Makapuku Forum

Makapuku Forum

Yanga
Zanaco

*Msuva 39'
*Nanihii 77'
.......
Mchezo huu ulikuwa ni mchezo mgumu sana kwa Yanga kama mwenyeji ila pia ni mchezo wa majukumu zaidi wa Zanaco..... Kuanzia katika eneo la kiungo cha kati lililo chini ya Moyo mpaka upande ule wenye Saith Sankala ni sehemu hatari zaidi na za kutaftia plan nyingi zaidi kwa GL.

Thaban Kamusoko ni miongoni mwa key player wa kikosi cha Yanga, ni mmoja wa viungo wanao kuwa wazuri zaidi pale mpira unapokuwa katika miguu yake..... Anatoka katika majeruhi na anakosa match fitness na kuingia moja kwa moja kwenye mchezo na kuonekana dhahiri shahiri kuzidiwa na kiungo rasta mwenzie wa Zanaco Moyo.

Njia ngumu kabisa Yanga wanayopita ili kuvuka hatua inayofuata basi ni njia ya Zanaco... Ile ball control, mpira wa kasi na physic ni kitu walichokuwa nacho wazambia ila pia ndicho kitu walichokikosa Yanga..... Walichokikosa Zanaco ni hesabu za kufungua eneo la mwisho la beki za Yanga....

Pasi aliyoipiga Zulu ilimhitaji Zulu peke yake na utulivu wa aina ile kwenye eneo kama lile na wakati kama ule..... Hii ndio pasi yenye akili, ubora na yenye macho katika pasi zote kwa timu zote katika mchezo huu...... Ile pasi inamtambulisha Zulu kama professional player.

Bado Yanga walikosa na kumhitaji haruna sana ili Msuva apete ile mipira yake...... Kumtumia Kelvin kama kiungo wa chini mbele ya Nadiri na Bossue kwa asilimia kubwa kuliwafanya wazambia kushindwa ku unlock mipango ya beki ya Yanga pamoja na wazambia ku dominant mchezo.

GL kabla hujaenda Zambia fanyia kazi mipira ya mwisho na ball control kwa wachezaji wako...... Tofauti na hivyo Zambia panaweza kuwa pagumu sana.... Pale Zambia unahitaji pasi za Zulu kama za Leo nyingi zaidi katika eneo la mwisho la Zanaco kuliko shoot off target za Emanuel Martin.

Faida na hasara waliyonayo Yanga ni kuwa wanacheza faulu nyingi nje ya eneo lao la hatari, lakini pia wazambia nao hawajui namna ya kuzitumia..... out of that Yanga wamecheza vizuri sana kutokana na ugumu wa mchezo husika tangu kipenga cha mwanzo mpaka mwisho.

Sare ilhii inaweza isiwe nzuri sana kwa Yanga kutokana na kwenda kuimalizia mchezo wa mwisho pale Zambia.

Naulizia tu bei ya Yule rasta wa Zanaco Moyonamba 4, na Yule winga Sankala namba 7....?

Yanga 1-1 Zanaco.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom