Makapuku Forum

Makapuku Forum

NUKUU NO 1#

Nikitofautisha haki-jamii (social justice) na haki-sheria (legal justice)
Haki-sheria maana yake ni kila mtu ana haki sawa mbele ya sheria
Huu ni msingi wa mfumo wa kibwanyenye.

Sheria haijari wewe ni nani - masikini au tajiri _ wote mna haki sawa. Kwa mfano, haki ya kuishi.
Lakini hali halisi usawa huo ni wa kinadhalia tu,kwa sababu masikini na tajiri, kwa vyovyote vile sio sawa. Haki-sheria haiangalii hali halisi, haijali tofauti za kijamii na za kiuchumi Kati ya mtu na mtu. Kwa sababu kinacholinganishwa katika dhana hii sio ubinadamu bali ni haki

Haya yalisemwa na Profesa maarufu Issa Shivji kutoka katika mada alioiwakilisha kwenye kongamano la kuadhimisha miaka 15 ya kumbukumbu za Mwalimu Nyerere, October 17,2014.
Kongamano liliandaliwa na taasisi ya Mwalimu Nyerere (MNF)
Shivji nae anatema cheche
 
NUKUU NO 2#

Ndoto za kuwa na Africa isiyo na ukabila haimaanishi kutokuwa na tofauti za kikabila katika Bara la Africa wala kifo cha kawaida cha kabila za asili za Africa.

Tofauti za utamaduni na lugha ni utajiri iliorithi kutoka kwa wahenga wake.
Changamoto imekuwa ni jinsi kutunza utajiri huo bila kuchochea migogoro ya kikabila na kutetelesha utaifa

Haya ni maneno kutoka kwa Profesa mashuhuri Alli Mazrui katika kitabu kinachoitwa "Julius Nyerere Africa's Titan on a global stage"
Kilichoandikwa na Profesa Mazrui pamoja na Lindah L Mhando, chini ya mada "post -Tribal Nyerere to post -Racial Obama: Comparative vision in political Leadership
Hiki kitabu kama unacho hakikisha napata copy yake
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom