Makapuku Forum

Muungano umewachosha kwa kiasi kikubwa sana Wazanzibar.

Hata hayati Abeid Karume aliwahi kusema Muungano ni kama koti hivyo likikubana huna budi kulivua.

Maneno hayo ya kejeli ya Karume kwa Nyerere yalimchafua mno Nyerere na wawili hao hawakuwa na uhusiano mzuri katika siku za mwisho za maisha ya Karume.

Pia Rais wa awamu ya pili ya Zanzibar, ndugu Aboud Jumbe Mwinyi alipohoji kuhusu muundo wa Muungano na kujaribu kuandaa hati za mashtaka kwaajili ya kuuvunja Muungano alijikuta akilazimishwa kujiuzulu nyadhifa zake zote ndani ya chama na serikali na alipojiuzulu tu 1984 akawekwa kizuizini nyumbani kwake Kigamboni mpaka alipofariki mwaka jana.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…