Amemuua mama yake, ashtakiwe kama mtu mzima..!
Huyu mtoto anaitwa Noah Mann -Tate, kulia ni marehemu mama yake Noah, anaitwa Quiana Mann. Noah ndie aliyemuua mama yake.
Noah na mama yake walikuwa wanaishi huko Milwaukee, Marekani. Mwaka 2022,wakati Noah akiwa na umri wa miaka 10 alimwomba mama yake amnunulie miwani ya kuchezea game inaitwa VR headsets.
Mama yake alikataa kwamba kwa sababu Noah alikuwa amefanya vibaya darasani, yeye kama mama asingemnunulia kitu hicho anachotaka mpaka pale atakapobadilika. Jibu la mama halikumfurahisha Noah.
Noah aliiba bunduki ya mama yake akamvizia mama yake wakati anaweka nguo kwenye mashine ya kufulia. Noah akamfyatulia mama yake risasi tatu usoni. Mama yake akalia, "Mwanangu unaniua". Quiana akafariki.
Baada ya mama yake kufariki, Noah alichukua kadi ya benki ya mama na kuagiza gemu lake mtandaoni. Masaa machache baadae gemu lake lilifika.
Gemu lilipofika Noah alicheza gemu lake, huku mwili wa mama yake ukiwa umelala pembeni hauna uhai. Baadae Noah alikamatwa na polisi na kufikisha mahakamani.
Baada ya mvutano mkali, mahakama imeamuru kwamba Noah atashtakiwa kwenye mahakama za watu wazima kama mtu mzima.
Kwa sasa Noah ana umri wa miaka 12, iwapo atakutwa na hatia ya mauaji atafungwa kifungo cha miaka 60 jela...!
View attachment 3294596