Makapuku Forum

1945 - Katika Vita kuu ya Pili ya Dunia: Ndege za Kijeshi za Marekani zashambulia mji wa Tokyo huko Japan na kuua takribani watu 100,000 wengi wao wakiwa ni wanawake na watoto.

Huo ulikuwa ni mfululizo wa mashambulizi wa ndege za kivita za Marekani katika anga la Japan kwa kutumia ndege aina ya B-29.
 
1952 - Fulgencio Batista anaongoza mapinduzi nchini Cuba na kujitangaza kama Rais wa Nchi hiyo ambapo aliongoza kidikteta.

Batista alikuwa ni kibaraka mkubwa wa Serikali ya Marekani.

Alikuja kutolewa madarakani katika Mapinduzi ya mwaka 1959 yaliyoongozwa na Wazalendo akina Fidel Castro, Camilo Cienfuegos, Huber Matos, Raul Castro, bila kumsahau baba wa mapinduzi hayo, Muargentina Ernest Che Guevara.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…