Makapuku Forum

Makapuku Forum

Leo katika Historia:

1922 - Simon Kapwepwe anazaliwa.

Alikuwa ni Makamu wa pili wa Rais nchini Zambia.
f4ea55d1756ebe01d879135f45c6c514.jpg
892b9f1c07ebb5e1f8884a2bb07f7482.jpg
952c6d547712eb2a64b528fafa36f5ef.jpg

Jina na sura km Kipepe vile
..
 
1941 - Bobby Moore anazaliwa.

Beki na kepteni wa zamani wa West Ham na timu ya taifa ya England.

Ndio kepteni pekee wa England kubeba kombe la Dunia walipofanya hivyo mwaka 1966 katika mashindano yaliyofanyika kwao Uingereza.

Ndio kepteni mdogo zaidi katika historia ya Soka la Uingereza baada ya kupewa Unahodha akiwa na miaka 22 tu.

Alifariki Dunia mwaka 1993, kwa heshima yake Jezi namba 6 haivaliwi tena kwenye klabu ya West Ham.

Waingereza wamejenga sanamu yake nje ya Uwanja wa Wembley kama njia ya kumuenzi.
 
1948 - Marcelo Lippi anazaliwa.

Kocha wa zamani wa Juventus, Inter Milan, Napoli, timu ya taifa ya Italy na sasa timu ya taifa ya China.

Ndio Kocha aliyewapa Italy Kombe la Dunia la Mwaka 2006 katika mashindano yaliyofanyika Ujerumani ambapo Fainali Italy anamfunga Ufaransa kwa matuta.
 
1969 - Lucas Radebe anazaliwa.

Beki wa kati wa zamani wa Kaizer Chiefs, Leeds United na timu ya taifa ya Afrika Kusini.

Ni wakati alipokuwa Leeds United iliyokuwa inashiriki EPL, Radebe alijitengenezea Jina kubwa katika Dunia ya mpira.

Alichaguliwa kuwa kepteni wa Leeds United na kumfanya kuwa Mwafrika wa kwanza kuwa nahodha katika timu ya ligi kuu Uingereza. Alikuwepo kwenye kikosi kilichofika nusu fainali ya Uefa Champions League mwaka 2001 akiwa na akina Rio Ferdinand, Alan Smith, Mark Viduka, Harry Kewell nk

Alitwaa ubingwa wa mataifa ya Afrika mwaka 1996 katika ardhi ya Nyumbani.
 
Ilikuwa usiku, hatimae kumekucha!ni upendeleo tuu wa Mwenyezi Mungu kwa majaaliwa haya, sifa na utukufu ni zake,tuzidi kuomba huruma zake atujaalie kutumia wakati kwa kutenda yampendezayo ili kupata kheri duniani na kesho kwenye ufalme wake, nawatakia wepesi ktk kazi za mikono yenu,siku njema!
Milele aminaa
 
1941 - Bobby Moore anazaliwa.

Beki na kepteni wa zamani wa West Ham na timu ya taifa ya England.

Ndio kepteni pekee wa England kubeba kombe la Dunia walipofanya hivyo mwaka 1966 katika mashindano yaliyofanyika kwao Uingereza.

Ndio kepteni mdogo zaidi katika historia ya Soka la Uingereza baada ya kupewa Unahodha akiwa na miaka 22 tu.

Alifariki Dunia mwaka 1993, kwa heshima yake Jezi namba 6 haivaliwi tena kwenye klabu ya West Ham.

Waingereza wamejenga sanamu yake nje ya Uwanja wa Wembley kama njia ya kumuenzi.
950995088d5cdb1ff56a7351129e1c83.jpg
2fa1d68119b2263074cf5f0e5a8a0f53.jpg
a4478866063c056771a276ad22b6eba7.jpg
9ad4f177c90ad258d9ce6d01f3a93cab.jpg
Ubingwa wenyewe wa mbeleko....watachukua tena siku wakiwa wenyeji
....
 
NUKUU YA LEO

Someone is sitting in the shade today because someone planted a tree a longtime ago

Kuna mtu amekaa kwenye kivuli leo kwa kuwa kuna mtu alipanda mti siku nyingi


Haya maneno yalipatwa kusemwa na mwekeaji, mfanyabishara wa kimarekani Warren Buffett aliyezaliwa 30/08/1930 ktk jiji la omaha, Nebraska nchini marekani.

Buffet kwa sasa ni tajiri no. 2 akiwa na utajiri unaokadiriwa kufikia $ 75.6 billion.

8e5dd367a07e0bc0da13ec029bcbca82.jpg


Buffett ni mkurugenzi na mmiliki wa makapuni ya Barkshire Hathaway yenye makao makuu mji wa omaha, Nebraska.
6645d6d84d034b32a6e9b6fe35619126.jpg


7b57092c6a684924dac82790abef4c83.jpg


Morning motivational.

Buffet anazungumzia maisha ya baadaye, ili uweze kuwa na maisha mazuri lazima uwe na maadalizi sasa hivi..

Panda mti leo ili kesho ufaidi kivuli chake, panda mti ili ufaidi matunda yake..

Transcend.
Ujumbe mzur

Uwe na siku njema
Cc:mshauri
 
1948 - Marcelo Lippi anazaliwa.

Kocha wa zamani wa Juventus, Inter Milan, Napoli, timu ya taifa ya Italy na sasa timu ya taifa ya China.

Ndio Kocha aliyewapa Italy Kombe la Dunia la Mwaka 2006 katika mashindano yaliyofanyika Ujerumani ambapo Fainali Italy anamfunga Ufaransa kwa matuta.
0f01cd881a16aa31f9d05a5b731ce010.jpg
09d0ce543d5954a8410c4d87f783d294.jpg
4a1af61e63e5a8ac8eddee735d581e52.jpg
Nakumbuka zaidi tukio la Zidane kumtwanga kichwa Materazzi na kupigwa RED CARD
Italy ilishinda kwa penalties
....
 
1984 - Edward Sokoine anafariki Dunia katika Ajali ya gari huko Dumila, Mkoani Morogoro.

Leo ni miaka 33 tokea kifo chake.

Alikuwa ni Waziri Mkuu wa Tanzania mara mbili, kipenzi cha Wanyonge na watanzania wengi.
Vita yake dhidi ya Uhujumu Uchumi ilipamba moto kiasi cha kufanya walanguzi kumuogopa vibaya.

Alifariki baada ya gari alilopanda kupata ajali ya kugongwa na gari la Mkimbizi wa Afrika Kusini aliyejulikana kama Dumisane Dube.

Alitajwa kama mtu ambaye angemrithi Nyerere kwenye Urais mwaka mmoja baadae 1985 mara baada ya Nyerere kutangaza kung'atuka.

Ajali yake mpaka leo imebaki kuwa na utata wa hali ya juu.

Chuo Kikuu cha Kilimo na Ufugaji mjini Morogoro, Sokoine University of Agriculture ( SUA ) , kimepewa jina lake kama kumuenzi.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom