Makapuku Forum

Wadau, tunaendelea tena na kipengele cha muziki hususani upande wa nyuzi aka gitaa. Na bado tuko Magharibi mwa Afrika.

Tunamwangalia nguli wa gitaa na muziki aliyejulikana sehemu nyingi ulimwenguni, huyu ni Ali Farka Toure, mshindi wa tuzo ya Grammy, ndiyo Grammy mwaka 1994 akishirikiana na Ry Cooder. Na sio Grammy moja tu, alishinda tuzo hizi mara mbili.
Ali Ibrahim Farka alijulikana kama 'godfather of the desert blues", kwa mujibu wa gazeti la The Guardian la Wednesday 8 March 2006 10.40 EST.
Ali Farka alifariki mwaka 2006. na kwa kuheshimu mchango wake, radio za serikali zilisitisha matangazo mengine na kucheza nyimbo zake siku nzima.


Hii hapa ni clip toka YouTube hapa akitumbuiza na gwiji la kora Toumani Diabaté


Hadi wakati mwingine tena, kwa wale wapenzi wa sauti za 'magitaa'
 
Mpendwa Bwana Yesu ,kama vile kuku awafunikavyo vifaranga wake kwa mbawa zake ili kuwaweka salama ,tulinde sisi Makapuku popote kila mmoja alipo usiku huu,chini ya mbawa zako za huruma ,Damu yako ya thamani inene mema kwetu itufunike..malaika walinzi waweke vituo kwa kila mmoja wetu na familia zetu..Amen

Usiku mwema wapendwa mbarikiwe
 
Jifunzeni tu kutumia "search" kutafuta mambo muhimu mnayoyapenda mfano magazeti, historia, nukuu n.k
Kurudia kupost kitu ni kujaza tu thread
Thread yenyewe ina post za kufa mtu
........
 
Homegirl punguza jazba..hutaniwi na wewe chalii ake
 
Naanza kuzipenda sasa...
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…