Makapuku Forum

Makapuku Forum

1965 - Bendera ya sasa ya Canada yaanza kutumika kwa mara ya kwanza.
3b3f48b5403aba49d471c412b39d109c.jpg
1afe636034f46c1bf5b6c44f689f78df.jpg
 
Paris sent German walianza kukabia juu kabisa ya eneo la Fc Barcelona.... Unapokabwa kuanzia juu kabisa ya eneo lako unakosa muda wa kupanga mashambulizi sambamba na kukosa nafasi ya kuanzisha mashambulizi kuanzia katika back line yako.... Barcelona walianza kufa kuanzia katika mipango ya kuanzisha mipira......

Iniesta, Neymar, Suarez na Mesi hawa ni 4 ambao ni wazuri sana wakati timu inamiliki mpira ila sio wazuri sana with wakati timu inautafuta mpira..... Hapa unaona Cavan pekee ndiye mchezaji ambaye anakuwa freeman wakati wa kukaba.

Kiungo cha Barcelona kinafia kwanza kwenye miguu ya Verate na Rabiot wakati PSG wakiwa na mpira lakini pia kiungo hichohicho cha Barcelona kinafia kwanza tena kwenye mapafu ya Matuid na Rabiot wakati Barcelona wanamiliki mpira....... Hapa wale 4 wa Barcelona ambao ni sio wazuri wakati wa kukaba wanakuwa mzigo kwa mabeki wao watano na kurahisisha mashambulizi katika lango lao Barcelona. Kushambulia kwa kushtukiza kwa haraka zaidi kuliwafanya Barcelona Wengi wakutwe mahala ambapo hawakustahili.

Ili MSN ife basi huna budi kuua kwanza mipango yooote ya kuanzisha mashambulizi kuanzia nyuma (hapa Unai Emery alifanikiwa)...... Ili MSN ife basi ni lazima uzibe mianya yote ya uzawa wa pasi zinazotakiwa kumfikia Eng. Mesi (kama PSG walivyofanya klna kufanikiwa kuziba mianya yote ya pasi zilizokuwa zikielekea kwa mesi...... Ili MSN isifanye kazi basi unahitaji viungo wenye pump yenye horse power kubwa katika defensive na offensive kama Verate, Rabiot na Matuid dhide Iniesta, Bosqute na Gomes....

Unai Leo atalala na suti..... Hichi alichokifanya Leo akiwa na jezi ya Emirate kifuani ndio aina ya vitu PSG walikuwa wanavikosa.... Kumfunga Barcelona unaweza ila goli nne ni anguko la kitaaluma na mbinu za makocha haswaa Unai Emery.

Mipira aliyopiga di Maria ni kama inafanana....magoli aliyoyafunga di Maria ni kama yanafanafa..... Draxler too much pace alafu inafuata poor last touch. Hakukua na namna kwa jinsi Barcelona walivyoshindwa kuwa na plan nyingi nje ya camp Nou...... Hapa Barca walikuwa na

Mipira inapokufa kwa Leonel Mesi basi na Luis Suarez na yeye na nafasi zake hupotea mazima..... Neymar naye akafa na aina yake ya uchezaji ikafa... Ubaya wa MSN ni kama mafiga likifa moja hayo mengine hayafanyi kazi.....

Sory Barcelona Naulizia tu bei ya Yule Rabiot...? anafanya interception, blocking na ana drive timu mbele kwa wakati mmoja, anapokonya sana mipira na Sprint za nguvu......

Paris Sent German 4-0 Fc Barcelona.
Aisee umewagusa watu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom