Familia yote imekufa...ni baba, mama na watoto wao watatu... helikopta waliyokodi kutalii Jiji la New York imedondoka mtoni.
Hakuna aliyepona.
Bwana Agustín Escobar na mkewe Bi Mercè Camprubí Montal wote walikuwa wanafanya kazi kwenye kampuni ya Siemens. Walikuwa wanaishi Uhispania walikwenda Marekani kutalii.!
Kufikia mwezi Septemba tutajua Usonji unasababishwa na nini..!
Waziri wa Afya wa Marekani, Robert F. Kennedy Jr. ameahidi kwamba katika kipindi cha miezi 5 ijayo serikali itakuwa inajua ugonjwa wa Usonji unasababishwa na kitu gani.
Waziri huyo amesema kwamba serikali itafanya tafiti kujua sababu za ugonjwa huo. Hata hivyo taasisi inayoshugulika na ugonjwa wa Usonji nchini humo imedai kwamba matamshi ya Waziri huyo ni hatari na ya kupotosha kwa sababu ni muda mfupi sana kufanya utafiti wa kubaini sababu za Usonji.
Mpaka sasa bado wataalam hawajajua Ugonjwa wa Usonji unasababishwa na nini. Hata hivyo kuna uwezekano mkubwa kwamba sababu za kurithi na kimazingira zinaweza kuwa zinasababisha ugonjwa wa Usonji.
Matukio wa watoto wenye Usonji yameongezeka zaidi miaka ya karibuni. Huko nyuma Robert amewahi kudai kwamba Ugonjwa wa Usonji unasababishwa na chanjo, hata hivyo tafiti nyingi zimekanusha kwamba chanjo hazisabishi ugonjwa wa Usonji..!
Colossal Biosciences ni kampuni inayojishughulisha na kufufua viumbe vilivyotoweka, imefanikiwa kufufua mbwa mwitu wa zamani ‘Dire Wolf’ (wanafahamika zaidi kupitia uhusika wao kwenye series ya Game of Thrones).
Kwa kutumia teknolojia ya hali ya juu ya kuhariri DNA, kampuni hiyo imefanikiwa kufufua mbwa mwitu watatu waliopewa majina - Romulus, Remus, na Khaleesi.
Mbwa Mwitu hao wana mjumuisho wa sifa kutokea nyenzo za zamani za maumbile ya kijenitiki ambazo hazijakuwepo kwa zaidi ya miaka 12,500.
Pia kampuni hiyo imeweza kuzalisha ‘Red Wolves’ wawili wengine kimaabara. Red Wolves ni spishi nyingine ya mbwa mwitu ambayo ipo kwenye hatari kubwa ya kupotea kabisa Duniani.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.