Makapuku Forum

Makapuku Forum

Unaendeleaje Seran ukimuona Obe nisaidie kumuuliza msimu wa korosho ni lini? Kama atakuwa anafahamu.
...mdau, msimu wa korosho tayari tangu Oktoba na sasa tunawasubiri watu wa AMCOS watupe mgao wetu wa pili, si unajua mambo ya stakabadhi ghalani.

Sasa nikisema nimeuza korosha, nimeng'oa mabati na kuezeka kwa nyasi, huwa sitanii.
 
Naendele powaa poker mzima weye??Aje atwambie tukamtembelee turudi na magunia ya korosho😅 Obe hebu njoo😁
Nimekuja mdau, nimeshamueleza patner shikizi wako kwamba nyie njooni tu, chumba nilichoweka magunia ya korosho, nimekisafisha, mtafikia humo, njoo na joto lako maana huku baridi, tumeng'oa viyoyozi maji tumeweka madirisha bila mapazia
 
Na uzuri amekwambia we mpe details hata za konda akutumie, hakika Obe ni mtu wa maana kabisa.
...konda asiwe mang'aa tu akapotea nazo kama mwaka ule namtumia Shunie korosho afu konda wa basi la Wifi Naye (wanapaki Sudan) akayeya nazo, nusu debe. Nilisikitika sana.

Au nikutumie wewe ili umfikishie na kifungashio cha ziada?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom