Makapuku Forum

Makapuku Forum

1470748789304.jpg
 
Swahiba yangu mmoja hivi anaishi nyumba moja na wazee ambao ni wazazi wake,
Siku moja alikua yuko uwani anaoga, babaake akambishia hodi kule bafuni akimuuliza,
"Hemedi uko chooni?"
Hemedi akaona sasa mbona mzee ananiuliza swali la kijinga hivi!! ...akamjibu ufedhuli
"Baba mimi niko London, hii sauti yangu waisikia kupitia idhaa ya kiswahili ya BBC",
Baba akamwambia;
"basi nakujulisha kua mkeo ameshika simu yako anasoma massage, anaangalia hadi picha, na mpaka sasa amefungua mdomo na amekodoa macho kwa hayo anayoyaona kwenye simu yako!
Na mimi nimechukua hili taulo ulokua umefunga kiunoni na kikoi uloweka mlangoni ili leo ulale huko huko London na ujifundishe namna ya kuongea na babaako mwehu mkubwa wewe...
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom