Mungu Baba Mwenyezi ,asante kwa siku njema ya leo tunajikabidhi mikononi mwako usiku wa leo utuondoe katika hatari za mwili na za roho,ponya wagonjwa,fariji wafiwa,watie moyo wajane,wagane na wapweke,walinde wasafiri majini,nchi kavu na angani Baba tunakuomba tusamehe yote tuliyokosa kwa mawazo,maneno na matendo uturehemu twakusihi na utuamshe tukiwa na nia njema ya kukutumikia.
Malaika walinzi waweke kituo kwa kila mmoja wetu Damu takatifu itufunike tunaomba yote kwa jina la Yesu Kristo Mpatanishi na Mwokozi wetu Amen

Mithali 18
10. Jina la BWANA ni ngome imara; mwenye haki huikimbilia, akawa salama.
MUWE NA USIKU MWEMA,NJOZI NJEMA,MLALE SALAMA.