Makapuku Forum

hahaha Makapuku mimi huwa mbona jukwaa lenu hili najaribu kulielewa lakini nashindwa? Hivi huwa mnajadili mada fulani au kuna mtiririko wa story maana mnaniacha kwenye mataa ....ila ninachoelewa kutoka kwenu ni kuwa mnatoa like kama njungu vile na kingine kinachonishangaza ni uzi wenu unavyokimbia kama marathon vile....
 
 
huwezi kuelewa kama unachungulia na kupita we kaa kalibia week usome kimya kimya utaelewa tu
 
Week end nyingine tena, siku ya kifamilia. Najua kuna mapya mengi kwenu, ila kwangu, nimenunua saa mpya. Sio jambo baya family ya Makapuku kujua.

Turudi kwenye nachopenda, nyuzi za gitaa.

Filamu ya Neria ni maarufu sana hapa Tanzania na duniani kote, ni moja ya filamu zilizopata maarufu mkubwa miaka ya 90s. Ukiacha wahusika, na mandhari, soundtrack ya Neria ilitungwa, kuandikwa na kuchezwa na gwiji Oliver "Tuku" Mtukudzi.

Mshindi wa muda wote wa Tuzo za Kora, Tuku ni mwandishi mzuri wa mashairi 'poems' na litunukiwa tuzo ya International Writers Project inayotolewa na Brown university.

Hapa mcheki akicharaza gitaa lake lililotawala wimbo wa Neria katika mwaliko maalum alioupata pale Bush House studios za BBC.

Usiku mwema

 
asante mkuu
ulale vyema
 
hahahhahh binamu hongera kwa kununua saa mpya
filamu ya neria naikumbuka yule mama mjane masikini alivyoanza kunyanyaswa na ndg wa mume

asante binamu kwa gitaa la mzee Oliver
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…