Makapuku Forum

Makapuku Forum

Tafakari ya kirat;
01b2853ae51e3009d87aa19849448627.jpg
 
1980 - Xavi Hernandez anazaliwa.

Kiungo wa zamani wa Barcelona na timu ya taifa ya Spain.

Anatajwa kama kiungo bora kabisa wa kati kuwahi kutokea katika mchezo wa soka. Pia alikuwa ni muhimili wa mfumo wa tiktaka, mfumo wa kupiga pasi uliokuwa unachezwa na Barcelona na timu ya taifa ya Spain kuanzia mwaka 2008-12.

Ameshinda kila taji kwa upande wa klabu na timu ya taifa.

Tuzo pekee aliyoikosa ni Ballon D'or ambapo bila shaka FIFA walimuhujumu yeye pamoja na Iniesta.

Kwangu mimi yupo kwenye First Eleven yangu bora ya wakati wote.
 
1984 - Robinho anazaliwa.

Ni mwanasoka toka nchini Brazil.

Wakati anachipukia alitajwa kama nyota hatari atakayekuja kuuteka mchezo wa soka, lakini ameshindwa kuonyesha uwezo wake na sasa mpira unaeleka mwishoni kwani umri ushaanza kumtupa mkono.

Alipitia klabu kama Man City, Real Madrid, Ac Milan nk
 
1967 - David Ginola anazaliwa.

Winga wa zamani wa Newcastle United, Tottenham na timu ya taifa ya Ufaransa.

Anatajwa kama sababu ya Ufaransa kushindwa kufuzu kombe la Dunia la mwaka 1994, baada ya Ufaransa kufungwa mechi ya mwisho ya kufuzu 2-1 na Bulgaria.

Mpira ukiwa unaelekea dakika za lala salama, alipewa pasi akaipoteza wapinzani wakachukua mpira wakaenda kufunga, Ufaransa akashindwa kufuzu. Akalaumiwa sana na Kocha wake wa wakati huo Gerald Houllier.
Mtukutu
 
1980 - Xavi Hernandez anazaliwa.

Kiungo wa zamani wa Barcelona na timu ya taifa ya Spain.

Anatajwa kama kiungo bora kabisa wa kati kuwahi kutokea katika mchezo wa soka. Pia alikuwa ni muhimili wa mfumo wa tiktaka, mfumo wa kupiga pasi uliokuwa unachezwa na Barcelona na timu ya taifa ya Spain kuanzia mwaka 2008-12.

Ameshinda kila taji kwa upande wa klabu na timu ya taifa.

Tuzo pekee aliyoikosa ni Ballon D'or ambapo bila shaka FIFA walimuhujumu yeye pamoja na Iniesta.

Kwangu mimi yupo kwenye First Eleven yangu bora ya wakati wote.
Ni kweli walimuhujumu aisee
 
1947 - Tostao anazaliwa.

Nyota wa zamani wa Brazil, anatajwa kama mmoja ya viungo bora wa uchezaji kutoka Brazil.

Alikuwepo Kikosini wakati Brazil ikitwaa kombe la Dunia la mwaka 1970 pale Mexico. Alikuwepo na akina Pele, Jaizinho, Carlos Alberto Torres na wengineo katika timu bora kabisa kuwahi kutokea kwa mujibu wa FIFA.
f8cc7be0a0cf3ec341426c040b3a335a.jpg
dd6cf6dc0603fda346844f36bdc48dda.jpg
3559dd98185414d44984ab8dd6a4471a.jpg
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom