Makapuku Forum

Makapuku Forum

Leo katika Historia:

1974 - Pambano la ngumi la kukata na shoka lililojulikana kama " Rumble in the Jungle " kati ya Muhammad Ali na George Foreman lafanyika huko Kinshasa nchini Zaire.

Pambano hilo linatajwa kama moja kati ya mapambano bora kabisa ya ndondi kuwahi kutokea.
Ngoja niwahi youtube niucheki huu mtanange, sijui utakuepo!...
 
1960 - Diego Armando Maradona anazaliwa.

Mwanasoka wa zamani wa Napoli, Barcelona na timu ya taifa ya Argentina.

Anatajwa kama mchezaji bora wa karne ya 20.

Ametwaa kombe la dunia mwaka 1986 pale Mexico akiwa kama nahodha.

Ana heshima kubwa sana ndani ya Jiji la Naples alipochezea Napoli na ndio mji ambao alijifunza madawa ya kulevya.
 
Bila kusahau ndiye mtu maarufu wa kufunga gori la mkono
 
Remembrance Week yaanza.

Waingereza waanza kuwakumbuka mashujaa wao waliofariki vitani.

Kilele cha maadhimisho hayo ni tarehe 13 November.

Katika kipindi hiko Waingereza huvaa maua mekundu iwe kwenye suti au nguo yoyote ile ikiwemo hata jezi kwa wachezaji.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom