Makapuku Forum

Nashukuru sana Mamndenyi

Ila bado tarehe 20 October kufikia
 
Hongera mashujaa
 
Mamndenyi ubarikiwe karibu
 
Ana mawe!!!
 
NUKUU YA LEO

We can not hope to solve our problems by pretending they do not exist


Hatuwezi kutatua matatizo yrtu kwa kujidanganya hayapo

Haya maneno yalipatwa kutamkwa na Baba wa Taifa la Tanzania Hayati Mwalimu Julius kambarage Nyerere aliezaliwa 13/04/1922 huko Butiama, mkoani Mara nchini Tanganyika.

Mwalimu Nyerere alifariki tar. 14/10/1999 akiwa na miaka 77.

Nyerere anakumbukwa kwa mengi Hapa Tanzania, Africa na Dunia nzima kwa simamia haki na usawa kwa watu wote..

Hayo maneno alitamka akimaanisha kukubali kuwepo kwa changamoto/matatizo ndio njia ya kuyatafutua ufumbuzi na jamaa inajua kuwa kuna changamoto kadha wa kadha za kutatuliwa.


Hili liko tofauti na Uongozi wa sasa hivi..Uongozi wa Tanzania baada ya miaka 50.

☞Sasa hivi kuna Hali ya njaa kwa wananchi ila viongozi wanadai Hakuna njaa nchini

☞Sasa hivi kuna upungufu wa Dawa hospitalini lakini Viongozi wetu wanadai kuna dawa za kutosha

☞ sasa hivi kuna changamoto ya Nishati hasa umeme na gesi ila utasikia tuna umeme wa kuuza kwa nchi jirani.


Taifa linahitaji uwazi na uwajibikaji wa kila mwananchi ili tuweze kufikia malengo yetu.


Mungu Ibariki Afrika,

Mungu Ibariki Tanzania.


Mchana mwema.
 
Seeing the invisible.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…