Makapuku Forum

Makapuku Forum

Mwanaume Wilaya ya Kayunga nchini Uganda (jina linahifadhiwa), ametozwa faini ya Sh400,000 (sawa na Sh600, 000 za Uganda) kwa madai ya kufanya mapenzi na mpenzi wake kwenye mimbari ya kanisa.

Wakazi wa mji huo wameuambia mtandao wa Monitor kuwa wiki iliyopita, waliwapata wawili hao wakifanya kitendo hicho ndani ya jengo jipya la kanisa la Bugonya katika Kaunti Ndogo ya Kayonza nchini humo.

Tukio hilo lilitengeneza vichwa vya habari kwa ‘utatu’ wake usio wa kawaida kwani mwanamume Mkatoliki alikutwa akifanya mapenzi na mwanamke Mwislamu kwenye madhabahu ya Kanisa la Anglikana.

Wawili hao walipelekwa hadi kwa Afisa namba moja moja wa eneo hilo (LC1), ambapo waliachiliwa wakisubiri kusikilizwa kwa kesi yao, hata hivyo, mwanamume huyo mwenye umri wa miaka 23 ametoweka.

Inasemekana mwanaume huyo anajificha kwa rafiki yake katika kijiji hicho, huku mwanamke ambaye ni ametalakiwa, akiwa amechukuliwa na mama yake.
Screenshot_20230714_051844_Instagram.jpg
 
Athuman Yengayenga aliyefunga ndoa na wake watatu hivi karibuni mjini Mpanda ameingia matatani baada ya kushindwa kukamilisha kandarasi ya ujenzi wa vyumba vitatu vya madarasa shule ya msingi Mnyagala wilayani Tanganyika.

Yengayenga ni kati ya watu wawili waliochukua kandarasi ya ujenzi wa vyumba 6 vya madarasa na matundu 10 ya vyoo katika shule hiyo, ambapo yeye anajenga vyumba vitatu vya madarasa.

Akizungumza na Mwananchi katika ziara ya Katibu Tawala Mkoa wa Katavi Hassan Rugwa, wakati wa ukaguzi miradi ya BOOST wilayani Tanganyika, Yengayenga amesema alipata tenda hiyo kupitia jina la Majaliwa Lusambo.

"Maandalizi ya harusi yangu yamesababisha mradi kutokamilika kwa wakati, niliweka mtu wa kusimamia lakini vifaa vilichelewa kufika site, msimamizi badala ya kutoa taarifa kwa maandishi yeye alitoa kwa mdomo,” amesema na kuongeza;

"Mimi hakunishirikisha, kitu ambacho kilisababisha pia wahusika kutotilia manani, najenga vyumba vitatu na kila kimoja kinagharimu Sh2.4 milioni, nimelipwa nusu yake na zimenisaidia kwenye harusi," amesema.

Screenshot_20230714_051942_Instagram.jpg
 
Waziri wa Mambo ya Ndani nchini Kenya Prof Kithure Kindiki amesema wote walioshiriki katika uharibifu mkubwa wa mali wakati wa maandamano yaliyofanyika Nairobi na maeneo tofauti ya nchini Kenya watakakutana na mkono wa sheria.

Kwa mujibu wa mtandao wa Nation, taarifa ya Prof Kindiki imemtaja Kiongozi wa Azimio, Raila Odinga na kundi la wanasiasa wanaomuunga mkono, akisema wanahusika na kuenea kwa ghasia, uporaji na uharibifu wa mali ulioshuhudiwa katika maeneo mbalimbali ya nchi.

Waziri Kindiki amesema vyombo mbalimbali vya uchunguzi vinafanya kazi usiku na mchana kuwakamata na kuwafungulia mashtaka wale wote waliotekeleza uhalifu wakati wa maandamano hayo, ambayo yalisababisha watu wengi kujeruhiwa na mali za mamilioni ya pesa kuharibiwa.

"Utamaduni wa kutojali utakoma. Wale wote walioshiriki moja kwa moja au kwa njia isiyo ya moja kwa moja katika ukiukwaji uliopangwa leo (jana) wa usalama wa umma na usalama wa taifa letu wataadhibiwa,” aliongeza Kindiki.

Waziri huyo amedai kuwa Raila amekuwa chanzo cha msukosuko wa kisiasa nchini humo huku akitaja visa kama vile jaribio la mapinduzi ya 1982 na machafuko ambayo yaliikumba Kenya baada ya uchaguzi wa 2017.

Screenshot_20230714_052214_Instagram.jpg
 
Kiongozi wa Umoja wa Azimio nchini Kenya, Raila Odinga amesema kuwa wanajipanga kwa awamu ya tatu ya maandamano ya kupinga kupanda kwa gharama za maisha nchini humo dhidi ya Serikali.

Odinga ameyasema hayo jana Jumatano, Julai 12, 2023 muda mchache baada ya kusitisha mkutano wake wa hadhara uliopangwa kufanyika katika uwanja wa Kamukunji.

"Tutamlazimisha Ruto (Rais wa Kenya) kuwapa Wakenya mpango mzuri. Hivi karibuni tutawasiliana jinsi awamu ya tatu ya maandamano itakavyokuwa,” amesema.

Screenshot_20230714_052352_Instagram.jpg
 
Polisi mjini Kampala jana wamesema silaha za jeshi zimekuwa zikitumika kufanya uhalifu karibu na jiji hilo na kusababisha vifo vya watu wengi katika wiki za hivi karibuni.

Katika moja ya matukio ya hivi karibuni ya unyang’anyi wa kutumia silaha Juni 30 mwaka huu, askari mmoja kutoka kambi ya Jeshi ya Kikubamutwe iliyopo barabara ya Kayunga wilayani Mukono, alivamia duka la kubadilisha fedha katika eneo la Luzira, jijini Kampala na kuiba fedha za Uganda Sh72 milioni.

Msemaji wa polisi wa Kampala, SP Patrick Onyango, ameiambia mtandao wa Monitor kwamba maafisa wa eneo la uhalifu wamefanikiwa kupata bunduki aina ya AK47 ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Uganda (UPDF) baada ya tukio hilo la Luzira.

Polisi wanasema askari huyo mhalifu ndiye chanzo cha bunduki zilizotumika katika matukio ya wizi ya hivi karibuni katika Wilaya ya Mukono.

Inasemekana mtuhumiwa huyo alipangiwa kazi ambayo ilimpa nafasi ya kuingia kwenye ghala la silaha katika kambi ya Kikubamutwe ambako alitoa silaha kwa ajili ya kuzikodi kinyume cha sheria.
Screenshot_20230714_052456_Instagram.jpg
 
Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya Simba SC Ahmed Ally ametolea ufafanuzi taarifa za Mkali wa soka Clatous Chama Raia wa Zambia kudaiwa kuwa amegoma kwenda Uturuki Pre Season na Club hiyo kwasababu anadai stahiki zake.

Kupitia fununu hizo wengine walidai @realclatouschama ana ofa mkononi na anataka kuondoka Simba SC lakini Ahmed Ally ameweka wazi kuwa Club hiyo haina ofa yoyote iliyopokea.

“Kumekua na sintofahamu kuhusu mkataba wa Mwamba wa Lusaka kiasi cha kuzua taharuki miongoni mwa Mashabiki wetu, taarifa ni kwamba Chama bado ana mkataba na Simba kwa muda wa mwaka mmoja hadi mwaka 2024 hatujapokea ofa kutoka klabu yeyote ikihitaji kumnunua Chama na wala hatujapokea maombi ya Mchezaji kutaka kuvunja mkataba”

“Mchezaji yeyote ambaye tunamuhitaji atabaki kuitumikia Simba kulingana na mahitaji ya mkataba wetu” ——
Screenshot_20230714_052738_Instagram.jpg
 
Shirikisho la Soka Afrika (CAF), limetoa Makundi ya kuwania kufuzu Fainali za Kombe la Dunia mwaka 2026 zitakazofanyika Canada, Mexico na USA.

Makundi yamepangwa tisa na kila kinara wa Kundi atakuwa amefuzu moja kwa moja kucheza Fainali hizo, Tanzania amepangwa Kundi E lenye Timu za Morocco, Congo, Niger, Eritrea na Zambia.
Screenshot_20230714_052842_Instagram.jpg
 
Mwanamke mmoja aitwaye Janath Swedi (72) Mkazi wa Mtaa wa Mtakumbuka, Kata ya Momoka Manispaa ya Sumbawanga Mkoani Rukwa ameuawa kwa kushambuliwa na kundi kubwa la nyuki nyumbani kwake.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Mwenyekiti wa Mtaa huo Mohamed Makubi amesema tukio hilo la lilitokea mtaani kwake July 10, 2023 na jitihada za kumuokoa Mwanamke huyo zilifanyika akapelekwa Hospitali lakini ilipofika saa nane usiku wa kuamkia July 12 akafariki.
Screenshot_20230714_052948_Instagram.jpg
 
Simba SC wametangaza rasmi kumsajili Kiungo Fabrice Ngoma (29) Raia wa Congo DR kama Mchezaji wao mpya kwa mkataba wa miaka miwili akitokea Al Hilal ya Sudan.
Screenshot_20230714_134032_Instagram.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom