Bitoz
JF-Expert Member
- Aug 27, 2015
- 30,823
- 126,632
NUKUU NO 1#
Amani hupatikana unapokubali kuketi meza moja ya adui yako unayemchukulia kuliko wote
Na hapo ndipo unapoweza kumtambua kiongozi aliye jasiri
Anapokubali kuketi na adui yake kwa majadiliano maana yake ni kwamba anajiamini - na hiyo ni sifa kubwa kwa kiongozi bora
Haya yalisemwa na mwanaharakati maarufu wa haki za binadamu, Askofu mkuu Desmond Tutu wa Africa kusini.
Alizaliwa huko Klerkdorp, Africa kusini October 7,1931
Mwaka 1978 aliteuliwa kuwa katibu mkuu wa baraza la makanisa ya Africa kusini
Mwaka 1985 aliteuliwa kuwa askofu wa kanisa la Anglican jimbo la Johannesburg na mwaka 1986 akawa askofu mkuu wa Capetown - mweusi wa kwanza Africa kusini kushika nafasi hiyo
Respect
.......