyike kiholela. Kuna siku atatokea rogue scientist huko North Korea achanganye DNA ya simba na binadamu kwenye lab ili kuzalisha wanajeshi wasioogopa halafu atuletee matatizo. Kama binadamu hatupaswi kuingilia uumbaji wa Mungu na kuanza kuhamisha DNA hovyo hovyo lakini huko ndiko tunakoelekea kwa sababu tiba za magonjwa mengi inaonekana zimejificha katika DNA na kwa kadri siku zinavyokwenda wanasayansi wanadai itafikia mahali wataweza kuzalisha binadamu asiyeugua wala kuzeeka.
Kama leo tunaweka brain cells za binadamu kwenye ubongo wa panya, vipi tukiweka kwenye ubongo wa simba au tiger? Tunacheza na moto![emoji291][emoji291][emoji291][emoji291]