Makapuku Forum

Makapuku Forum

SEHEMU YA SITA
SEHEMU YA SITA
AKILI ilikuwa imesimama na si haba nilielekea kuwa mwendawazimu huku nilichokumbuka pekee ni midomo yangu kutetemeka huku nikimtaja Eva na mama yake. Mizimu niliyoiomba haikuniletea muujiza wowote.
Mlinzi Yule aliendelea kucheka kifedhuli huku akijitahidi kadri ya uwezo wake kuvuta sigara na kupuliza moshi hewani katika namna ya majigambo.
Nikiwa katika hali ileile niliisikia sautio nyembamba ya kike ikisema name katika namna ya kusihi, nilipata nguvu ya kugeuka huku nikiilazimisha akili yangu isijiruhusu kukutana na mama mwenye nyumba.
Kha!! Hapakuwa na mtu yeyote, hii nayo ikanistaajabisha. Lakini sauti iliendelea kusihi. Nikajipa ujasiri huku nikijitoa hofu kuwa mimi si mwizi wala sijaua. Na kwa misingi hiyo sitakiwi kuwa muoga.
Kwa mtazamo huo na masikio yangu yakafunguka. Nikasikia sauti ikisema name kiingereza.
Maneno yakaniingia na nguvu ziukanijaa tena, ilikuwa ni sauti ya Anitha ikinisihi jambo, macho yangu yakang’ara na kung’amua kuwa Yule mlinzi alikuwa amezeeka na hakuwa na ubavu wa kunizuia kwa lolote lile.
Na hapo nikagundua kwa nini nilikuwa na hofu kubwa mwanzoni.
Kauli ya Anitha ikanisukuma. Nikatoka mbio na kumvamia Yule mzee, nikamjaza kilo kadhaa za ngumi usoni. Tukio ambalo hakulitegemea, akapepesuka huku sigara ikimtoka mdomoni. Akatoa miguno ya maumivu, na hapo nikapata upenyo.
Kauli ya Anitha ikarudi tena kwa nguvu katika kumbukumbu zangu. Kauli aliyoniambia kwa lugha ya kiingereza.
“Hilo kufuri ni bovu….”
Nikalivuta likaachia, nikatoka mbio huku bahasha yangu ikiwa mkononi. Wakati napepea nikaiona gari aina ya difenda ikitimua vumbi kuja katika nyumba yam zee Matata.
Walikuwa wamenikamata hawa wajinga!!
Nilijisemea huku nikijilazimisha kurejea katika hali ya kawaida.
Nikaingia mitaa miwili ama mitatu na kutokea Sinza kijiweni. Nikajichanganya na umati wa watu wengi, kwa tahadhari kubwa kabisa nikachukua tena pikipiki na kuondoka hadi Mbezi ya Kimara. Huko nikachukua chumba kama kawaida katika nyumba ambayo ni ngumu kufikika katika mazingira ya kawaida.
Nilipojifungia ndani nilifikiria jambo moja tu!!
Nilikuwa napambana na nguvu kubwa!! Nilitakiwa kuwa makini.
Anti Ezekiel!!!!
Jina hilo likanijia kwa kasi katika namna ya kustukiza, kijana ambaye nilionana naye mara tatu katika maisha yangu huku ile ya nne ikiwa utata. Utata mtupu!!
Huyu Ezekiel anayesadikika kuwa ni shoga ni nani hasa hadi asababishe yote haya?
Na nkwanini haya yote yatokee baada ya mimi kufahamiana naye kwa uchache sana?
Nilijiuliza bila majibu!! Nikabaki kufahamu kuwa jambo pekee nililokuwa nalifahamu kiuhakika kabisa ni kuwa Yule bwana aliitwa Ezekiel. Sikujua jina la baba wala mama yake.
Nikaifungua bahasha yangu tena na kuanza kupekua huku na kule, nilikuwa sijamaliza kupitia zile karatasi ambazo nilizichukua nyumbani kwa Ezekiel. Nikaamua kuzipitia zilizokuwa zimesalia.
Nikapekua huku na kule, nikakutana na karatasi moja ambayo iliandikwa jina tena, si karatasi hii pekee iliyokuwa imeandikwa jina lakini hili lilikuwa na utofauti katika akili yangu.
Kindo!!!
Kindo halikuwa jina geni katika akili yangu, ika karatasi ile chini ya jina iliwekwa tarehe, tarehe ya mbali sana. Takribani miezi tisa iliyopita.
Cha kushangaza sikutaka lile jina linipite kama mengine kuna mahali nimewahi kulisikia, ama nimewahi kumuita mtu jina lile.
Nikaigeuza ile karatasi kwa nyuma na hapo nikakutana na neno lililonipa uhai wa kuendelea kutafuta jibu la wapi nimeskia jina lile.
Sinza.
Mwandiko ule mbovu uliandika vile. Hivyo nikawa na kazi ya kuunganisha mwezi jina na mahaliu.
Kwanini kindo, Sinza na mwezi huo.
Ghafla nikasimama wima na kukibinya kichwa changu, kuna kitu kilijileta katika mstari.
Jina la Kindo nililisikia wakati natafuta pikipiki ya kunibeba na kunifikisha Mbezi. Nilisikia kama si yeye akijitambulisha kwa jina basi alikuwa ameitwa na mwenzake.
Mtu sahihi wa kunisaidia katika safari ya kuutatua utata huo alikuwa ni Kindo!!
Lazima kuna kitu alijua juu ya Ezekiel, huenda ni ndugu ama jamaa au vyovyote vile lakini lazima tu!!
Lazima angefahamu lolote kuhusiana na Ezekiel.
Nikataka kutoka chumbani muda uleule nikamtafute Kindo lakini nikahofia kujiingiza matatani mapema sana, Sinza na Shekilango hayakuwa maeneo yanayoachana kwa mbali sana.
Shekilango nilikuwa nimezusha balaa tayari nyumbani kwa Mzee Matata, hapakuwa mahali sahihi hata kidogo kuonekana hata kwa bahati mbaya.
Muda huo nikataka kujipumzisha lakini nikamkumbuka Enock. Niliahidi kuzungumza naye kwa njia ya simu siku iliyopita lakini nikashindwa kutimiza ahadi. Nilifikiria ugumu ambao atakuwa anapitia katika kichwa chake kutokana na ukimya wangu na pia akilinganisha na vuguvugu hizo zilizosambaa mtaani tayari.
Nikautambua umuhimu wa simu, nikakifunga chumba change, bahasha nikiiweka chini ya godoro na kuondoka kuingia mitaani, nikapata simu ya bei rahisi, nikanunua na kadi mpya nikaiwekea pesa. Nikaondoka na kurejea chumbani.
Nikaiandika namba ya simu vyema kutoka katika kumbukumbu ya kichwa change na kisha nikapiga.
Simu ilinitia matuamini ilivyoanza kuita na baadaye kupokelewa.
Alikuwa mke wa Enock. Nilitaka kujitambulisha lakini mara Enock akawa ameichukua simu.
“Noki eeh!!” nilimwita. Na hapo akaitambua sauti yangu!!
Simu ikakatwa nisijue nini tatizo lakini baada ya dakika zisizozidi kumi na tano alinipigia.
“Kaka, nini tena hicho umefanya lakini eeh nini kaka, halafu hata hujaniambia. Mimi na wewe tumeanza kufichana mambo yetu tangu lini Sam eeh Sam…” alilaumu Enock.
“Sikiliza Enock…hivi umeyaamini hayo uliyoyasikia.” Nilimuuliza kwa sauti iliyotulia kabisa.
“Sijaamini hata moja Sam lakini kama ulijua una msala kwa nini usiniambie. Sikia polisi wamekuja kunisumbua hapa yaani wamepekua kila kona ya nyumba hii kaka. Hivi mbona hata hukuwahi kuniambia kuwa una bunduki Sam eeh Sam ilikuwa nia yako kuniingiza matatani ama?” sasa alisikika kupandwa na hasira.
Nikastaajabu, ina maana hawa watu wameunda uongo kiasi hicho hadi wamebambika kesi kuwa mimi namiliki bunduki? Nilikaa kimya Enock akaendelea kulalamika, “Sasa mimi hiyo kesho naenda kutoa maelezo gani kituoni eeh naenda kusema nini mimi. Urafiki gani huu sasa?” alizidi kufika mbali na nikaisikia ile kauli yake ya mwisho iliyokuwa katika mtindo wa kujutia urafiki wetu.
Yaani Enock niliyempokea Dar es salaam maisha yangu magumu lakini nikamtunza, nikamtafutia kazi na mwisho akaweza kujitegemea na kuoa, leo hii anasikitika kuwa rafiki yangu.
Nilitaka kumweleza mengi kuhusiana na ule mfuko wenye makaratasi lakini sikuona umuhimu wowote ule kwa sababu tayari alikuwa mguu ndani mguu nje. Nusu aliniamini na nusu hakuniamini.
Hakunifaa hata kidogo katika harakati.
Nikakata simu na kuizima kabisa, hasira ilinichemka kichwani!!!
Nilijua kuwa anaweza kunitumia ujumbe wowote ule na pia nilijua kuwa namba yangu ile ipo matatani tayari.
Sikuiweka tena katika simu!! Nikatoka nje na kwenda kununua kadi nyingine. Zote nilikuwa nazisajiri kwa majina feki.
Ile namba ya awali nikaitupilia mbali kabisa baada ya kuivunjavunja, sikutaka kumfikiria Enock tena, nikazitazama nguo zilizokuwa katika mwili wangu, zilikuwa mali yake. Nikachukia kujitazama.
Nikatamani kununua nguo nyingine lakini nikatambua kuwa katika kipindi hicho nilikuwa naihitaji pesa kuliko wakati mwingine.
Nikarejea chumbani!!
Nikajitupa kitandani usingizi nao ukasusa kunipitia, nikagalagala huku na kule pasi na mafanikio!! Saa kumi na moja ikanikuta nikiwa bado sijaupata usingizi. Nikaishika simu yangu yenye kadi mpya nisijue ni kitu gani inanisaidia.
Nikabofya namba nyingine nilizozikariri huenda nitapata msaada wa kimawazo. Sikujua kama nitabonyeza namba zile kwa usahihi, lakini nilifanikiwa kubofya.
Simu ikaita kwa muda mchache sana na kisha ikapokelewa.
Alikuwa yeye!!! Sauti yake haikuwahi kupotea masikioni mwangu kamwe!!
“Nani mwenzangu mbona huongei?” alikaripia nilivyoendelea kuwa kimya.
“Anitha…..Sam hapa….upo mahali sahihi tuzungumze kidogo.” Nilinong’ona. Kimya kikatanda, na mara Anitha akazungumza nami, alikuwa amejifungia chumbani mwake.
Sikutaka kujua nini kilitokea baada ya mimi kufanikiwa kutoroka lakini nilitaka msaada wake kimawazo kama bado angekuwa radhi kunisaidia. Anitha aliniambia kauli moja nzito ambayo ilinifanya niamini kuwa sasa nimepata wa kunishika mkono.
“Sam, kwa lolote lile nipo na wewe, najua wewe si muuaji, najua kuna kitu nyuma ya pazia japo sijakijua kitu hicho, nipo tayari kushirikiana na wewe ilimradi tu mimi na wewe tukivumbue kitu hicho.” Kisha akashusha pumzi na kunisikiliza.
“Anitha wewe ni msichana wa kipekee, nisizungumze sana lakini naomba nikuamini wewe. ….aaahm ni lini unaweza kutoka nyumbani.’
“Siku yoyote ile, si unajua nipo chuo siku hizi.”
“Ok kesho naomba ufanye jambo moja la msingi na litakalotuwezesha kujua wapi tunaanzia, hapo Sinza Kijiweni ama Sinza popote pale kuna mtu anaitwa Kindo, simjui kwa sura wala sauti lakini ni huyu anajua kuhusu Ezekiel..”
“Ezekiel ni nani?” alinikatisha. Nikalazimika kumsimulia upesi kwa ufupi sana juu ya hadithi ya shoga niliyemuona Ubungo akanipa funguo na kisha nikaikuta maiti yake ikioza kitandani Yombo Temeke.
Maelezo yangu yakamuacha Anitha katika kigugumizi lakini akaahidi kushughulikia jambo hilo.
“Kwani huwezi kuja chuoni kesho.”
“Hapana sitakiwi kuonekana kwenye hadhara kubwa namna hiyo ni hatari.”
“Ila kweli, sawa Sam nitakupigia kwa lolote.”
“Hautanipigia wewe nitakupigia mimi Anitha. Simu haitakuwa ikipatikana mara kwa mara.”
Nilimaliza mazungumzo na kisha kukata simu.
Hapo sasa niliweza kulala na amani kidogo moyo wangu nikiuegemeza kwa Anitha ambaye niliamini anaweza kunisaidia kwa lolote lile, lakini sikujitoa moja kwa moja kwake. Nilikuwa nusu namuamini na nusu nikiishi kwa tahadhari.
Baada ya kula chakula cha usiku majira ya saa tatu usiku niliiwasha tena simu yangu na kisha nikambipu Anitha.
Upesi akanipigia.
Hakunipa nafasi ya kuzungumza na badala yake akachukua usukani kusimulia.

ANITHA

SAM najua upo matatani sana, nisingeweza kungoja hata kidogo hiyo kesho ifike ili nianze kumtafuta huyo mtu wa kuitwa Kindo.
Sinza ni kubwa lakini kama una nia ya dhati ni mtaa mdogo sana kuumaliza,. Niliondoka nyumbani nikimuaga baba kuwa naenda chuoni, lakini sikuwa na safari hiyo, safari yangu ikaishia mitaani. Halikuwa jambo jepesi kumpata mtu usiyejua hata kazi yake, lakini nilifanya kwa ajili yako Sam.
Nilifanya nikijua kuwa wewe upo upande wa haki, na hakika upo katika haki.
Mungu hamtupi mwenye nia na anayemtegemea, nilipopiga hatua yangu na kuanza rasmi kumtafuta Kindo nilimtanguliza Mungu, niliulizia kila kona na kila ofisi lakini sikumpata Kindo. Wengine walidai kumfahamu lakini hawakuonyesha ushirikiano kabisa, hadi ilipotimu saa kumi na mbili jioni maeneo ya Sinza kijiweni nikiwa najiandaa kupanda gari nirejee nyumbani pasipo na mafanikio nikasikia jina kama hilo likiitwa. Nilikuwa nimebanwa hasa lakini nguvu za kusukuma abiria wengine zilipatikana nikafanikiwa kupenya na kushuka chini, nikamuuliza mwanafunzi mmoja akaninyooshea kwa kidole huyo mtu wa kuitwa Kindo.
Ni teja…teja aliyekubuhu, madawa ya kulevya yameweka makazi katika mwili wake, sikuweza hata kusema naye maana alikuwa akitiririkwa na udenda na alikuwa ameuchapa usingizi. Nikapata kigugumizi kuamini kama kweli huyu ndiye Kindo uliyeniagiza kumtafuta ama kuna Kindo mwingine.
Swali hili nilitamani nije kukuuliza lakini ukadai kuwa hujawahi kumwona Kindo na hata hujui sura yake ilivyo. Kama ungekuwa unamfahamu walau ningekwambia haya Sam. Kuwa kindo ni mweupe wa zamani lakini sasa hajulikani rangi yake, ni mrefu wa wastani na kichwani hana nywele.
Kwa sababu nisingeweza kusema na mtu asiyesema kwa tahadhari kubwa nilijipiga picha nikiwa usawa wake na katika hiyo picha ameonekana, kama unayo barua pepe nitakutumia uweze kumwona teja huyu wa kuitwa Kindo.
Na hapo tutajua kama ndiye ama siye!!
Kesho nitaenda tena kumwona kama akiwa anaongea nitamuuliza juu ya Ezekiel. Tumwombe
Mungu atoe jibu zuri, maa sura yake licha ya kumwagika kwa madawa inatangaza chuki kali. Sijui anachukia nini Mungu wangu!!!
ANITHA akamaliza!!!
Nilibaki nimekaa hivyohivyo kitako katika kitanda cha futi nne kwa sita, maelezo ya Anitha yalizidi kuzua utata. Japo mwanga ulionekana lakini mwanga huu ulikuwa hafifu sana walau kunipa uwezo wa kupiga hatua moja mbele.
Ni kweli nilikumbuka kuwa nilisikia jina kindo palepale Sinza kijiweni, lakini katika ile karatasi paliandikwa kuwa ni miezi tisa iliyopita.
Sasa kilitokea nini miezi tisa iliyopita. Je ni kweli huyu Kindo anayetakiwa ama? Ama Anitha naye anataka kunichezea kamchezo!!!
No no no!! nililipinga wazo la kumfikiria Anitha vibaya, ni asubuhi tu alitoka kuniokoa sasa iweje jioni anikane???
Hapana ilikuwa mapema sana kumwazia vibaya!!!
Nikarejesha mawazo yangu kwa Kindo!!
Kindo teja, kindo mwenye kipara Kindo asiyejitambua, kindo wa miezi tisa iliyopita.
Kindo ambaye Anti Ezekieli alikuwa amemworodhesha katika karatasi zile.
Hakuna picha wala neno la ziada!!!
Utata!!!!

**JIFUNZE: Katika maisha usipende kumfahamu mtu kwa kuhadithiwa na fulani, ili umfahamu mtu vyema na tabia zake basi akili yako ikupe majibu yenyewe kutokana na vitendo vya huyo mtu. Usimuulize jirani yako ama usitumie tetesi kumfahamu mtu. Je? Utajuaje kama hao wanaokwambia wana chuki naye? Utajuaje kama ni marafiki zake na sasa wanamsifia kwa lolote!!!
Epuka!! Na hii itakusaidia kujua kuishi na mwanadamu!!
 
SEHEMU YA SABA
SEHEMU YA SABA
ASUBUHI sana nilidamka, kitu cha kwanza nikapanga mipango ya kuhamia nyumba nyingine ya kulala wageni. Nilijiwekea tahadhari kabla ya hatari, ingewezekana kabisa namba yangu ya simu kutumika katika kunisaka na hii ingekuwa hatari sana kwangu. Isitoshe Anitha hakuwa akijua lolote juu ya Ezekiel, hakumjua hata sura. Hivyo kama ningekubali kukamatwa hata kama kweli alikuwa na nia ya kunisaidia ndo basi tena mwisho wa jeuri yake.
Na nilivyoijua sheria ya Tanzania mwenye haki hana haki tena akiwa nyuma ya vyuma vya mahabusu ama gereza. Nani angenielewa na kunisikiliza nimweleze juu ya hadithi za bunuasi kuhusu Ezekiel wa Ubungo na yule maiti wa Temeke.
Hakuna sheria ambayo ingenilinda hata kidogo!! Huenda hata Anitha naye angebadili misimamo yake juu ya jambo hilo!!
Nilitambua kuwa sijaswaki baada ya kuzungumza kwa sauti bila kujua na hapo nikatambua kuwa kinywa hakikuwa katika usafi. Lakini nani angejali hali ile!!
Hakuna hata mmoja!! Nikaendelea kutembea nikiangalia chini, mara mbele na wakati mwingine kushoto na kulia.
Sikuwa na amani!!!
Nikakatisha mitaa zaidi na zaidi na jua lilianza kuchomoza nisijue wapi naelekea.
Umati wa watu ukanivuta katika eneo la wazi, nikajisogeza kwa tahadhari nisijue ni nini nafuata huko.
Magazeti!!! Kundi lile lilikuwa likipepesa macho katika vichwa vya magazeti.
Na mimi nikajiunga huku nikiwa makini kabisa nisiweze kumtazama yeyote machoni, kofia yangu ya pama nayo ilinifunika vyema.
“ALVIN ALILAWITIWA KABLA HAJAUWAWA!!” kichwa cha habari katika gazeti mojawapo kilisomeka hivyo, pembeni yake ilipambwa picha yangu ikisheheni maneno machache
“ANATAFUTWA”
Nikajikaza na kuendelea kutazama habari nyingine.
“MUUAJI ANASAKWA AUWAWE” pembeni yake kulikuwa na picha ya kitanzi.
“MIAKA THELATHINI JELA INAMNGOJA SAMSON” kichwa kingine cha habari.
“ALVIN AFA NA SIRI NZITO!!” hili lilikuwa gazeti la udaku nikasonya.
“MANENO YA MWISHO YA ALVIN KABLA HAJAUWAWA. ALIMUACHIA SAMSON UJUMBE MZITO.” Kichwa hiki cha habari kikanivuta zaidi. Na hapo nikapata jibu langu huku utatat ukizidi.
Kumbe aliyekufa anaitwa Alvin, sasa hili jina la Ezekiel limetoka wapi? Nikajipekua na kutoa pesa kiasi na kumpatia muuza magazeti, kisha nikaondoka nikiwa nimeinama chini vilevile.
Mawazo lukuki yakinikabili, nilitarajia nitakuta habari juu ya kuonekana kwangu maeneo ya Shekilango labda hata nguo nilizokuwa nimevaa zingeweza kuandikwa pale. Ajabu hakuna kitu kama hicho kilichoandikwa!!
Nikajikongoja hadi katika mgahawa mmoja, nikapata chai na chapati mbili.
Baada ya hapo nikahama tena, safari hii nikajichimbia maeneo ya Kimara Suka. Mbezi nikatoweka bila taarifa.
Majira ya saa sita nikaiwasha simu yangu!!! Ukaingia ujumbe kutoka kwa Anitha, alikuwa anahitaji kuzungumza name.
Nikambipu palepale!!
Baada ya dakika tano simu ikaingia!! Anitha alizungumza kwa sauti yenye tumaini kiasi fulani.
Nikamwachia ukumbi Anitha akiwa msimuliaji nami msikilizaji.

ANITHA

KUTOKA saa kumi na moja alfajiri katika nyumba ya mzee Matata si jambo jepesi hata kidogo, lakini yawezekana ikiwa tu ukiwa jasiri. Nami niliuvaa ujasiri nikatoweka nikidanganya kuwa kuna jambo la msingi la kufanya chuoni asubuhi hiyo. Mzee wangu na shule nadhani unafahamu, hakunioinga hata kidogo. Lakini hasira zake tangu usiku uliopita zilikuwa bado zimemtawala, nadhani hakulala hata kidogo maana tangu akaripie sebuleni usiku ule nilimkuta hapo hapo. Baba ametamka kuwa anakuchukia sana huenda kupita wanadamu wote duniani, eti kisa tu wewe ni mlawiti. Dhambi kubwa kupita zote, analalamika kuwa umemnlawiti kijana wa kuitwa jina la Alvin na ukaona hiyo haitoshi ukamuua ili asikufichulie siri, aliyazungumza haya akiwa na bastola yake ile ya tangu miaka ile. Akakulaani huku akimlaumu mama kwa kushindwa kukufyatua ulipojileta wewe mwenyewe nyumbani. Akatukanya sana nkuwa kwa lolote lile tukiwasiliana nawe tumpe taarifa, hakika amechukia mzee yule. Kila mmoja alimuunga mkono, dada Jenipher akamtukana mama aliyekuzaa na mjomba Yakobo naye akakilaani kizazi chako, mama akatoa ushauri kuwa wakuendee kwa mganga ili wakufanye kichaa milele. Baba akasema akikuona atakuua kwanza nd’o mengine yafuate. Sasa nikajiuliza kuwa kishakuua ni kipi kinafuata zaidi yaw ewe kuzikwa!!!
Niliumia moyoni lakini maneno yao hayakunifanya niwe upande wao, nakufahamu zaidi ya wao wanavyokufahamu.
Kama ulikuwa mkweli kwangu ni vipi ufanye yote haya nyuma yangu???
Nikaamua kuutafuta ukweli kama kweli upo…nikatoweka alfajiri.
Sinza Kijiweni ilikuwa kimya!! Kama pangekuwa kijijini basi lazima kuku wangekuwa wanawika lakini huku palikuwa kimya, ni magari kadhaa tu yaliyokuwa yakipita na kupiga kelele.
Nilinyata hadi nikalifikia eneo ambalo nilimkuta Kindo usiku ule uliopita, nikaangaza huku na kule nikajikuta katika ugumu. Huu nd’o ubaya wa jiji la Dar es salaam, watu wengi hawana makazi ya kudumu, vijana wanasota na jua mchana na bado usiku wanalala nje.
Nikashindwa kuelewa yupi ni Kindo na yupi si Kindo. Hofu ya kubakwa ikaniandana iwapo vijana wale wataamka pamoja na kutambua kuwa nilikuwa sina uelekeo maalum. Nilijikabidhi kwa Mungu asubuhi ile kama nifanyavyo siku zote hivyo ni yeye tu alikuwa tegemezi langu!!
Moshi mweupe hewani ukanivuta kutazama unatoka wapi, nikasogea huku nikiwa tayari kwa hatari yoyote iwapo itatokea nitimue mbio!!
Si unanijua tena mimi kwa riadha!!
Sura ya Kindo ilikuwa imara sasa. Haikuwa imemwagika hovyo kama usiku ule, nikamsogelea huku nikihofia lolote ambalo lingeweza kutokea. Sura yake ya kigaidi ilinitisha.
“Kaka…..” nilimwita mara moja na yeye akageuka. Nikamsabahi kwa heshima zote naye akanijibu kwa upole.
Sikutegemea kabisa!! Nikakosa pa kuanzia akanikaribisha katika gogo la mti nikaketi!!
“Naitwa Sarah” nilimlaghai jina ili kwa lolote lile la mbele ushahidi usiwepo. Akatikisa kichwa akingoja nimuulize zaidi, nikamuuliza iwapo yeye ndiye kindo akanijibu kwa kirefu kuwa jina lake sahihi zaidi ni Kindole Emmanuel. Mwenyeji wa Iringa!!
Nikastaajabu, hakufanania hata kidogo na maneno yake ukifananisha na ugumu wa sura yake.
Nikamuuliza kuwa kama miezi tisa iliyopita aliwahi kumjua Ezekiel, alijaribu kuvuta miezi nyuma lakini kabla ya kujibu akaniuliza mimi ni nani. Nikakosa cha kujibu nikadanganya kuwa ni rafiki yake Ezekiel na nimepotezana naye siku nyingi lakini katika kumbumbukumbu zangu aliwahi kuniambia ana ndugu ama jamaa aitwaye Kindo na ni mwenyeji wa Sinza. Nikaendelkea kulaghai kuwa nina siku chache sana jijini Dar es salaam na nimekuwa nikipatafuta Sinza na nikimtafuta yeye.
Baada ya kunisikiliza kwa makini alionekana kustaajabu mno, lakini alikana kabisa kumjua Ezekiel. Hakika uso wake ulimaanisha alichokuwa anakisema.
Baadaye akanieleza kuwa miezi tisa iliyopita wala hakuwa jinni Dar es salaam alikuwa zake huko Iringa. Akaniamini na kunieleza kuwa hata yeye si mwenyeji sana jijini Dar es salaam na maisha magumu nd’o yanamfanya alivyo!!
Nikamuuliza huko Iringa akumbuke kwa makini, akakataa katakata kumjua Ezekiel.
Nilijaribu kukupigia simu labda walau uelezee muonekano wa Ezekiel huenda anaweza kukumbuka lakini kama ulivyopanga kutoniamini ulikuwa hupatikani hewani!!
Na asubuhi ikatukuta tukiwa katika mgahawa, Kindo si katili kama nilivyodhani, Kindo si mkorofi hata kidogo!! Na Kindo ni kama alikuwa anafahamika maana watu walitutania sana walipotuona na yeye aliishia kucheka tu na wakati mwingine wakirushiana matusi ya nguoni ambayo hayakumwathiri Kindo.
“Wapiga debe wenzangu hao wakorofi sana…” aliniambia Kindo na hapo nikaijua kazi inayomuweka mjini, nisiite kazi bali kibarua kisichokuwa rasmi.
Kindo alinishukuru kwa ukarimu wangu!! Na baadaye nikamuachia namba za simu iwapo atakumbuka lolote juu ya Ezekiel. Nikampatia na kiasi cha pesa.
Nikaondoka na kwenda kituoni!!!
Hata kabla sijapanda gari nikasikia kilio kikuu kutoka upande niliomuacha Kindo. Nikachungulia na kugundua kuwa anayelia ni Kindo!!
Nikarejea upande ule kutazama kulikoni, alikuwa analia akisema wamemuua kaka yangu, wamemuua kaka yangu!! Sikuelewa ana maana gani bado. Hakutaka kuguswa na mtu hata mimi hakutaka kunisikia.
Watu walibaki kuduwaa wasijue analia nini. Akakimbia na kuvamia meza ya magazeti, akajipekua na kutoa pesa niliyompa akanunua gazeti. Watu wakabaki kuduwaa hakuomba chenji yake, sasa akawa amelikumbatia gazeti.
Na hata alipoliachia alikuwa akiililia picha ya mtu aitwaye Alvin, ambaye amekufa ama ameuliwa na muuaji unasadikika kuwa wewe Sam. Kindo analia akisema ni kaka yake, kwa maana hiyo yawezekana Alvin ndo Ezekiel!!! Nikaishiwa nguvu nikakaa chini. Na hilo nd’o jibu!!!
Kindo akiwa katika kuruka ruka huku na kule mara wakatokea watu wawili waliojazia miili yao wakamchukua na kuondoka kwenda naye wanapojua wenyewe!!!
Hakuna aliyejali, Kindo hakuwa na ndugu!! Nami nikaogopa kujipeleka kimbelembele kwa sababu tayari alikuwa amenikataa na mimi baada ya kuona habari ile katika gazeti!!!
Majira ya saa tano asubuhi!! Nikapanda gari Sam na muda huu naongea na wewe nipo chuoni mpendwa wangu!!
Sijui hata ni kipi kinafuata, labda nitaenda kuonana na Kindo tena akishapoa nimweleze kuwa Alvin nd’o Ezekiel nimsikie ataniambia nini japo ameonekana kuumia sana.
ANITHA AKAMALIZA………

UPANDE WANGU
Kijasho chembamaba kilikuwa kinanitoka, habari ile ilinisisimua sana, ni kama mwanafunzi anayekaribia kulipata jibu lakini mwisho analisahau tena, nd’o kilichotokea Kindo alikuwa mtu sahihi wa kuweza kutupa mwanga juu ya Alvin ama Ezekiel kama nilivyomtambua lakini mkanganyiko wa majina ulituzuzua na sasa yule mtu sahihi akashindwa kutueleza juu ya jambo tunalohitaji.
Nilijilaumu kwa kutokuwa hewani, labda kweli Anitha alikuwa sawa kuweka hisia za mimi kutomwamini. Nilifadhaika lakini ni kweli sikuwa nimejitoa kwa asilimia mia kwake, na nisingeweza kufanyanhivyo kwa sababu.
Aumwae na nyoka akiguswa na ujani hushtuka!!!
Kama baba yake ananichukia vipi kuhusu yeye!!! Na wahenga walisema damu ni nzito kuliko maji???
Majira ya saa kumi jioni nilikuwa katika pikipiki, sasa nilijipanga kwa ajili ya kuonana na Kindo mimi mwenyewe, maelekezo ya Anitha jinsia alivyokutana na kijana huyu yalinisaidia na hatimaye nikajikuta eneo lile. Nikajiweka kijiwe cha kahawa nikaanza kunywa kikombe kimoja baada ya kingine. Wazee walikichangamsha kijiwe kwa hadithi zao za uongo na kweli huku mimi nikiwa msikilizaji.
Laiti kama ningekuwa huru kama zamani basi kijiwe kingepata wateja wengi sana siku hiyo kwani zile zilikuwa hadithi nilizozipenda, hadithi za uongo na kweli kutoka kwa wazee.
Nilichangia mada mara moja moja sana huku saa zote nikijifanya kukolewa na utamu wa kashata!!
“Samahani mzee hivi bwana Kindo leo wapi?” nilimuuliza mzee mmoja aliyevalia kibalaghashia. Aliangaza huku na kule kisha akanieleza kuwa labda ameenda kwa daktari, nikamchimba zaidi akanieleza kuwa daktari ni yule anayewadunga madawa ya kulevya!!
Nikakubaliana naye!!!
Majira ya saa moja usiku kijiwe cha hadithi za sungura na paka kikageuka kuwa cha hadithi ya kutatanisha.
Bwana mmoja akaketi na kunyamazisha wote kisha akaelezea kuwa Kindo amekutwa ufukweni mwa bahari akiwa amekufa!!!
Labda mimi ndiye nilishtuka zaidi, jina Kindo lilikuwa jina nililofuata pale. Lakini kabla sijaiona hata sura yake naambiwa kuwa amekutwa amekufa!!
Nikatahamaki!!
Lakini kabla sijakaa sawa mara nikashtushwa na kauli iliyotolewa na mzee mwenye kibalaghashia ambaye awali nilimuuliza juu ya Kindo.
“Huyu kijana ni mgeni hapa na amekuwa akimuulizia kindo katika namna ya kipekee, kwanza usiku huu na amefunika kichwa chake, macho pia yana mawani namna gani yakhee!! Kwani huyo Kindo ulimtakia nini weye!!” aliwaka kwa sauti ya juu, umati ukjnigeukia, wote wakawa kimya wakisubiri niseme neno.
Sikutarajia shambulio hilo, nikabaki kutetemeka. Hali yangu ya hofu ikawafanya wateja wa kahawa wavutike zaidi kujua ni kwa nini nilimtaka Kindo!!
Wakaanza kunizongazonga, wengine walikuwa mateja na wengine makondakta na wapiga debe, muuza kahawa akaanza kukusanya vilivyo vyake. Hali ilikuwa tata!!
Mara mmoja akanikwapua kofia kichwani na mwingine akanitoa mawani nyeusi usoni!!
Hawakuwa na utani wale watu!!
“Mlete kwnye mwanga huku…mlete huyoo, hawa ndo tunawatafuta hawa hata Rama walimuua hivihivi….” Alikoroma kijana mmoja. Wenzake wakatii wakaanza kunighasi huku na kule!! Wakinivuta kuelekea kwenye mwanga, yule mzee mwenye kibandiko alikuwa jirani na mimi akinitukana sana huku akisisitiza kuwa najua kinachoendelea.
Nilijaribu kujitetea kuwa hata sura ya Kindo siifahamu lakini hakuna aliyeisikia sauti yangu!!!
Sam mimi nilikuwa nimepatikana!! Tukazidi kuuelekea mwanga, na lazima ntungeufikia tu!!! Sura yangu ilikuwa katika magazeti ya siku hiyo!!
Lazima watakuwa waliiona!! Isitoshe sakata alilonisimulia Anitha la Sam kulilia picha katika gazeti. Basi wengi watakuwa waliliangalia gazeti lile!
Gazeti lenye sura yangu!!

**JIFUNZE: KATIKA maisha vikwazo ni sehemu ya mapito!! Hakuna mapito nyoofu mpaka mwisho, jiandae kukabiliana na makwazo maana hayo tuliumbiwa sisi wanadamu ili kupimwa imani yetu!!!
 
SEHEMU YA NANE
SEHEMU YA NANE

Lile kundi lilizidi kunighasi bila kunipa nafasi ya kunisikiliza. Mwanzoni walisema wanaufuata mwanga ili wanitambue vizuri lakini sasa waliupita ule mwanga na kukifuata kichochoro walichokijua wao. Kuna lugha zao waliambiana na sikuweza kuzikumbuka wala kuambulia chochote!!
Baada ya kukifikia kichochoro kile mara ghafla mimi na yule mzee mwenye kibalaghashia tukajikuta tumewekwa katikati. Harufu kali ya moshi wa bangi ilitawala eneo lile na palikuwa kimya.
“Toa kila kitu ulichonacho bazazi wewe!!!” aliamrisha bwana mmoja, nikashuhudia kisu kikubwa mkononi mwake!! Mzee mwenye kibalaghashia akatumbua macho, hakutarajia kama tukio linaweza kubadilika namna ile!! Yeye alitarajia labda nikishatambuliwa basi atapongezwa lakini mambo yaliharibika wale waliotuzunguka neno kifo cha Kindo lilikuwa la kawaida sana kwao.
Wote tukajikuta tunatetemeka, lakini kwangu ilikuwa nafuu zaidi kutekwa na wale watu ambao niliamini kuwa ni vibaka tu wa kawaida kuliko kuingia katika mikono ya wale watu wabaya ama serikali ambayo ilikuwa imehadaika na sasa ikinisaka kama muuaji na mbakaji!!
Niliangusha simu yangu wakaikwapua!! Nikajipekua na kutoka na kiasi cha pesa na hiki pia wakachukua. Wakatoa vitisho kadha wa kadha
Yule mzee alikuwa na kanzu tu hakuwa na kitu cha ziada, wakamweka kando!!
Si kwamba walimwachia la!!
Nilishangaa ghafla alikuwa hewani na mara akatua chini, alikuwa amepigwa ngwala ya ghafla, yule mpigaji akajikausha kana kwamba si yeye aliyetoka kufanya tukio lile lililoipasua kanzu ya yule mzee na kukirusha kibalaghashia chake kando!! Hawakumwambia lolote.
Wakanirudia mimi tena, hawakuwa na utani hata kidogo na nyuso zao zilijawa chuki tupu!!
Kujifanya wananizongazonga waweze kunitambua mimi ni nani hiyo ilikuwa hila tu hakuna lolote walilotaka zaidi ya kuniibia na hilo walikuwa wamefanikiwa!!
Ajabu ni kwamba kuna watu walilishuhudia tukio hili lakini hata kujihusisha kutusaidia hawakujisumbua, na ilikuwa heri hawakujihusisha nasi maana wangeweza kutokea ambao aidha wangeweza kunitambua ama wangeyafanya mambo kuwa magumu zaidi!!
Hakika jiji la Dar es salaam lilikuwa limeoza na maovu kama haya yalikuwa kama kitu cha kawaida mbele ya macho ya watu!!
“Kindo umemfahamia wapi we bwege?” mara aliniuliza yule bwana aliyezungumza kama kiongozi na wenzake kumsikiliza.
“Ni jamaa yangu tu….mimi ni mtu wa Iringa nd’o nilikuwa namuulizia jamani” nilijitetea. Mara bwana mmoja akadakia hoja.
“Na wewe ndo wahanga wa ridandansi ya Michigani ama?” aliniuliza, akili ikafyatuka hilo neno Michigani halikuwa geni hata kidogo masikioni mwangu.
“Hapana, ni ndugu tu jamani!!” niliendelea kujitetea.
Ile kusema neno Michigani basi kila mmoja akacheka kati ya wale vibaka. Bila shaka halikuwa neno geni kwao. Ajabu ni kwamba neno lile hata kwangu pia halikuwa geni kuna mahali niliwahi kuliona kisha nikalipuuzia na sasa nalisikia tena.
“Yaani kila mtu wa Iringa huwa anadanganya kuwa alikuwa Michigani amefukuzwa kazi aisee sijui huko Michigani nd’o kampuni pekee kubwa??….haya dakika moja potea hapa urudi Michigani kwenu huko!!! Moja mbili…..” aliamuru na hakuwa na utani, kabla hajafika tatu nikatimua mbio kali huku nyuma nikimsikia yule mzee mwenye kibalaghashia akilalamika kwa maumivu, bila shaka alikuwa akipokea kipigo kingine kwa kutembea bila pesa.
Sikusimama maana nilikuwa nimeponea katika tundu la sindano, nilikimbia bila kukoma hadi maeneo ya Tandale, nikachepuka na kona kadhaa kabla sijairuhusu akili yangu kufanya kazi tena.
Uzuri ni kwamba nilikuwa nimechukua tahadhari mapema sana, pesa zangu niliziweka katika mafungu mbalimbali kwenye nguo nilizokuwa nimevaa. Hivyo hata nilipowapa wale wakora zile pesa na simu bado nilibakiwa na fedha nyingine ambazo zilinitosha kufanya safari ya kurejea kule nilipofikia kwa kutumia usafiri wa pikipiki tena!!!
Badala ya kusikitikia suala la kukaribia kukamatwa nilitamani tufike upesi Kimara niweze kuwa huru na kisha kujipanga tena upya kujitafutia haki yangu bila uhai wa Kindo!!
Maeneo ya Tandale sokoni, kabla sijachukua pikipiki, kwa tahadhari kubwa nilifanikiwa kununua kofia nyingine, na pia nikavutika kununua fulana kubwa na suruali nyingine.
Ile kofia nikaivaa muda uleule na kisha kutoweka, nikiwa kama mzuka aliyefufuka kutoka katika wafu nisiamini kama na hatua ile nimepona pia.
Majira ya saa mbili nilikuwa chumbani!! Upesi nikachukua bahasha yangu ambayo nilikuwa nimeificha chini ya godoro, nikamwaga makaratasi yote chini na hapo nikaiona ile picha ambayo jengo lake dogo limeandikwa Michigan. Ni hapa nilipokuwa nikisumbua akili yangu kupatambua!!
Niliitazama kwa makini sana, na hapo nikaanza kuunganisha matukio, nikayakumbuka mazungumzo baina yangu na Anitha aliponambia kuwa Kindo ambaye anasadikika kuwa marehemu tayari alikuwa mwenyeji wa Iringa, kama hii haitoshi wale vibaka waliposikia kuwa mimi ni jamaa yake Kindo mara moja wakadakia kuwa na mimi ni wa Michigan!!
Huko Michigan ni wapi?
Na je panahusika nini ni mauaji ya Ezekiel ambaye kwa jina halisi ama vyovyote vile ni Alvin.
Kwa maana hiyo Kindo aliwahi kuwaambia vibaka hao kuwa yeye alikuwa muajiriwa huko Michigan? Baadaye akapewa ridandansi!!!
Hapa kuna tatizo lazima!! Kindo amekufa na siri kubwa sana!!
Nikatamani sana kuzungumza na Anitha usiku huo lakini tatizo sikuwa na simu tena wale mabazazi huenda walishaiuza kwa bei ya kutupa tayari!!
Nikatoka nje na kumkabili muhudumu aliyekuwa mapokezi, nilimkuta akiwa ametingwa katika kusikiliza muziki na ilinilazimu kumuita mara tatu hata akanisikia, nikamsihi aniazime simu yake kuna simu ya muhimu sana nahitaji kupiga!!!
Akalalamika kuwa simu yake huwa haibadilishwi kadi, nikamweleza kuwa sitabadili. Bado akalalamika mengi na klusema simu yake haina muda wa maongezi, nikatoa shilingi elfu tano mfukoni. Uzuri huduma ya vocha ilikuwa pale, hapo akakosa ujanja na kufikia hatua ya kuniazima!!
Nikatoweka na ile simu na kuelekea chumbani kwangu!!
Nikajisifu kwa uwezo wangu mkubwa wa kukariri. Nikaziandika namba za Anitha katika simu ile na kungojea simu ile iiite.
Ikaanza kuita na baada ya dakika kadhaa ikapokelewa!!
Kama mimi nilivyotegea upande wa pili uanze kuzungumza na upande wa pili nao ukangoja mimi nianze kuzungumza!!
Mtego!! Nikajiwazia huku nikiendelea kukaa kimya!!
“Halo!” hatimaye sauti kutoka upande wa pili ilinong’ona. Alikuwa Anitha!!
Hapo nikapata ujasiri wa kujitambulisha upesiupesi!!
Anitha akasikika akikurupuka kwa fujo kutoka alipokuwa na nikasikia vishindo na baada ya hapo aliniuliza kama nilikuwa salama!! Nikajibu kuwa nipo salama kabisa, akaniuliza tena na tena kama nina uhakika na usalama wangu nami nikasisitiza kuwa hakuna baya lolote upande wangu!!
“Kindo amekufa….” Aliniambia binti huyu kitu ambacho nilikuwa nakitambua tayari.
“Nini kivipi?” nilimuuliza kana kwamba hakuna nijualo!!
Alinielezea kuwa na yeye hajui lolote lakini katika mapito yake pale kuhakikisha kuwa anazungumza tena na Kindo alipewa taarifa hiyo.
“Mbona unaulizia mara mbilimbili juu ya usalama wangu lakini!!” nilimuuliza kutaka kujua.
ANITHA akachukua nafasi kusimulia!!
SAM naomba nikiri kuwa naipongeza nafsi yangu kwa kuendelea kukuamini kila kukicha. Sikuwahi kukatishwa tamaa na habari za kwenye magazeti. Kashfa na tuhuma zote ulizozushiwa hazikuwahi kuniteteresha kamwe! Baada ya kifo cha Kindo, nimeamini kuwa kuna watu wabaya wengi wamelizunguka tukio hili na hakika u katika wakati mgumu sana.
Sam najua hujipiganii peke yako na labda unaona haya kunieleza kuwa unao uchungu sana kuwa hujui mkeo alipo na usalama wa mtoto wako. Ni kweli ninao wivu kwa sababu nakupenda lakini amini haya ninayokuambia. Sam naumia sana ten asana, juu ya mama Eva na Eva mwenyewe. Mama Eva ni mwanamke mwenzangu, hana kosa alilowahi kunitendea zaidi tu ya kujikuta katika penzi lako.
Eva ni mtoto mdogo hajui lolote kuhusu hisia zangu kwako!! Hastahili kuchukiwa!! Na sijawahi kumchukia unalitambua hilo.
Sam kwa hali ya amani ilivyo juu yako, kwa jinsi watu wabaya wanavyoisaka roho yako.
Nipo radhi niambie unahitaji kitu gani kingine naweza kufanya kwa ajili yako wewe, Eva na mama Eva. Niambie chochote hata kama ni kigumu nami nitakujibu kuwa naweza ama kipo nje ya uwezp wangu!!!” alinieleza kwa hisia kali huku akizungumza kwa sauti ya chini, kila neno likawa na maana kwangu nami nikajibu.
“Anitha, kama nilivyosema awali kuwa hata nikikushukuru namna gani bado sitafikia kiwango unachostahili.
Anitha naomba niwe muwazi kuwa hakika baada ya usaliti alioufanya mzee Matata ambaye ni baba yako imani yangu kwa wanadamu imekuwa hafifu sana. Yaani namuogopa kila mtu!!
Laiti kama ningekuwa sina familia nisingeogopa lolote lakini Eva ndo ananiumiza zaidi huku mama yake akinipagawisha kabisa, sijui alipo huenda hata wamemuua naye tutasikia kama hivyo kwa Kindo!! Anitha nimeamua kitu kimoja, nimeamua kujikabidhi kwako Anitha. Kujikabidhi kwa asilimia zote mia moja.
Kama sitakuwa sahihi basi chozi la Eva na damu ya mama Eva iwe juu yangu kwa upumbavu wangu!! Kilio cha Eva na kinisulubu iwapo sitakuwa sahihi kukuamini wewe kama mtu wa mwisho pekee ninayeamini upo upande wangu!!
Sina lolote la kufanya ikiwa sura yangu haitakikani mtaani na sasa Tanzania nzima wanaijua sura na jina langu popote pale nitakamatwa tu! Anitha narudia tena na samahani kama nitakuwa nakukera, tambua kuwa mimi Sam sijaua mtu wala kulawiti!! Iwapo baba yako ama familia kwa ujumla zimekumezesha sumu na kuamua kunikamata mimi sasa nipo radhi, lakini nikiwekewa kitanzi shingoni, neno nitakalosema juu yako ni kwamba lawama za Eva na mama yake ziwe juu yangu lakini damu yangu na uhai nitakaoupoteza kwa hila na hujuma ya hali ya juu, vyote vitakuwa juu yako Anitha. Namkabidhi Mungu uaminifu huu wa mwisho mkubwa ninaoamua kuuleta kwako. Yeye pekee ndiye ajuaye ni kiasi gani nipo upande wa haki na sijui lolote kuhusu kuua. Na ni yeye huyuhuyu aliyeniambia kuwa kesho nikutane na wewe ana kwa ana!!” nilimaliza huku nikishindwa kuyazuia machozi yangu nilipomkumbuka mke wangu asiyejulikana mahali alipo na Eva anayesadikika kutunzwa na jeshi la polisi Tanzania.
Upande wa pili nilimsikia Anitha naye akililia kilio cha kwikwi, na hata alipozungumza alitoa kauli fupi tu.
“Na kilaaniwe kizazi changu chote milele na milele iwapo siku moja nitasimama na kutetea maovu…Sam tukutane kesho saa tatu usiku. Utaniambia muda huo nije wapi??” kisha akakata simu!!
Sikutaka kumpigia simu kwa sababu nilijua hataweza kuzungumza tena, maneno yangu huenda yamemuumiza moyoni ama yamemtia aibu kwa mpango aliokuwanao na sasa anajutia kwa machozi!!
Nikamtumia ujumbe mfupi. Nikamuelezea wapi nitakuwepo, sitakuwa na simu lakini nitafika kwa wakati!! Pia nikamsisitiza asitumie namba ile tena!!
Nikamaliza nikaifuta namba yake katika simu ile na kumrejeshea muhudumu, salio lililobaki mle lilimfanya atokwe na tabasamu, meno yake ya njano yakaonekana.
Sikurudi kulala, nikaondoka na kujipatia mkate na soda dukani, nikarejea chumbani kwangu kupooza njaa huku nikitafakari Michigani ni kitu gani na kwanini Kindo ahusike nayo na kisha Alvin.
Michigan Michigan!!!
Nililala nikiwaza hayo!!
SIKU iliyofuata kama ilivyoutaratibu wangu nilihama nyumba ile na kuhamia kwingine kabisa maeneo ya Ubungo. Baada ya kuwa nimepata supu ya maana nilijifungia ndani mara nilale mara niamke huku nikitafakari mambo mengi yasiyokuwa na ufumbuzi, kisha nikamtafakari Anitha na uamuzi wangu wa kukutana naye!!
Roho ilinidunda sana na kujiona kuwa najikabidhi kwa muuaji kirahisi, lakini ni kipi ningefanya iwapo hakuna anayeniamini na ushahidi wangu wenyewe ulikuwa utata mkubwa kuliko utata uliokuwepo. Picha na maandishi yaliyoandikwa na msichana ama mvulana asiyejua kuandika vizuri yangeisaidia nini mahakama zaidi ya kubambikiwa kesi nyingine ya kudanganya mahakama.
Eva na mama yake hawa ndio waliniumiza zaidi!!
Hawakuwa na kosa na huenda wangekuwa wameaminishwa kuwa mimi ni mtu mbaya, mwanangu Eva anaambiwa baba yako ni gaidi,.
Nikazichanga karata na kisha nikaitupa kete moja tu kubwa nay a mwisho kwa Anitha!! Kama ana mnapenzi ya kweli ama anatumiwa!!
Nikasinzia tena!!
Majira ya saa mbili nilitoka nyumbani na kwenda eneo la miadi ambalo nilimtumia Anitha katika ujumbe mfupi wa maneno.
Niliwahi maksudi ili niweze kusoma mchezo kama utakuwepo japo hiyo ilikuwa mbinu hafifu tu ya kujihami, kama wamejipanga tayari nisingeweza kuchomoka tena!!
Saa mbili na nusu kwa mujibu wa saa iliyokuwa katika mnara nilimuona Anitha akitembea kwa madaha kuelekea katika eneo nililomwelekeza.
Baada ya kutingwa na mawazo siku kadhaa sasa nilikumbuka kuwa kumbe Anitha ni msichana mrembo kiasi kile. Nalivalia vazi refu jeusi lililozichora nyonga zake vyema, vazi lile halikuishia kiunoni bali lilipanda hadi usawa wa kifua chake na kuzistiri embe sindano ndogo zilizong’ang’ania kukomalia pale kifuani na si mahali pengine, mgongo ulikuwa wazi lakini si wazi kiasi cha kuitwa uchi la! Ulifunikwa na nywele ndefu ambazo alijitambia kila leo!!
Macho yake yalizibwa na miwani yenye mahadhi ya kuvaliwa usiku, mkononi alibeba kipochi kilichofanana na miwani.
Hakika aliwaka!!!
Niliwahi kuwa naye katika mahusiano lakini sasa alipendeza zaidi!! Alichukua nafasi na kuagiza maji ya matunda!!
Akiwa anakunywa kinywaji kile hakuonyesha hofu yoyote machoni mwake.
Nikatazama juu mbinguni na kusema na Mungu!!
“Wajua kuwa sikuua, wajua kuwa mimi ni mja wako!! Nitazame baba huku ninapoelekea, kama ni sahihi nyanyua mguu wangu sasa lakini kama si sahihi baba nitegue nisiweze kuifikia meza ile” nilimaliza ile dua na kisha hatua moja hadi nyingine hadi nikaifikia ile meza.
Nilikuwa nimevaa zile nguo nilizonunua Tandale usiku uliopita!!
Anitha aligeuka na kunbitambua akasimama na kunikumbatia.
Marashi yake yakamfanya azidi kuwa mrembo, joto lake tulivu likanikumbusha mengi yaliyopita!!
Nikavuta kiti na kuketi mkabala naye sasa tukawa tunatazamana. Alipotoa miwani uso wake ulikuwa umechafuliwa na michirizi ya machozi.
Anitha alikuwa analia, na hapa akanyanyua mdomo na kuniambia jambo ambalo sikuwahi kuliwaza.
“Sam umekonda hivi jamanii!!”
Nikashangaa!! Akasema tena, “Yaani umepauka kabisa si wewe Sam. Pole sana.”
Alinibembeleza, nikajisikia vibaya badala ya kupata ahueni!!
Robo saa baadaye tukiwa tumeagiza vyakula, nilikuwa nikimuelezea juu ya Michigan na utata niliokutana nao nikiwa namtafuta Kindo.
“Kwa hiyo hukuniamini hata kidogo Sam ukaamua kwenda mwenyewe!! Ni lini utaamini kuwa Anitha yu upande wako.” Alilalamika, nikajifanya sikumsikia nikaendelea kumweleza mambo kadha wa kadha!! Yote haya nilimsimulia nikiwa sijaifungua bahasha mkononi mwangu!!
Ukafika wakati wa kuifungua bahasha, hapa akalazimika kuja kuketi katika ubavu wangu ili nimwelekeze kitu kimoja baada ya kingine ili atambue ni kitu gani namaanisha.
Picha moja baada ya nyingine, andishi moja baada ya nyingine…
MARA tukakatishwa na sauti ya mwanamke, “Heloow!!” tukadhani ni muhudumu wa ile sehemu tukapuuzia na kuendelea na mambo yetu!!
Niliponyanyua macho kwa mbali niliona kitu kama ninacho kifananisha na mzimu usiotakikana machoni kwangu!! Lakini wakati naendelea kuduwaa mara mbele yetu akaketi mwanamama akiwa anatabasamu. Tabasamu la kinafiki.
Nikamtambua upesi yeye na kisha nikapata jibu la yule niliyemfananisha alikuwa ni nani!!
Mbele yangu alikuwa ni mama yake Anitha na yule mzee aliyekuwa anakaribia kufika pale alikuwa ni mzee MATATA…..baba yake mzazi Anitha…….
Bahasha yangu mezani, najilazimisha kufumbua macho lakini hayafumbuki zaidi ili iwe ndoto!!
Nilikuwa maeneo ya Saveyi karibu na chuo kikuu cha Ardhi na mbele yangu alikuwapo mama Anitha na huyu anayemalizia hatua afike nilipokaa alikuwa ni mzee Matata.
Mapigo ya moyo badala ya kwenda kasi yakaanza kushuka kwa fujo!!
Jasho halikutoka lakini mwili ukawa wa baridi sana. Ganzi ikanishika.
NAKUFA!!!! Nikajiwazia…………..

JIFUNZE!!! DUNIA inapokugeuka mwamini Mungu pekee, yeye hadanganyi, yeye si mnafiki wala si msaliti!! Ukimwambia baba tenda miujiza anasikia palepale!! Sema naye kwa imani naye atatenda!!!
 
SEHEMU YA TISA
SEHEMU YA TISA
Mzee Matata hakuwa akikosea uelekeo alimaanisha kufika katika meza ambayo nilikuwa nimeketi na Anitha. Usoni alionyesha tabasamu lililojawa karaha tele, na alitembea kama asiyetaka kufika upesi eneo lile lakini alikuwa makini.
Nikajikuta nipo nje ya ujasiri na suruali yangu ikajikuta ikijitahidi kuumeza mkojo uliokuwa ukinitoka bila kuzuiliwa, kwa sekunde kadhaa nikafanikiwa kuuona uso wa Anitha….
Ajabu!! Alikuwa anayo hofu kubwa kuliko mimi, jsho lilikuwa likimtiririka na midomo ikimchezacheza.
Anaigiza!! Niliwaza huku nikiwa sijajua kipi cha kufanya, nisingeweza kukurupuka na kukimbia bila kutambua iwapo mzee Matata anayo silaha yoyote kwa wakati ule, maana bunduki yake ndogo alikuwa akiimiliki kihalali na angeweza kuitumia kunishambulia. Hata akiniua ataishia kupewa pongezi kwa kumuua muuaji na mbakaji, asingelaumiwa na mtu yeyote.
Nilibaki katika hali ileile ya kuinama nisijue wala kuamini iwapo, Anitha amenisaliti ama naota!! Kama kweli alikuwa amenisaliti nikajikuta lawama zangu nikizigeuzia kwa Mungu!! Mbona nilimsihi sana kabla sijajikabidhi kwa binti yule!!
“Si nilikwambia…..haya hii nd’o diskasheni…ooh Anitha hawezi kulaghai hawezi sijui nini haya hapa ndo mpo katika kudiskasi?” mama Anitha alihoji swali ambalo liliniduwaza.
Mwanga mwekundu wa taa haukunizuia mimi kuwatambua wazazi hawa lakini ajabu wao waliuliza kitu kingine kama vile hawanitambui!!!
Mzee Matata alishusha pumzi za nguvu sana, sikuwa nimemtazama machoni bado moja kwa moja, niliendelea kuinama huku kofia yangu ikinifunika.
“Mama!! Hivi mnataka kunichunga hadi lini?” alijibu Anitha kisharishari!!
Nikazidi kupagawa.
Ina maana wote wawili wananiigizia Mungu wangu weee!!
“Johnson!! Johnson, nisamehe bure kwakweli halikuwa dhumuni langu, naomba uniachie nafasi nizungumze nao hawa ni wazazi wangu!! Samahani tena Johnson!!” alinisisitiza Anitha, nikapagawa, inamaana yale mavazi yangu niliyonunua Tandale na hilo kofia vimenibadilisha kiasi kile?? Ilistaajabisha sana.
Sasa naitwa Johnson!! Nikashindwa kuelewa kama nisimame ama nisisimame, Anitha akaugundua udhaifu ule akanikanyaga mguu upesiupesi, bado sikuelewa nifanye nini. Akaniinamia na kuninong’oneza.
“Baba haoni usiku ana ‘night blindness’ hajui lolote na mama bado anajiuliza. Ondoka upesi ondoka tutawasiliana.” Kwa kauli hiyo sasa nikatambua nini kinaendelea.
Nikasimama na kuondoka nikiwa na uoga mkubwa na kichwa nikiwa nimekiinamisha. Bahasha yangu mkononi!! Mapigo ya moyo yakiwa katika hali ya kufifia na miguu ikitetemeka kwa fujo.
Anitha!!! Anitha steringi!! Ndo kitu nilichobahatika kukitamka kwa midomo yangu baada ya kujikuta nipo peke yangu mahali bahasha yangu mkononi na hakuna wa kunighasi.
Suruali ilikuwa imelowana bado, sikuamini hata kidogo kama tulikaa meza moja na mzee
Matata na mkewe na sasa nilikuwa nimeondoka tena.
Nikaikumbuka kauli ya mzee Matata tangu akiwa bosi wangu aliponieleza kuwa Anitha ndo binti yake kipenzi, hana la kusema juu yake na hataki baya lolote limtokee.
Naam!! Mtoto wa baba alikuwa ametumia nafasi kuniokoa!!
Nikazitazama mbingu na kumwomba msamaha Anitha kwa lolote lile baya nililowahi kumuwazia!!
Anitha alikuwa upande wangu kwa asilimia mia!!
Sikupoteza muda zaidi nikatokomea!! Si kuelekea katika nyumba ya wageni niliyofikia bali kwingine kabisa ambapo nilifahamu mimi na akili yangu!! Zile nguo nilizopewa na Enock yule rafiki msaliti nikaamua kuachana nazo. Cha muhimu kilikuwa mimi na bahasha yangu!!
****

Majira ya saa nne usiku nilikuwa nikiusaka usingizi kwa juhudi zote, suruali yangu nilikuwa nimeifua na kuinika chini ya feni ili kufikia asubuhi iwe imekauka.
Niliwaza mengi na kisha kukumbuka kuwa pesa ilikuwa inayoyoma hatimaye. Hili likanitia wasiwasi maana pasi na pesa bila shaka njaa ingeniumbua na kujikuta naomba msaada, msaada kutoka kwa mtu yeyote yule pasi na kujua kama ni mtu hatari ama salama!!
Asubuhi kama nilivyopanga wakati usingizi unabisha hodi nikamkumba muhudumu wa nyumba ile ya kulala, huyu hakuniletea ugumu katika kuniazima simu yake. Nilimwambia kuwa kuna mtu nataka kumbipu!!
Nilipopigiwa simu nikakimbilia chumbani kwangu na kisha kwa tahadhari kubwa nikaipokea simu!!
“Nilijua tu ni wewe na hakika nilisubiri sana kuzungumza nawe!!” Anitha kutoka upande wa pili alizungumza. Sauti yake ilikuwa inaunguruma kiasi na nhakika hakuwa sawa na siku nyingine. Kabla sijamuuliza lolote akaendelea.

ANITHA.

HUWA ni jambo gumu sana kuupina ama kuubatilisha usemi wa damu nzito kuliko maji!!
Lakini hubidi kuwa hivyo pale upendo unapochukua nafasi!!
Tukio la jana ni kama ndoto na hata muda huu naamini ni ndoto labda ni wewe wa kuibatilisha ndoto hii, ndoto ya mwanamke kujikuta katika maamuzi ya kuachana na usemi wa damu nzito na hatimaye kuubadili kuwa penzi zito kuliko damu!!
Sijui nilitoa wapi ujasiri ule wa kujitetea mbele ya baba na mama yangu!! Na wala sikutarajia ujio wao usiku ule tena wakinifumania mimi na wewe. Ambaye wanakuita mtu hatari.
Sam, nafsi yangu ilijawa na baridi, lile barafu la ubaridi likazidi kuvimbiana na nikajihisi kukosa amani kwa zana kuwa waweza kuniita msaliti!!! Naam!! Ni mwanadamu gani awezaye kuamini eti mama alishika simu yangu nikiwa nimeenda kuoga akausoma ujumbe uliokuwa umenitumia kunielekeza mahali tulipotakiwa kukutana. Yule mama akawa mjuaji zaidi akaangalia huduma za kipesa katika namba hiyo na kugundua kuwa ulikuwa ukijiita Gabriel Madaraka. Kwa hili naomba nikupongeze sana Sam, yaani laiti kama ungekuwa umetumia namba ambayo umeisajili kwa jina lako basi nadhani ule ujio wa wazazi wangu usingekuwa wa kupooza namna ile.
Mama akamshirikisha baba yangu juu ya mimi kutaka kukutana na mwanaume majira ya saa tatu usiku maeneo yale tuliyokutana. Nadhani wajua ni jinsi gani baba yangu ananipenda kwa dhati, hili kwako si jipya hata kidogo kuwa hataki baya lolote linitokee, akasikia natarajia kukutana na mwanaume ilhali nimewalaghai nyumbani kuwa naenda katika majadiliano ya kimasomo na rafiki zangu. Wazazi wakaitegea mida na hatimaye wakatufuma katika hali ile.
Najua kuwa usingepatikana muda wa mimi kusimulia haya na unielewe iwapo wazazi wangu wangekugundua na kukukamata, na jambo hili lingenifanya niwe adui yako namba moja maisha yako yote!! Sikuwa tayari nikaamua nkuwakosea heshima, nikakutetea na hatimaye ukaondoka.
Sam!! Nilibebwa mzega mzega nikaingizwa katika gari na kuendeshwa moja kwa moja hadi nyumbani!!
Hakuna jambo baya kama kupingwa na wazazi wote wawili katika jambo unalojaribu kulifanya, katika utetezi hakuwepo aliyesimama upande wangu!! Nilipigwa sana na utu uzima wangu huu, baba alinipiga kwa kutumia mkanda huku mama akinipiga vibao na makofi!! Hasira za baba zilikuwa juu zaidi, baada ya kunipiga sana hakutaka kulala nyumbani. Akatoweka na mama naye akaondoka kwenda kumtafuta.
Nadhani waisikia sauti yangu ilivyo mbaya, hii ni kwa sababu nina vidonda mdomoni, walinipiga sana Sam. Lakini niliamua kubeba maumivu haya kwa ajili yako!! Nikateseka lakini uwe na imani kuwa sijawahi kukukana hata siku moja!!
Kosa walilofanya wazazi wangu ni kujiridhisha kuwa Anitha mimi sijakomaa kiakili, wakadhani siyajui mapenzi na sina uamuzi wangu wangu wa mimi kama mimi!!!
Nilitarajia utanipigia simu Sam usiku ule niweze kukushirikisha katika jambo nilililokuwa nimefikiria lakini sikupokea simu yako na nililazimika kuchukua maamuzi ili tu haki ipatikane, Sam mimi nasomea sheria na haki za binadamu. Lazima kuna kitu katika mlolongo huu, nami nataka nitambue kuna nini hapa katikati, hii ni nchi yetu Sam na sis indo vijana kama kuna uvundo wowote unaendelea na vijana tunafumbia macho, amini umri na elimu zetu hazitusaidii kitu chochote na ni watumwa wa elimu ya mkoloni huku tukiwa vibaraka wa ukoloni mamboleo. Maumivu hayakunizuia kukivamia chumba cha wazazi wangu ambacho haikuwa mara ya kwanza kuingia. Ile imani ya baba yangu kwangu na kuonyesha mapenzi waziwazi sasa ulikuwa wakati muafaka wa kuitumia. Nikafungua sanduku ambalo nilizijua namba zake za siri, naam!! Nilichokitarajia nikakikuta!!
Unadhani ni kitu gani kinachokwamisha mkakati huu zaidi ya pesa!! Unadhani kwa nini Eva na mama yake wapo mahali usipopajua zaidi ya pesa? Sam Pesa haina mdomo lakini ikipaza sauti basi itasikika dunia nzima na wanyonge watatetemeka!!
Pesa inaficha maovu na pesa hii inatibua haya maovu!!
Pesa nyingi inaweza kuficha maovu milele lakini akili nyingi na pesa kidogo hutibua mipango hii!! Sijielewi mimi lakini natambua kuwa Sam wewe unao uwezo mkubwa sana wa kufikiri, naam!! Kwa pesa hizi kidogo nilizochota naamini harakati za kuirejesha amani, kutibua fumbo hili gumu na kumrudisha mama Eva na Eva katika himaya yako basi zote zitawezekana!!
Michigani, Kindo, Ezekiel, Alvin vyote hivi vitajulikana!!
Sam! Baada ya kuiba pesa hizo kutoka kwa wazazi wasiofungamana nami!! Nilitoweka mlinzi akiwa amelala!!
Sasa nane usiku, kila kiungo kikiwa kinauma kutokana na kipigo, macho yakikosa nuru kutokana na uchovu, bado niliweza kuzurula mitaani.
Nakukumbusha kuwa Mungu ni muweza wa yote haogopi usiku wala mchana maana vyote alivibuni yeye!!
Mungu alinisimamia na hadi muda huu unanipigia simu nipo Royal Hotel Temeke chumba namba 18, Anitha huru katika fikra na maamuzi huru!!! Simu yangu iliingoja simu yako tu ili niweze kuizima na rasmi nakutambulishia namba yangu mpya isiyojulikana na yeyote zaidi yako ni 07...675493. nimeamua kuungana na wewe Sam, kama ni batili wazo hili na niadhibiwe nikiwa hai. Na kama nikifa kabla ya kupewa adhabu basi nifanyiwe alichofanyiwa yule dada katika simulizi uliyoiandika na ikavuta maelfu ya watu..”NIKIFA MAITI YANGU IPEWE ADHABU!!”
ANITHA AKAMALIZA!!!!

UPANDE WANGU
Nilibaki kuduwaa nisiamini nilichokisikia, sauti kakamavu japo inayokoroma kutoka kwa Anitha ilibeba ujumbe mzito sana. Harakati nilizokuwa nasisitiza kila siku katika makala zangu, ule uzalendo uliopotea kwa vijana wengi na hali ya kuthubutu sasa niliionja tena kwa Anitha. Na kubwa zaidi yale mapenzi wanayodai kuwa yamelogwa na kuwa ya kudanganyana sasa niliyashuhudia katika upande wa mapenzi ya kweli.
Anitha alikuwa mwanaharakati!! Nilizungumza naye kwa kina akanielekeza juu ya hiyo hoteli ilipo.
Sikupoteza muda nikaivaa ile nguo yangu ambayo siku iliyopita ililowana mikojo ya kiutu uzima. Moja kwa moja nikaenda Temeke kukutana na anitha.
Wakati huu sikumtilia mashaka tena!!
Nilifika hadi chumbani baada ya kuruhusiwa kuingia. Anitha hakuwa akidanganya jambo lolote lile, uso wake mweupe ulikuwa mwekundu, midomo ilivimba sana na yale macho yaliyowahangaisha wanaume wengi sasa hayakuwa na mvuto wowote. Alijaribu kutabasamu lakini akaishia njiani ni kama alipatwa na maumivu kinywani. Nikajisikia huruma nikamkaribia, nilimpooza kwa maneno ya hapa na pale na kisha nikakiri mbele yake kuwa yeye alikuwa ‘steringi wa kike’ katika filamu asiyehofia chochote.
“Anitha sasa vipi kuhusu shule….” Nilimuuliza, badala ya kujibu akalazimisha tena tabasamu.
“Sam!! Tunasoma ili kupambanua mambo katika jamii inayotuzunguka, na si kupata shahada ya makaratasi huku tukishindwa kutatua matatizo katika jamii yetu. Huku nilipoamua kuingia ni shule kubwa zaidi ya hiyo ya makaratasi bila uwezo wa kuchanganua na kupambanua mambo!!!
Unamfahamu Nelson Mandela?? Alifungwa akiwa na miaka mingapi? Alifungwa gerezani miaka mingapi?? Je alipotoka alitumia makaratasi ya shuleni kulipigania taifa lake alilolipenda?? La!! Ile shule ya kunyanyaswa ilikuwa kubwa kabisa katika maisha yake!! Ama labda nikuulize ni wanafunzi wangapi wanaopata daraja la kwanza vyuoni na nchi haiwatambui kwa lolote lile zaidi ya sifa wapatayo siku ya matokeo?? Lakini ni nani awezaye kumsahau yule mwanafunzi kijana kabisa kutoka chuo cha Havard Marekani aliyebuni mtandao wa kijamii wenye nguvu kupita yote duniani?? Nani wa kumsahau Mark Zuckerberg na facebook yake.? Unadhani Mark alitumia makaratasi yake ya kufaulu!! Tuutumie muda uliopo vyema ili tusijutie wakati ujao!!” alijibu kwa kujiamini Anitha hadio akanishangaza, nikaamini kwa kile alichokisema kuwa elimu ya darasani bila uwezo wa kutatua tatizo ni buree!!
Tulizungumza mengi!! Majira ya saa kumi na mbili jioni tukawa na maamuzi, nikaondoka na kwenda kukata tiketi kwa ajiri ya safari ya kwenda Iringa. Kwa lengo moja tu kuitambua Michigani ambayo hadi wakati huo hatukujua kama ni hoteli, casino ama mgahawa!! Lakini tulitaka kuijua Michigan.
Tuliamua iwe siku inayofuata ili kuokoa maisha ya Eva na mama yake ambao lazima sumu za kwenye magazeti kuwa mimi kibaka tena muuaji na mlawiti zilikuwa zimeathiri akili yao kupindukia!!
Nilifanikiwa kupata tiketi mbili za kukaa katika siti moja. Nikiwa nimeandika majina ya bandia!!
Tulilala kimya kila mmoja na tafakari yake, nilikuwa na amani kuwa nipo na mtu sahihi kabisa katika harakati hizi za kunirejeshea amani iliyotoweka na pia kunirejeshea familia yangu!!!
Alfajiri tulikuwa tayari kwa safari ile, safari matata kabisa kila mmoja akiwa mgeni katika mkoa wa Iringa!
Safari ya kwenda kutafuta kitu tusichokijua, lakini kitu tulichoamini kuwa kitatuletea majibu ya maswali yetu ambayo yalikuwa gizani nasi tukiwa gizani huku tukilazimika kuyajibu ili utokee mwanga!!!
Badala ya kupata siti mbili zilizoungana kwa ajili yetu tulijikuta tukiwekwa katika siti ya watu watatu!! Hatukulalamika kwa sababu tulikuwa na shida ya kusafiri!!
Pembeni yetu alikuwepo msichana machachali ambaye alizoeana na kila abiria kana kwamba ni ndugu yake!! Na sisi tuliokuwanaye siti moja alitulazimisha hadi tukamzoea, hadi kufikia Mikumi Morogoro ni kama alikuwa ndugu yetu wa karibu!!
Hapo nikatumia nafasi ya mazoea hayo nikauliza swali.
“Hivi Michigani huwa ni Iringa ama Mbeya maana niliisikia nikiwa Dar es salaam enzi hizo.” Swali lile lilimfanya acheke na kisha kwa kutuonyesha ukomavu wake alitoa majibu yake!!
“Yaani Michigani zimebakia picha tu, aisee paliteketea moto mbona!! Miezi tisa iliyopita mbona ilikuwa mshikemshike, sema uzuri hakuna mtu aliyekufa!! Kwa hiyo Michigani imebakia stori tu hakuna kitu kama hicho kule kama hukubahatika kupaona basi tena watafute akina sisi malijendari wa miji tukuonyeshe picha!!” alijibu kwa kirefu kisha akatoa cheko refu!!
Anitha akanibinya kuniondoa katika mshangao ule!! Lakini na yeye alikuwa ameduwaa!!
Michigani iliteketea miezi tisa iliyopita, katika karatasi lililoandikwa jina la kindo limendikwa miezi tisa iliyopita.
Kuna picha ya mahali panaitwa Michigani!!!
Mkasa ukaingia ugumu mwingine!!
Tunatafuta mahali ambapo pamebakia historia!!!!
Nikalegea kwa uchovu na kukata tamaa!!
***JIFUNZE!!...UZALENDO ni hali ya kuwa tayari kupigania kitu kwa manufaa ya wengi. Lakini Uzalendo huja hata katika mazingira ya kawaida, je wewe ni mzalendo kwa familia yako? Je una uzalendo kwa umpendaye ama ndo akiwa katika ugumu unajiepusha naye!! Taifa lako ni kubwa sana kulifanyia uzalendo, lakini vipi kuhusu jamii ndogo inayokuzunguka, vipi kwa watu wema kwako??
 
SEHEMU YA KUMI
SEHEMU YA KUMI
Safari iliendelea huku dada msema mengi akiwa anazidi kutuburudisha kwa tuo. Mara alete simulizi hii mara ahamie hii, Anitha alikuwa wa kwanza kuyachoka maongezi na uchovu wa safari. Akasinzia!!
Kisha Yule dada naye baada ya porojo za muda mrefu na yeye akasinzia!!
Binafsi sikuwa na hamu hata kidogo ya kulala, na macho yalikuwa angavu kutazama hapa na pale ndani na nje ya basi lile.
Ninakumbuka jina lake ni Super Feo!!
Tulipofika Mikumi basi lilisimama katika hoteli fulani, kusimama huku kukamzindua tena yule dada msema sana. Akaanza kusimulia juu ya hoteli ili kuonyesha kuwa anaijua sana. Sote tulitelemka na kujipatia mahitaji yetu, kisha tukarejea ndani ya basi tena kuendelea na safari ya masaa kadhaa, tukaupita mlima Kitonga na hatimaye Iringa ikaanza kunukia.
Nikamnong’oneza Anitha kuwa tusishukie Iringa bali twende mbele kidogo aidha Mafinga ama Makambako kabisa.
Aliniuliza kwa nini lakini sikutaka kumweleza kwa kirefu, kichwani mwangu niliamua kuishi kwa hofu tena bila kumwamini kiumbe aitwaye mwanadamu.
Dada msema mengi alikuwa ameahidi kuwa mwenyeji wetu mjini Iringa na kama ikifaa atatuonyesha picha za Michigani na eneo lenyewe.
Lilikuwa jambo ambalo tulikuwa tunalihitaji sana, lakini hapakuwa na haja ya kuingia katika hatari usiyojua kama ni hatari na kushindwa kujihadhari na mwishowe kuambulia mabaya!!!
Tulipofika Iringa yule dada alijikuta akishuka yeye pekee nasi tukiunganisha hadi Mafinga!!
Huko tukatelemka, bila kupumzika tukachukua gari ndogo ikatusafirisha kurejea Iringa tena!!
Hatimaye majira ya saa kumi na mbili unusu jioni tulikuwa Iringa mjini.
Hoteli inayokwenda kwa jina la MR ndo ilituhifadhi usiku ule katika mji ule ambao una baridi haswa.
Ilikuwa hoteli yenye hadhi yake na tuliamua kujihifadhi katika hoteli ya hadhi ile kwa sababu ilitulazima kwanza kuupata usalama kabla ya kuendelea na jambo lolote lile.
Hakika tulikuwa salama!!! Lakini hatukulala kabla ya kuamua jinsi ya kuianza safari yetu!!
Nilimweleza Anitha kuwa ule ulikuwa usiku wetu pekee wa kuwa pamoja kabla hatujatengana na kisha kuwa tunaonana mara moja moja iwapo inabidi!!
“Anitha, unajua fika kuwa mimi natangwaza magazetini nikishushiwa kesi lukuki ambazo sihusiki nazo. Najua hata wewe utatangazwa kupotea labda kutokana na kutoweka nyumbani ghafla lakini taarifa zako haziwezi kuwa nzito kama zangu. Hivyo kwa upande wako ukiamua kufanya jambo moja tu la kuubadilisha mwonekano wako hakuna ambaye atakuwa na shida na wewe. Na ninakwambia kuwa inatulazimu kuwa mbalimbali ilimradi tu mkakati usije kukomea njiani. Kesho nitakuwa nawe katika kuitazama Michigan kwa jicho la tatu lakini baada ya hapo Anitha utalazimika kuwa pekee nami kuwa mtu wa kupewa taarifa na kutoa ushauri!!” nilimweleza kwa kirefu zaidi na hakuonyesha kushtuka hata kidogo.
“Niliamua kuja huku kwa hiari yangu mwenyewe!! Sikulazimishwa na litakalotokea huku ni juu yangu!! Usijali Sam mimi nitasimama imara kukabiliana na lolote.” Hiyo ilikuwa kauli kuu ya mwisho kabla kila mmoja hajapitiwa na usingizi!!
MKAKATI WA UKOMBOZI
MAJIRA ya saa nne asubuhi tulikuwa eneo ambalo lilijulikana kama Michigan miezi kadhaa nyuma, sasa liliitwa Semtema na katika eneo hilo kilikuwepo chuo kikuu cha Tumaini.
Hapakufanania hata kidogo na hali ya hatari, kila mmoja alikuwa na mambo yake eneo lile.
Semtema!! Tulilazimika kujaribu kuuliza kwanini paliitwa hivyo, wenyeji wakadai kuwa kwa kihehe jina linaloanzia se linamaanisha mwanamke, hivyo kama pangeitwa Mwamtema, hii ingesimama badala ya mwanaume!!
Ilistaajabisha. Hiyo Michigan mbona haipo sasa. Wenyeji wakakana kujua kuhusu Michigan na wengine wakasema walisikia tu uvumi.
Yule dada msema mengi alitudanganya ama!!! Nilijiuliza huku nikizidi kustaajabu.
Majira ya saa sita tuliamua kuzurura zaidi na kutafuta chakula. Bila kujua wapi tunaelekea tulijikuta katika eneo ambalo lilifahamika kwa jina la Isoka. Wenyeji hawakuwa na haja ya kutueleza lolote mtaa huu ungeweza kuuita uswahilini.
Kona hii bangi, mara gongo na kona kona nyingi bila kukutana na mtu anayejali ya mwenzake!!
Tuliamua kutumia eneo lile ili kufaidika na ushushushu wa watu wa uswahilini. Baada ya chakula ilikuwa zamu ya Anitha. Akamuuliza mama muuza chakula juu ya Michigani.
Uzuri wa wahehe, wabena na wakinga ambao ndo wengi katika mkoa wa Iringa, ni wakarimu sana na wanapenda kuzungumza.
Huyu mama hapo tukawa tumemfikisha!!
Na yeye kama yule mama wa kwenye basi aliyetusimulia juu ya Michigani huyu naye aliielezea kadri awezavyo. Hapo sasa tukapata jibu kuwa huenda kule Semtema tulikuwa tunapata majibu kutoka kwa wanachuo ambao wengi si wenyeji wa Iringa na hawaujui mkoa ule.
Maelezo ya huyu mama yakaambatana na ucheshi kidogo. Ni kweli alisisitiza kuwa Michigani haikuwepo tena Iringa, lakini kicheko kilikuja alipomfananisha Masawe kama mshamba!!
“Masawe nd’o nani tena?” Anitha alimuuliza.
“Yupo mchaga mmoja hivi ambaye amekimbia uchagani huko si unajua walivyo wale kwa maduka!! Amefungua duka huku eti akaliita Michigani, kiduka chenyewe kibovu!! Sijaona wachaga wasiojua kufanya biashara kama Masawe yaani!! Ukienda leo mara mafuta hakuna, kesho kiberiti hakuna!! Hovyo kabisa nimemuhama. Michigani ilikuwa enzi hizo, ye analeta leo khaaaa” Alijibu kwa sauti ya juu yule mama na kuyapuuzia yote aliyokuwa anayasema kama hayana maana!!
Tulimdadisi huku tukimuunga mkono kila alipotaka kucheka nasi tulicheka!!
Tulipomaliza tukamlipa pesa yake na kuondoka.
“Mh!! Mama mcheshi yule.” Anitha alinisemesha. Badala ya kumjibu nilimtazama na kuhisi mwenzangu hajang’amua kitu fulani, kuwa yule mama ni zaidi ya ucheshi aliotupatia!! Lipo neno la ziada!!
Michigani!! Michigani ya Masawe!! Huyu Masawe lazima tu atakuwa anajua jambo kuhusiana na Michigani, huwezi tu kuita Michigani bila kujua kwanini unaita.
Anitha akagutuka na kusawazika usoni katika namna ya kustaajabu!!!
Tukapitia kibanda cha kutengeneza nywele.
Anitha akaingia mimi nikabaki nje kungoja!!
Alipotoka hakuwa na nywele hata kidogo na hakutisha wala kuchekesha kwa muonekano ule lakini alikuwa amebadilika na asiyemjua asingeweza kuamini kuwa ni Anitha!!
Akiwa katika hali ile ile tulifanikiwa kukifikia kibanda cha Michigani. Kilikuwa kibanda kidogo tena pa kichovu sana. Tulikata tamaa huku tukijiaminisha kuwa maneno ya yule mama ni kweli kabisa.
Katika ya wachaga waliochoka kimawazo huyu alikuwa mmoja wao!!!
Anitha akanipa moyo kuwa tukae mahali na kungoja lakini sikuwa nahitaji la ziada tayari nilikata tamaa.
Masawe anauza pipi kifua, ubuyu, na keki ndogondogo!! Wa nini sasa huyu!!
Hana maana Anitha!! Nilimwambia!!
“Sasa unadhani Sam ni wapi tutampata huyo mwenye maana?”
“Anitha ujue tunapigwa baridi saa mbili usiku hii, sikia kwani ile pesa tuliyoiacha ndani ni shilingi ngapi? Na je una pesa ya dharula tuachane hadi kesho tena nitakaponunua simu nd’o tuwasiliane!!”
“Ni milioni nne ile….”
“Weee Anitha umemfilisi mzee Matata we mtoto.”
Hakujibu na badala yake tukakubaliana kuwasiliana siku inayofuata!!
Nikamsindikiza hadi katika hoteli nyingine ya hadhi ya kawaida nami nikarejea MR Hoteli huku matumaini yakianza kufifia.
Matumaini ya kumrejesha Eva na mama yake katika himaya yangu!!
Matumaini ya kuwaaminisha watanzania kuwa sikufanya yote yali yaliyoandikwa gazetini.

****

Saa nne asubuhi tayari nilikuwa na simu, nikaandika namba za simu za Anitha alizokuwa amenipatia!! Upesi akapokea.
“Sam!! Sam!! Mvumilivu hula mbivu!!” alianza hivyo na hapo akaanza kutiririka.

ANITHA…….
“Kuwa wamoja haimaanishi hata mioyo yenu itaegemea upande mmoja, iwapo itakuwa hivyo basi mmoja akianguka nyote mnaanguka, mmoja akikata tamaa wote mnakata tamaa.
Ningeweza kuwa kama wewe Sam, ulivyokata tamaa nami nikate tamaa, lakini kama ulidhani kuwa nililala, mimi sikuwa tayari kulala huku moyo wangu ukinisukuma kufanya jambo fulani. Nilirejea kule uswahilini Isoka. Nilirejea na kuitazama hiyo inayoitwa Michigani Sam, nilikuwa makini sana kutazama huyu mchaga wa kuitwa Masawe anafunga duka saa ngapi, anaishi wapi kama ikibidi na muonekano wake maana jana alikuwa kwenye kidirisha hatukumuona vizuri.
Sam. Kwa duka ama niite kiduka kama kile unaweza kufuatwa na magari mawili!! Kwa hatari ipi iliyopo hadi iwe hivyo, sijaiona sura yake kutokana na giza lakini sam. Hapana mi nakataa yule Masawe yule…sijui lakini huenda anajua juu ya Michigani. Ama la anazo biashara za magendo anafanya na hicho kiduka ameweka kama gelesha tu!!” alinieleza kwa hisia huku akiahidi kuwa analivalia njuga suala hilo hadi ajue la ziada kuhusiana na kiduka kile.
Sikujua Anitha ataweza vipi kumchimba Masawe ambaye anaonekana kujikita katika hiyo biashara yake ya duka!!
Nilitamani kumuuliza lakini nikaona huu ni ukatishaji tamaa.
Nikampa hongera kisha nikakata simu na kujipanga vyema kitandani!!!
Bado nikiwa siamini kama kuna lolote linaweza kutokea katika kile kibanda walichokiita Michigani.
Nikiwa nimekubaliana na Anitha kuwa mimi nitaweza kuwa natoka mida ya usiku tu si vinginevyo kulingana na usala wangu!! Basi niliendelea kuwasiliana naye mara kwa mara kila palivyokuwa na tatizo lolote.
SAA NANE MCHANA. SIMU KUTOKA KWA ANITHA.
Wakati huu alizungumza kwa tahadhari kubwa sana. Sauti yake ni kama ilikuwa inanong’oneza.
“Sam, nimefanikiwa kumfuatilia Masawe na gari ile iliyomchukua usiku. Sam yule wa dukani si Masawe, Sam niamini ninachokwambia, Masawe si yule wa dukani, kuna mtu ameniambia kidogo juu ya uhusiano wao lakini hatuwezi kuzungumza katika simu nitakueleza nilichofanikiwa kujua juu ya Masawe. Sam kuna kitu kinazunguka hapa hata wana Iringa hawakijui!! Nipo mitaa ya huku wapi, sipajui ni wapi Sam lakini ndo huku anapokaa Masawe mwenye lile banda wanaloliita Michigani. Muonekano wake hauendani hata kidogo na kile kiuchafu….kuna picha nimefanikiwa kuipiga japo pamewekwa onyo kuhusu kupiga picha eneo hili. Nimekutumia katika barua pepe!!!.......
(Mara anitha akanyamaza…nikamuita hakunijibu!!! Kama sekunde kumi zikapita Anitha akaanza kuongea huku akitetemeka.
“Sam….Sam..kuna wanaume wanne, yeah wanne wamevaa suti nyeusi wawili nyuma yangu na wawili mbele yangu….Sam wanakuja kwangu hawa…macho yao wameziba kwa miwani…Sam nakamatwa….Sam Sam……Sam weeeee nakamatwa mimi Sam!!.......”
Ghafla nikasikia Anitha akipiga kelele, na pale simu ikakatika.
Nilipojaribu kupiga hakuwa akipatikana tena!!!
Maajabu haya!! Nilijaribu tena na tena kumpigia Anitha lakini simu haikupatikana.
Mungu wangu weee!! Mtoto wa watu nitajibu nini kama si kizaazaa kingine tena kikubwa zaidi.
Nilikaa, nikasimama, nikaingia bafuni na kutoka bila kufanya lolote.
Wanaume wamevaa suti nyeusi mbele na nyuma wakamzunguka!! Mungu wangu, sasa walijuaje kuwa anawafuatilia.
Nilitoka haraka katika hoteli ile na mimi nikaizima simu yangu kwa hofu ya kusomwa mtandao wa mahali nilipokuwa!!
Moja kwa moja nikaingia mitaani, nikazama katika kibanda kinachotoa huduma za Internet, upesi nikafungua barua pepe yangu!!
Nikakuta kweli Anitha alituma picha.
Picha ikafunguka!!
Hamad!!! Ilikuwa picha ya mtoto fulani ambaye niliwahi kumuona tena katika picha!!
Picha zilizokuwa katika fundo la makaratasi niliyochukua kwa Ezekiel!!
Palepale nikajipekua na kutoka na ile picha.
Naam!! Ilikuwa yenyewe na ilifanana kwa kila kitu.
Kuna nini hapo Iringa? Iringa kubwa sijui hata ni wapi alikuwepo Anitha hadi akafanikiwa kuchukua picha ile!!
Baada ya malipo nilikuwa kama nakaribia kupandwa na wazimu!! Nikajilaumu kwa kumwacha Anitha peke yake lakini kwa upande mwingine nikaona ni sawa kwa sababu kama tungeambatana tungekamatwa wote na huo ungekuwa wakati mbaya pengine kuliko yote katika maisha yangu!!!
Nilijaribu kwa mara nyingine kuwasha simu!! Nikajaribu kupiga simu ya Anitha lakini tatizo likawa lilelile. Nilipokata nikakumbana na ujumbe katika simu yangu.
“UTAKUJA KUMCHUKUA MWENYEWE!!” ujumbe uleule kama nilioachiwa wakati wakimchukua mama wa watoto wangu!!
Mama Eva!!....
Ilistaajabisha sana, hawa watu walikuwa wametambaa kiasi kikubwa hivyo????
Sasa nafanya nini? Hilo likawa swali ambalo sikuweza kupata jibu mara moja!!!
Nikaumiza kichwa zaidi na kufikiria ni nani anaweza kunisaidia.
Kwa mara ya kwanza tangu niingie katika kshkash hilo nikakumbuka kumpigia simu. Mama Samson!!
Mama yangu mzazi!!!
Nilikuwa nimeegemea chini ya mti simu ikiwa inaita……..
Kwa mara ya kwanza haikupokelewa!!!
Nikapiga tena, safari hii ikapokelewa.
Nikasikia kelele nyingi sana zinazofanana na vilio. Hatukuwa tukielewana, ikabidi mama akate simu.
Nikapiga tena, sasa alipokea na tulijitahidi kusikiana vyema.
“Nipigie baadaye nipo msibani!!!”
“Mama….” Nilimuita.
“Nani wewe mbona kama eeeh ni nani?” nilimsikia mama akibabaika, ni kama alikuwa amenigundua lakini hakuweza kusema moja kwa moja nami sikutaka kumhadaa.
“Sam hapa mama mwanao Sam.”
“Koma koma….ukome kuchezea akili yangu we mtoto…..ni nyie mmemuua mnanitania sivyo!!!” mama alinistaajabisha kwa majibu yake!!
“Mama mimi ni Sam mama, mama ni mimi.” Nilibaki kusisitiza tu. Mama hakujibu kitu nikalazimika kufanya jambo moja kuu la mwisho la kumsisitiza kuwa mimi ni Sam.
“Mama mimi ni Mwikwabe..” nikamtajia jina ambalo alinitungia utotoni. Hapa nikamsikia mama akihema kwa nguvu.
“Sam…..ni wewe mwanangu!! Mbona mnanichanganya, na huyu wanayemleta kwenye jeneza ni nani sasa.” Alitokwa na kauli ambayo ilinitoa machozi, mama alikuwa amechanganyikiwa kweli na nilijua jinsi gani akili yake imeghafirika.
“Mama sauti hii unayoisikia ni ya mtoto wako wa kumzaa, nipo hai mama. Kama utaletewa mwili hakikisha unautazama kwa makini mama utaamini kuwa nani ni mwanao.” Nilijieleza.
“Sam si wanasema mwili hauna kichwa sijui kimefanyanini huko na huku siwaelewi ujue, yaani Sam nimechanganyikiwa mwanangu!! Mdogo wako amepoteza fahamu hadi leo, baba yako ananiita mimi mchawi eti nimekutoa kafara Sam wangu!! Kweli nilivyoteseka na wewe Sam miezi na miaka leo hii nikutoa kafara Sam. Nilivyobangaiza pesa uende shule na ukapata lazi bado nikutoa kafara. Kweli baba yako ni wa kusema haya mbele ya watu kabisa ananitukana kiasi hicho na watu wanaamini kuwa nimekuua. Sasa wameweka kikao wananidai kichwa chako, eti kama sikitoa kichwa chako basi wananikata changu!! Si uje Sam uniokoe mama yako huku!! Ni wewe sam ujuaye mimi nina nafasi gani kwako Sam. Kama kweli upo hai Sam nakuomba ufanye jambo hili dogo kabisa kwangu!!! Njoo uwaumbue wazee hawa wanaoniita mimi mwanga tena mchawi niliyeshindikana!!” mama alimaliza kuzungumza huku akijizuia kulia, mimi kwa upande wangu sikuweza kujizuia, nilikuwa nalia. Sauti ya mama iliniumiza, waliomwita mama yangu mchawi waliniumiza zaidi nafsi.
Hadi mama yangu anakata simu nilikuwa katika mgagagiko wa aina yako!!
Mpalanganyiko usio kifani.
Anitha amekamatwa na niliisikia sauti yake ikiomba huruma yangu katika simu.
Mama yangu mzazi naye anazushiwa kuwa ameniua angali nipo hai!! Nilijua ni hila za watu wale wabaya kunifedhehesha na kuisababisha jamii nzima inilaani!!
Lakini kwanini sasa wamemgusa hadi mama yangu!! Kwanini uchungu wangu nichangie na mke wangu, mwanangu Eva, Anitha na sasa mama yangu mzazi.
Mwanamke mwenye thamani kwangu kuliko wanawake wote!!!
**JIFUNZE!! Wakati wa malalamiko yako uyatoayo kila siku na kujifanya wewe unaonewa kupita watu wote, kujifanya kuwa ni wewe umetendwa kupita watu wote duniani. Wapo wengine ambao kilio chao ni kikubwa zaidi na hawana amtu wa kuwasikiliza kama ilivyo kwako wewe!! Hawana msaada wowote na badala yake wanalia na nafsi zao!!
Wakati unajifikiria wewe kumbuka kumfikiria na jirani yako.
Huo nd’o UPENDO!!!
 
Kwetu hakuna umeme Leo cm haina chaji
Baadae ndugu
...............
Tumia njia hii
65789e9fd5d5232ede94d11aeae699d2.jpg
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom