Ha hahahhaa, mtego huu kaka, Diblo alikuwa kama Gaucho, hujui anashambulia au anaunganisha timu, kama kiungo. Gitaa lake analicharaza kwenye sebene za kasi, zile ambazo mikatiko ya kutosha, utamuelewa zaid kwennye nyimbo za Aurlus Mabele kwenye band ya Loketo, au kwenye Empire Bakuba ya mkali Pepe Kalle akiitwa machine gun.
Dally Komoko yeye gitaa lake la solo, utampenda katika miziki ya taratibu, ile ambayo ushapiga Safari zako tatu za moto, umeagiza mishkaki na una mrembo anahakikisha wahudumu hawakuzidishii bill. Goma la Tobina utalielewa sana. Kwa hiyo hapo mimi ninaanguka na Dally Kimoko na ninasimama na Diblo Dibala.
Mdau lakini zama mpya usimsahau Alain Makaba ndani ya Wenge BCBG.
Ngoja nikomae na likizo ndugu yangu