Makapuku Forum

Nyuzi Time!

Wakati mwingine tena tusikize nyuzi za gitaa kama zinavyokuwa zinasikika katika muziki mtamu tunaoupenda, na hata kama hatuupendi, nakukaribisha kusikiza gitaa tu.

Leo tumwangalia Bill Withers, huyu ninaweza kumwandika kila wiki na wala usichoke kusoma au kusikiliza nyimbo zake. Ni mwanamuziki, mwandishi wa nyimbo, mpigaji wa gitaa na muongozaji wa muziki.

Sawa, anaweza kuwa mpya kwako kwa jina, lakini nina uhakika kuna nyimbo za kina Michael Bolton, Mary Blige, Will Smith, Akon, DMX na wanamuziki wengine zaidi ya 250 duniani ambao wamerudia kuimba nyimbo zake. Unashangaa, ndiyo, hadi Michael Jackson kaimba nyimbo za gwiji Bill Withers. Clinton na Obama walijaribu kuimba pia (hawakurekodi -usijenitoa macho na source blah blah)

Mshindi wa tuzo kibao za Grammy, kuanzia wimbo Ain't No Sunshine (1971), Just The Two of Us (1981), Lean On Me (1987).

Ana nyimbo nyingi nzuri na bado nukuu yake ' Unapoiangalia dunia na masuala yanayoendela kwa kutumia kioo, hutakuwa timamu, utajiona mwenyewe na vichache vilivyo nyuma yako. Fungua dirisha uweze kuona mengi, tizama.

Niko huku niliposema nitakuwa leo furahiday, nagonga moja moja huku namsikiza gwiji wa kukopi nyimbo za zamani (sio Zahiri Zoro baba wa Banana Zoro - huyu utampenda akiziimba nyimbo hizi na gitaa lake la nyuzi sita), na bila hiana nikaomba wimbo huu naouweka hapa kama nilivyoutoa katika clip ya YouTube.

Burudika.


Ninaamini mjombaangu lee empire (hivi anajua kama nina saa, wiki ya pili sasa!?)anauimba wimbo huu kwa ajili ya Shunie
 

May 14
Spurs v Man Utd
Itakuwa ndio mechi ya mwisho kuchezwa White Hart Lane baada ya kutumia kwa miaka 118
Nsimu wa 2017/18 Spurs wataanza kutumia uwanja mwingine....kwahiyo United tukomae tuuage uwanja wao kikauzu
.........
 
AJ atakasambaratisha haka kazee round za mwanzoni kabisa
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…