Makapuku Forum

Makapuku Forum

Habarini makapuku;
Natambua uwepo wa bitoz, Jimena, musolin5, werrason na shululu kwa wakati huu.
Musolin5 ametukumbusha jambo muhim sana lililotuunganisha tukawa family, hakika ni family sababu kila siku lazima tukutane, tusalimiane, tufundishane, tukosoane nk.
Mshikamano wetu umekua sana ndani na nje ya kf, nami nasema hongera kwa waasisi na members wote.
Kama tujuavyo wanadamu hatukosi mapungufu, hata kwetu hujitokeza, na yakijitokeza hurekebishana na maisha yanasonga. Jambo la msingi ni tumefahamiana kiasi flani na hii imetupa fursa ya kuvumiliana na mambo yanasonga.
Jambo lingine; tulikuwa wengi lakini kwa sasa tuko wachache LAKINI TUPO IMARA KULIKO WAKATI WOWOTE, cha msingi ni kushikamana zaidi na KUONGEZA UBUNIFU NA LUGHA ZA STAHA MIONGONI MWETU.
Wale ambao hawaonekani aidha;
1) kukosa uvumilivu
2)kutingwa na majukumu
3)kukosa mb
4) au hata kujitoa
Hili lisiwe tatizo sisi tuendelee tukiwa wamoja na kuleta ubunifu ili kuleta mvuto zaidi. Na ndg zetu wakirudi pia itakuwa jambo la kheri kwetu na wasiporudi isiwe tabu pia.
Ni maombi yangu kama family tutambue tuna wajibu wa kuchukuliana, kupendana na kuvumiliana.
Mwisho ni maombi yangu kf idumu zaidi.
Nawaomba mniruhusu wanaume wenzangu ni mpongeze huyu kiumbe jimena a.k.a jike shupavu, mwanamke wa shoka, kwa kusimama kidete peke yake bila kukata tamaaa, najua dada zake ipo siku watarudi.
Nawapenda wote mliopo
Pia nawamiss waliotingwa na walio tuacha, nawakaribisha tena na tena tulisongeshe
AMEN...
 
Na miezi hiyo ni3 haikuwa rahisi kuna watu tuliwapokea wakiwa VIKAPUKU wana viLIKE vi3 lkn leo hii wamekuwa juu na kuota pembe na kuanza kujiona mastaa na kutaka wabembelezwe ili waendelee kuwepo au warudi tena....kwa taarifa yao HATUSHOBOKEI MTU na thread haiwezi kufa kwa wao kutoshiriki labda wataanza wao na wataumia kila siku wakiingia na kuona tunaendelea kupeta
Watakufa na wivu na cuki zaovzisizo na faida kwao wala kwetu
Idumu KF milele
.............................
Tudumu zaidi, In God We Trust.
 
afc9020bc66a5352129583022a225f6e.jpg
Mambo ya Jacuzi
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom