Makapuku Forum

Makapuku Forum

Kiungo wa Simba, Luis Miquissone alieungana na wenzake kambini amekiri kwa sasa Simba ina kikosi kizuri na chenye ushindani na anaweza kusema wazi msimu ujao wapinzani watapata tabu sana.
.
“Lengo letu ni kuhakikisha msimu ujao tunamaliza tukiwa na mataji yote muhimu, na kufanya vyema Kimataifa. Hilo linawezekana tutapambana kuhakikisha tunatengeneza muunganiko mzuri ambao utakuwa na tija ndani ya timu.”
Screenshot_20230727_051901_Instagram.jpg
 
WAKATI mashabiki na wadau wa soka wakisubiri taarifa ya kuagwa kwa aliyekuwa mshambuliaji wa Yanga, Fiston Mayele mchezaji huyo amekubali ombi la kiungo wa Azam FC, Feisal Salum ‘Fei Toto’ kushangilia kwa kutetema endapo atafunga bao.
.
Maongezi hayo yamefanyika juzi jioni mastaa hao walitumia zaidi ya saa mbili walipokuwa wanazuingumza kwa njia ya Instagram live.
.
“Naomba niendelee kutetema, niruhusu kabisa sio nikifunga na kushangilia hivyo unanipigia simu na kuniambia kwa nini nafanya hivyo, nipe ruhusa kabisa ili mtetemo uendelee kuwepo; “Pia nakutakia kila la kheri wewe na familia yako kwenye majukumu yako ya kazi na maisha popote utakapokwenda nitakukumbuka daima,” alisema Fei Toto.
.
Mayele bila hiyana alimjibu kuwa hakuna shida kufanya hivyo, anaamini ataendelea kumuenzi kwa mazuri huku pia akikiri atakumbuka pasi zake za mwisho ‘asisti’. “Hapana wewe tetema tu, hamna shida lakini nimefurahi kuzungumza na wewe na nitakumbuka pasi zako pia nakutakia kila la kheri na naamini utakuwa bora zaidi ya vile tulivyokuwa tunacheza.”
Screenshot_20230727_052023_Instagram.jpg
 
Staa wa kwanza raia wa Afrika Kusini kucheza Ligi Kuu Tanzania, Mahlatse Makudebela ‘Skudu’, amesema anataka kuwaona Simba ili afahamu ubora wao.
.
“Nasubiri kuwaona Simba ili nijue wana ubora kiasi gani, lakini kwa ujumla lazima nikuhakikishie kuwa tuna timu bora. Ni kazi kubwa kupata namba hapa kwani wachezaji wengi wako vizuri na wanahitaji nafasi ya kucheza, hivyo mtihani mkubwa ni kuonyesha uwezo kwenye kila mchezo,” alisema staa huyo aliyejiunga na Yanga akitokea Marumo.
Screenshot_20230727_052133_Instagram.jpg
 
TETESI ni kuwa Winga wa Zamani wa Yanga, Simon Msuva ametaka klabu hiyo kumpa zaidi ya milioni 700 ( USD 300k) ili aweze kurejea kuitumikia tena klabu hiyo.

Msuva amekuwa akitumika nje ya Tanzania kwa mfanikio ambapo ameitumikia, Difaâ El Jadida, Wydad Casablanca zote za Morocco na Al Qadsiah Fc ya Saudi Arabia.

Taarifa zaidi zinaeleza kuwa Yanga hawapo tayari kutoa kitika hicho cha Fedha ili kupata saini ya winga huyo.
Screenshot_20230727_052253_Instagram.jpg
 
AL Hilal ya Saudi Arabia ipo hatua za mwisho kukamilisha uhamisho wa straika wa Fulham, Aleksandar Mitrovic, 28. Taarifa za awali zinaeleza wababe hao wameshafanya makubaliano binafsi na Mitrovic na kinachoendelea ni mazungumzo baina mabosi wa timu zote juu ya ada ya uhamisho.

Awali Fulham iliweka wazi kwamba haina mpango wa kumpiga bei fundi huyu lakini mchezaji amewaambia hataki tena kubaki kwenye timu hiyo
Screenshot_20230727_052353_Instagram.jpg
 
Inter Milan imewasilisha ofa ya Euro 15 milioni kwa Aston Villa ili kuipata huduma ya kipa wa timu hiyo, Emiliano Martinez mwenye umri wa miaka 30, katika dirisha hili. Inter Milan inataka kumsajili staa huyu ili akawe mbadala wa Andre Onana ambaye amejiunga na Manchester United, Martinez alionyesha kiwango bora kwenye michuano ya Kombe la Dunia mwaka jana kule Qatar akiwa na Argentina.
Screenshot_20230727_052448_Instagram.jpg
 
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwakushirikiana na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) imesema Serikali imefanya mabadiliko ya Sheria ya Serikali za Mitaa ya Utozaji wa Kodi ya Majengo, SURA 289 kupitia Sheria ya Fedha ya 2023 ambapo viwango vya utozaji kodi hiyo vimebadilika pamoja na wigo wa ukusanyaji kodi hiyo umeongezeka kwa kujumuisha nyumba zilizopo maeneo yote ya Wilaya.

Viwango hivyo vya utozaji Kodi ya Majengo vilivyobadilika na ambavyo vitaendelea kutozwa kupitia ununuzi wa umeme ni nyumba ya kawaida iliyokuwa inatozwa shilingi 12,000 kwa mwaka sasa itatozwa shilingi 18,000/ kwa mwaka sawa na shilingi 1,500 kwa mwezi.

Nyumba za ghorofa katika maeneo ya Majiji, Manispaa na Halmashauri za Miji zilizokuwa zinatozwa shilingi 60,000 kwa kila sakafu kwa mwaka sasa zitatozwa shilingi 90,000 kwa kila sakafu kwa mwaka sawa na shilingi 7,500 kwa mwezi.

Nyumba za ghorofa katika maeneo ya Halmashauri za Wilaya zilizokuwa zinatozwa shilingi 60,000 kwa kila nyumba kwa mwaka sasa zitatozwa shilingi 90,000 kwa kila nyumba kwa mwaka sawa na shilingi 7,500 kwa mwezi.

Utekelezaji wa kutoza kodi hii ya majengo kwa kufuata mabadiliko tajwa hapo juu, unaanza mwezi Julai, 2023. (taarifa zaidi zipo kwenye swipe)
Screenshot_20230727_052622_Instagram.jpg
 
Spika wa Bunge la Marekani Kevin McCarthy amesema huenda Wabunge wa Chama cha Republican wakatafakari hatua ya uchunguzi kumwondoa madarakani Rais wa Marekani Joe Biden kutokana na madai ya utovu wa nidhamu katika masuala ya fedha ambapo Chama chao kimewapa shinikizo la kumuunga mkono Donald Trump kabla ya uchaguzi wa Rais wa mwaka ujao nchini humo.

@dw_kiswahili inaripoti kuwa Wabunge wa Republican wapo chini ya shinikizo kubwa wakitakiwa na Chama chao kuonesha msimamo wa kumuunga mkono Donald Trump kabla ya uchaguzi wa Rais wa mwaka ujao nchini Marekani.

Spika Mccarthy amesema Bungeni kwamba mambo yanayotajwa na Wabunge wa Republican juu ya masuala ya fedha ya Familia ya Biden yanapaswa kuchunguzwa.

Hata hivyo Spika McCarthy amekiri kwamba mpaka sasa Bunge halijathibitisha kosa lolote lakini amesema uchunguzi unaliwezesha Bunge kupata taarifa na hivyo kubainisha ukweli.
Screenshot_20230727_052728_Instagram.jpg
 
Bunge la Ghana limepiga kura kufuta adhabu ya hukumu ya kifo na sasa inakuwa Nchi ya hivi karibuni kati ya Mataifa 29 ya Afrika ambayo yamefuta hukumu ya kifo.

@dw_kiswahili imeripoti kuwa kwa mujibu wa Ripoti ya Kamati ya Bunge, muswada huo mpya unalenga kurekebisha Sheria ya Makosa ya Jinai, ambapo nafasi ya adhabu ya kifo sasa itakuwa kifungo cha maisha jela lakini ili ianze kutekelezwa sheria hiyo lazima kwanza iidhinishwe na Rais wa Ghana, Nana Akufo-Addo.

Mbunge Francis-Xavier Sosu, aliyewasilisha muswada huo ameielezea hatua hiyo kama maendeleo makubwa ya rekodi ya Haki za Binadamu nchini Ghana.

Idara ya Magereza nchini Ghana imesema hakuna Mtu ambaye amenyongwa nchini humo tangu mwaka 1993 licha ya Watu 176 kuhukumiwa kifo hadi mwaka jana.
Screenshot_20230727_052920_Instagram.jpg
 
Tahadhari ya uwepo wa upepo mkali unaofikia kilomita 40 kwa saa na mawimbi makubwa yanayofikia mita mbili itakayodumu kwa siku tano kuanzia kesho Alhamisi, imetolewa na Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA), leo Julai 26, 2023.

Kupitia taarifa yake TMA, imetaja baadhi ya maeneo ya ukanda wa pwani ya bahari ya Hindi, mikoa ya Lindi, Mtwara, Tanga, Dar es Salaam na Pwani, ikijumuisha visiwa vya Mafia, Unguja na Pemba.

Pia tahadhari hiyo imetolewa kwa baadhi ya maeneo ya ukanda wa Ziwa Victoria (mikoa ya Kagera, Geita, Mwanza, Simiyu na Mara) pamoja na ukanda wa Ziwa Nyasa, mikoa ya Mbeya, Njombe na Ruvuma.

TMA imezitaja athari zinazoweza kujitokeza ambazo ni kuathirika kwa baadhi ya shughuli za uvuvi na usafirishaji baharini.
Screenshot_20230727_053121_Instagram.jpg
 
Katika hali isiyo ya kawaida, nyumba ya Seleman Mussa (65), Mkazi wa Kijiji cha Nkoma, wilayani Meatu, Mkoa wa Simiyu, iko hatiani kuuzwa kama fidia ya deni la Sh1.1 milioni, analodaiwa baada ya kutokamilisha kulipa mahari ya kijana wake.

Kijana wake huyo ambaye ni mwalimu wa shule moja ya sekondari mkoani Shinyanga, alimuoa binti wa Mwita Kati, toka mwaka 2019 kwa ndoa ya kimila, kwa makubaliano ya mahari ya ng'ombe 15.

Akizungumza na Mwananchi Digital, Mussa amekiri juu ya makubaliano hayo kwa kusema: “Tulikubaliana mahari ya ng'ombe 15 kwa thamani ya Sh150, 000 kila mmoja, baada ya maridhiano, walikuja nyumbani wakasema wanataka mahari yote, lakini tuliwaomba wachukue nusu na inayobaki tutailipa baadae," amesema Seleman.

Hata hivyo kwa mujibu wa Seleman, ilipofika mwaka 2020 baba mzazi wa binti alianza kudai mahari iliyosalia, ndipo alipoomba muda wa kuendelea kutafuta pesa ili kukamilisha deni hilo, na hapo ndipo ugomvi ulipoanzia.

Baada ya vikao kadhaa vya kifamilia na kiserikali kushindwa kufikia muafaka, mdai alilifikisha suala hilo mahakamani ambapo hukumu ilitolewa.

Katika shauri hilo la madai namba 81 la mwaka 2020, hukumu ilitolewa ilitaka kukamata nyumba ya Seleman namba 27B iliyopo kijiji cha Nkoma ili kufidia kiasi cha Sh1.21 kilichokuwa kimebaki.
Screenshot_20230727_053314_Instagram.jpg
 
Mahakama ya Hakimu Mkazi Mtwara, imemhukumu Shaibu Ally Mtepa (64), kifungo cha miaka 13 jela, baada kumtia hatiani kwa kosa la kujaribu kuua na kumjeruhi aliyekuwa mke wake Fadina Mussa, kwa kumkata viganja vya mikono nyumbani kwao Tandahimba mkoani Mtwara.

Kesi hiyo namba 11 ya mwaka 2023, imetolewa hukumu yake leo Julai 26 na Hakimu Mwandamizi Mwenye Mamlaka Ziada Frederick Lukuna.

Wakili upande wa utetezi Alex Msalenge amesema kuwa hayo ni maamuzi halali kwa kuwa mteja wake hakuisumbua mahakama.

“…hayo ni maamuzi halali kama mliivyosikia mteja anajutia kosa sio kwamba ameisumbua mahakama amekili kila kitu tupeni muda tuongee na mteja tutashaurina alafu tutajua hatua zinazofuata” amesema Msalenge

Kwa upande wake Fadina Mussa akilia mahakamani hapo alisema kuwa hajaridhishwa na hukumu hiyo angalau angefungwa miaka 20 ama 30 ingekuwa ni fundisho kwa watu wengine.

“Naomba Serikali inisaidie kwakuwa miaka 13 sio haki kwa mtalaka wangu ambaye ambaye aamenikata mikono yote miwili…naomba Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, pamoja na Rais wangu Samia Suluhu, wanisaidie,” amesema Fadina.
Screenshot_20230727_053424_Instagram.jpg
 
Baada ya mvutano wa siku kadhaa hatimaye leo Mahakama Kuu Mbeya imeanza kusikiliza hoja za upande wa madai katika kesi ya kupinga makubaliano ya ushirikiano wa Serikali ya Tanzania na Dubai katika uwekezaji Bandari za Tanzania zilizopo mwambao wa bahari na katika maziwa.

Wakati wa usikilizwaji huo leo Jumatano, Julai 26, 2023 mawakili hao wa upande wa madai, Mpale Mpoki, Boniface Mwabukusi, Philipo Mwakilima na Livino Galimitumba wamechambua ibara moja baada ya nyingine na kuonesha kile wanachodai masharti mabovu yasiyo na maslahi kwa Taifa na jinsi unavyokiuka Sheria na Katiba ya Nchi.

Mawakili hao katika hoja zao wamejaribu kuishawishi mahakama kuwa mkataba huo ni batili kwa kuwa na ibara zenye masharti yanayokiuka Sheria za Ulinzi wa Raslimali na Maliasili za Nchi, Katiba na kwamba unaondoa ukuu wa nchi na kuiweka chini ya Dubai na vile vile kuathiri Maliasili za Taifa na kuhatarisha Usalama wa Taifa.

Vilevile wamefafanua madai yao ya mchakato wa kuridhiwa na Bunge ulivyoikuka Sheria kwa kutowapa wananchi kwanza nafainya kutoa maoni yao kama kabla ya kuridhiwa kama Sheria zinavyoelekeza.
Screenshot_20230727_053644_Instagram.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom