Makapuku Forum

Ndo tabu ya kuongozwa na MASKINI
*Mikopo kwa waliosoma private kabana
*Ajira kabana
*Matumizi kabana
Anaonyesha chuki za waziwazi kwa matajiri na watu wa kipato cha kati kwavile yeye kapitia maisha ya kuchunga ng'ombe
...
Baseless generalizations! Ng'ombe tumechunga. Mamvi mpaka leo anachunga. Wakati mwingine ni falsafa tu ya mtu na watu wa aina yake waliopata bahati ya kusoma falsafa za akina Marx na kusomeshwa na kukulia enzi za Nyerere hakuna cha kushangaza.

Inabidi pia tukiri kuwa alipewa nchi ambayo ilikuwa haina mwelekeo na ufisadi ulikuwa umezidi mno - tena wa waziwazi kabisa. Sinema ya Escrow inayoendelea kuitafuna TANESCO mpaka leo itakuja kuvishangaza hata vizazi vijavyo. Amefanikiwa kubadilisha mwelekeo wetu na nidhamu imerudi. Hii haikuwa rahisi lakini imewezekana. Ingependeza sana kuanza kuona mwelekeo wa nchi mpya na vigezo vipya vikiwekwa wazi. Tatizo sasa hata huwezi kujua kinachoendelea na hata vipaumbele vyetu havijulikani. Pengine anajaribu kufanya mambo mengi sana kwa wakati mmoja badala ya kuchagua jambo moja au mawili muhimu na kupambana nayo kufa na kupona (mf. elimu, kilimo nau viwanda). Hapa ndipo penye tatizo kubwa, kwa maoni yangu. Hatujui kinachoendelea na watu subira inakaribia kuwaishia. Inaonekana kama vile tumegota mahali!
 
Umechambua vizuri, lakini mtu ambaye haheshimu raia na sheria ni janga kwa taifa, yeye kila mtu kwake ni kumuwazia mabaya
 
Uchambuzi nzuri
Hivyo ndo shida kipaumbele chake ni viwanda lakini hadi sasa porojo zimekuwa nyingi
Ikifika 2019 tutaona mwelekeo
......
.
 
Umechambua vizuri, lakini mtu ambaye haheshimu raia na sheria ni janga kwa taifa, yeye kila mtu kwake ni kumuwazia mabaya
Unajua. Wanahistoria wanaweza kukupa mifano mingi ya viongozi waliopindisha sheria ili kuweza kuleta mabadiliko waliyoyataka. Historia ina huruma sana kwa viongozi waliofanya hivyo ili kuleta mabadiliko chanya kwa watu wao. Kwa bahati mbaya mifano mingi ni negative na wengi baada ya kuonja absolute power iliwawia vigumu kurudi nyuma kwenye utawala wa sheria na nidhamu. Na hawa historia ina tabia ya kuwatupa katika shimo la takataka!

Jambo linalonishangaza mimi na hata kunitia wasiwasi ni kutojali hata pale ambapo angeweza kujipatia pointi za bure kisiasa. Mfano, mambo yaliyofanyika baada ya tetemeko la ardhi Kagera yalinishangaza sana. Anyway, tumo barabarani na safari ni lazima iendelee. Si vibaya wasafiri wakilisimamisha gari na kudai waelekezwe wapi wanapelekwa hasa kama wanahisi wanakopelekwa ndiko-siko. Ni haki yao!
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…