Makapuku Forum

Makapuku Forum

Kilichoandikwa na gazeti la jamhuri kuhusu vifo vya askari wetu 8..

5eacbb858626cfc89923819261d36344.jpg


Matukio ya ujambazi wa kutumia silaha, mauaji ya polisi na viongozi wa vijiji katika wilaya za Mkuranga, Kibiti na Rufiji mkoani Pwani, yanahusishwa na vikundi vya vijana wanaopata mafunzo kutoka kwenye kundi la al-Shabaab nchini Somalia, JAMHURI limefahamishwa.

Kwa miaka minne hadi mitano iliyopita, vijana kadhaa kutoka maeneo mbalimbali ya Wilaya ya Rufiji, hasa Ikwiriri, wamekuwa wakisajiliwa na kundi hilo la kigaidi, huku wazazi wao wakiambulia ujira wa dola 3,000 za Marekani (zaidi ya Sh milioni 6).

Akizungumza na JAMHURI, mmoja wa wakazi wa Ikwiriri ambaye hakupenda kutajwa jina lake gazetini kwa sababu za kiusalama, amesema kumekuwa na wimbi la vijana wenye umri wa miaka 16-25 kupelekwa kwenye mafunzo huko Somalia.

“Hapa Ikwiriri katika kipindi cha miaka kama mitano iliyopita kumekuwa na wimbi la vijana wadogo kupelekwa Somalia. Inasemekana wanakwenda kujiunga na kikundi cha al-Shabaab, lakini vijana hao wamekuwa wanapatikana kupitia kwa mawakala kadhaa kwenye misikiti.

“Si kweli kwamba polisi hapa Ikwiriri hawajui, maana hata ukifuatilia wale viongozi wa vijiji ambao wamekuwa wakitoa taarifa za vijana hao wamekuwa wakiuawa kwa staili inayofanana… sasa hapo unaweza kuona namna zoezi linavyokuwa gumu,” amesema.

Chanzo chetu kingine kimemtaja mtu ambaye jina lake tunalifupisha kwa kifupi kama S.B., kuwa ndiye hufanya kazi ya udalali wa kuwapeleka vijana hao nchini Somalia, huku wazazi wa watoto hao wakiambiwa kuna kazi wanakwenda kuifanya huko.

Chanzo hicho kimesema hata baada ya baadhi ya wenyeviti wa vijiji kupeleka taarifa za uhusika wa S.B. kilichofuata ni mauaji.

“S.B. alipotea hapa Ikwiriri kwa takribani miaka mitatu, hata baada ya kurejea amekuwa na mali nyingi. Mali ambazo si za kurithi na haziendani na utafutaji wa halali katika kipindi hicho kifupi. Yamekuwa yanasemwa mengi, lakini ukimgusa andaa sanda kabisa,” kimesema chanzo chetu.

Chanzo chetu kimeliambia JAMHURI kuwa vijana zaidi ya 27 kutoka maeneo mbalimbali wilayani Rufiji, wamechukuliwa kwenda kujiunga na al-Shabaab, chini ya udalali wa Bwana S.B.

Chanzo hicho kimesema mmoja na vijana ambaye alichukuliwa alishindwa aina ya kazi na akarudi.

Habari ambazo JAMHURI, limezipata zinaonesha kwamba kikundi hicho cha wauaji kimekuwa kikimtumia mtoto mdogo mwenye umri chini ya miaka 18, kuwapelekea chakula huko msituni eneo la Mparange wilayani Rufiji. Jina la mtoto huyo tunahifadhiwa kwa sababu za kitaaluma.

“Kijana huyo mdogo amekuwa akitumiwa na hao wauaji kuwapelekea chakula. Mtoto huyo amekuwa akiwahudumia pasipokuwa na simu. Akikamatwa huyo anaweza kusaidia sana upelelezi wa polisi… hapa kila mtu amejaa hofu kuhusu usalama,” kimesema chanzo chetu.



Ushauri

Baadhi ya wataalamu wa masuala ya usalama waliozungumza na JAMHURI wametoa ushauri kwa Serikali wa namna ya kukabiliana na wimbi la mauaji ya viongozi na polisi yanayoendelea Mkuranga, Kibiti na Rufuji mkoani Pwani.

Serikali inashauri wa kuwahusisha viongozi wa dini na wataalam wa saikolojia katika kutatua vitendo hivyo.

Akizungumza na JAMHURI, mchambuzi wa masuala ya usalama mwenye makazi yake Johannesburg, Afrika Kusini, ambaye kwa maudhui ya kiusalama tunamtambulisha kwa jina moja la Alexandre, anasema sehemu kubwa ya Afrika Mashariki inakabiliwa na matatizo ya usalama, hivyo njia pekee ya kukabiliana na tatizo hilo ni kuzihusisha pande zote.

Alexandre, anasema kumekuwapo tatizo linalohusishwa na vitendo vya ujambazi (ugaidi) katika Pwani ya Bahari ya Hindi, ukanda wa Mombasa, Tanga, Zanzibar, Mtwara, Lindi na Dar es Salaam.

“Ninashauri kwamba mamlaka; hasa vyombo vya usalama visifikirie kuhusu ‘confrontation’ na vikundi hivyo…Polisi wanapowaua, hao ‘majambazi’ nao wanahakikisha wanalipa kisasi. Katika mambo kama hayo ni busara wanasaikolojia pamoja na viongozi wa dini wakaingilia kati.

“Wanasaikolojia wanatakiwa kufanya utafiti, kwanini matukio kama hayo yamekuwa yanajirudia katika ieneo hilo hilo katika siku za hivi karibuni? Hapo inawezakana kukawa na jambo kubwa zaidi…” amesema.

Inaendelea ....
Wengine waliouawa ni Ofisa wa Misitu ambaye alikuwa Mkaguzi wa Kituo cha Ukusanyaji Mapato ya Ushuru katika Kijiji cha Jaribu, Peter Kitundu na Rashid Mgamba ambaye ni mlinzi/mgambo ambao walipigwa risasi na walikufa papo hapo eneo la tukio.

Mei, mwaka jana Mwenyekiti wa Kijiji cha Nyambunda, Said Mbwana, aliuawa kwa risasi.

Oktoba, mwaka jana Ofisa Mtendaji wa kijiji hicho hicho, Ally Milandu, aliuawa kwa kupigwa risasi na watu wanne. Novemba, mwaka huo huo wenyeviti wawili wa vitongoji wa kijiji hicho waliuawa kwa kupigwa risasi.

Januari, mwaka huu watu ambao Jeshi la Polisi hadi sasa halijawafahamu walimuua mfanyabiashara Oswald Mrope kwa kumpiga risasi mbele ya familia yake.

Februari 3, mwaka huu watu wasiojulikana walivamia nyumba ya Mwenyekiti wa Kijiji cha Jaribu, Bakari Msanga na kuichoma moto huku yeye mwenyewe akifanikiwa kutoroka.

Matukio ya aina hii yanayotia shaka ustawi wa amani ya Tanzania, kwa mwaka 2013 yalitokea wilayani Kilindi mkoani Tanga ambako msikiti wa Madina ulibainika katikati ya pori kati ya Tanga na Bagamoyo.

Kama hiyo haitoshi, mwaka 2014 vijana waliokuwa wakipewa mafunzo ya kigaidi walikamatwa mkoani Mtwara wakiwa wanapewa mafunzo tayari kujiunga na al-Shabab.

Kenya kwa muda mrefu sasa imekuwa katika mapambano yasiyokwisha na kundi la al-Shabaab wanaoaminika kuwa wanatetea imani na Waislam nchini Somalia.

Ni kwa mantiki hiyo, matukio ya mauaji kwa mikoa ya Pwani, Mtwara na Lindi wachambuzi wa masuala ya kiusalama wameishauri Serikali kutumia zaidi diplomasia kuliko nguvu.
 
Tunakushukuru Mwenyezi Mungu Baba wa rehema asante kutuamsha salama,tunajikabidhi mikononi mwako tuongoze tutende mema na kukutii asante kwa ajili ya familia na Makapuku wote,tulinde tuongoze tuepushe na hatari zote za mwili na roho bariki kazi za mikono yetu walinde wasafiri,wajane,yatima,waponye wagonjwa wafariji wafiwa na wote wanaopitia changamoto wape wepesi na kushinda bariki marafiki na maadui tupe mshikamano asante kwa ni utatenda sawa na mapenzi yako katika jina la Yesu Amen

USHIRIKIANO

HERI WAWILI KULIKO MMOJA

MHUBIRI 4

9.Afadhali kuwa wawili kuliko mmoja ;maana wapata ijara njema kwa kazi yao.

10.Kwa maana wakianguka ,mmoja wao atamuinua mwenzake;lakini ole wake aliye peke yake aangukapo wala hana mngine wa kumuinua

Tunahitaji watu wa kutimiza ndoto zetu.

Kama tunahitaji mtu /watu basi tumuombe Mungu sana atukutanishe na:
Mtu /watu sahihi
Mahali sahihi
Wakati sahihi
Kwa utukufu wa jina lake na kwa mafanikio yetu wote.
Watu wote ni muhimu kwetu kwa nyakati tofauti,shetani huwa anatuangusha tusikutane na watu sahihi wakati sahihi.

Heshimu watu,wasiliana na watu,wapende watu,watendee mema ndugu,jamaa,rafiki,jirani,wageni,adui na wote wanaotuzunguka.

MUNGU ATUSAIDIE

MBARIKIWE SANA

SIKU NJEMA KWENU
shukran mama mchuchu ubarikiwe sana na ww
 
KITU CHA KUJIFUNZA LEO NDUGU ZANGU, KUHUSU MARAFIKI WANAOTUZUNGUKA, MAKAPUKU OYEEEE

Kuna mengi hatujui kuhusu marafiki zetu.
Kuna watu wameumizwa na marafiki zao kwa sababu hawakuwa na macho ya rohoni kuweza kuwatazama.
Kama wewe ni mmoja kati ya wale ambao marafiki wamekuwa jaribu, basi somo hili na likawe msaada kwako.

1⃣ *CONFIDANTS*
Hili ni kundi la kwanza la marafiki.
“Confidants” ni wale marafiki wanaokupenda bila masharti. Wako nawe ukiwa juu au chini, ukiwa tajiri au maskini, ukiwa sahihi au ukikosea, wako pamoja na wewe. Ukipelekwa gerezani watakufuata, ukilia watalia pamoja nawe, na ukifurahi watafurahi pamoja nawe. Ni watu ambao unakuwa huru zaidi kuwaeleza kila jambo kuhusu maisha yako (kuliko hata ndugu zako) na kwa kufanya hivyo unajikuta unafarijika na kupata amani moyoni. Hutaweza kutimiza maono yako bila kuwapata “Confidants” wako.
Confidants ndio wanaoelezwa katika Mithali 18:24; kuwa ni marafiki wanaoambatana na mtu kuliko ndugu. Mungu anakuletea watu kama hawa kwenye biashara, katika huduma, katika uongozi n.k. ili wakusaidie kwa maombi, ushauri na kukuonya, ili uweze kufanikiwa kama Mungu alivyokusudia. Ukipata wawili au watatu katika maisha yako, basi wewe ni mtu uliyebarikiwa sana, kwa sababu bila watu hawa hutaweza kuwa vile Mungu alivyotaka uwe. Usiwapoteze confidants wako kirahisi. Mungu akusaidie uwe confidant kwa mtu fulani.

2⃣ *CONSTITUENTS*
Hawa ni marafiki hatari, kwa sababu hawako kwa ajili yako, wapo kuiba maono yako. Ni wezi wa maono. Biblia inasema pasipo maono watu huangamia (Mithali 29:18); Kwa hiyo anayekuibia maono kwa lugha nyingine amekuangamiza. Unakuta binti amepata mchumba, (au hata wakaka sometimes!!!!) anamshirikisha rafiki yake kile Bwana alichomtendea, lakini baada ya muda mfupi anaachwa na anashangaa rafiki yake mtu aliyemuamini saaaaaana amemuibia mchumba. Watu wengi wameumizwa na marafiki kwa namna hii but kiukweli hawasemi tu.. Huyo alikuwa rafiki aina ya “constituent”, unachotaka ndicho anachotaka. Ole wako wewe mwenye constituent kwenye mahusiano au biashara yako ukidhani ni confidant. Ukimueleza constituent habari za mchumba wako atakuibia (abiria chunga mzigo wako!!!) Ukimueleza constituent habari za wazo la biashara unayotaka kuanzisha atakuibia hilo wazo.
Kumbuka vizuri habari za Yakobo na Esau, Yakobo alikuwa “constituent” kwa Esau, akamwibia baraka. Na Mungu amekupa marafiki kama hawa kwa lengo moja kubwa, _kukufundisha kwa vitendo kwamba maono yako yanaweza kuibiwa usipoyalinda_ .. Mungu akupe “MACHO” ya kuwajua constituents katika maisha yako.

3⃣ *COMRADES*
Hawa ni marafiki ambao Mungu anawaleta katika maisha yako kwa kusudi maalumu, sometimes kwa muda maalumu tu na baada ya hapo hutawaona tena. Ni watu wanaopigana na kile unachopigana nacho, kukusaidia kushinda upinzani mkubwa na baada ya hapo hutawaona tena. Sasa usipate shida wakikuacha na kuondoka, hawa hawatadumu nawe kipindi kirefu. Hawa ni kama ngazi (ladder) ambayo inahitajika sana wakati nyumba inajengwa, lakini nyumba ikishakamilika ngazi itaondolewa ila nyumba itabaki.

Simoni mkirene alionekana tu wakat wa kumsaidia Yesu msalaba na kuufikisha Golgotha, baada ya hapo hatujui alielekea wapi (Mt 27:32). Pia kumbuka Yonathani alivyomsaidia Daudi kupigania nafasi yake ya ufalme, na baadaye tunaambiwa Yonathani mwenyewe akafa muda mchache kabla hata Daudi hajalipa fadhila (2 Sam 1:26), kwa sababu Yonathani alikuwa Comrade wa Daudi. Huwezi kuwa Daudi bila kumpata Yonathani wako!! Pia kumbuka namna Filipo alipomsaidia Towashi wa Kushi kuokoka. Baada tu ya kumbatiza, Biblia inasema Filipo akachukuliwa na Roho mtakatifu. Comrades si marafiki wa kudumu.

NB.
Wako marafiki wengine hawako kwenye kundi lolote kati ya hayo niliyoyataja hapo juu.
Hao nawaita “wrong partners”. Hutaweza kufika unakokwenda usipojitenga nao mapema. Mkumbuke Yona. Watu wote kwenye meli wangeangamia kama wasingemtupa Yona baharini. He was a wrong partner (japo ni mtumishi wa Mungu). Mtupe Yona wako, ili ufike salama. Kuna huduma zimekwama, kuna makampuni yamerudi nyuma, kuna biashara zimefilisika kwa sababu wamembeba Yona bila kujua atawaletea shida safarini.. mtupe
Yona wako, Tafuta Confidants wako,..
Much love to YOU guys In Here Makapuku oyeeee
Baba paroko ubarikiwe sna hilo kundi la kwanza aisee nina rafiki zangu zaidi ya ndg Mungu azidi kuwaweka
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom