Makapuku Forum

Makapuku Forum

NUKUU NO 1#

Nikitofautisha haki-jamii (social justice) na haki-sheria (legal justice)
Haki-sheria maana yake ni kila mtu ana haki sawa mbele ya sheria
Huu ni msingi wa mfumo wa kibwanyenye.

Sheria haijari wewe ni nani - masikini au tajiri _ wote mna haki sawa. Kwa mfano, haki ya kuishi.
Lakini hali halisi usawa huo ni wa kinadhalia tu,kwa sababu masikini na tajiri, kwa vyovyote vile sio sawa. Haki-sheria haiangalii hali halisi, haijali tofauti za kijamii na za kiuchumi Kati ya mtu na mtu. Kwa sababu kinacholinganishwa katika dhana hii sio ubinadamu bali ni haki

Haya yalisemwa na Profesa maarufu Issa Shivji kutoka katika mada alioiwakilisha kwenye kongamano la kuadhimisha miaka 15 ya kumbukumbu za Mwalimu Nyerere, October 17,2014.
Kongamano liliandaliwa na taasisi ya Mwalimu Nyerere (MNF)
Mwalimu wangu huyu [emoji106]
 
Back
Top Bottom