Makapuku Forum

Makapuku Forum

Screenshot_20230712_064210_Opera%20Mini.jpg
 
Yanga imetangaza rasmi viingilio vya Tamasha lake la Wiki ya Wananchi ambalo hufanyika kila mwaka ambapo mwaka huu litafanyika July 22 katika uwanja wa Benjamin Mkapa Dar es Salaam na kukipiga na Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini.

VVIP: Tsh 500,000/=
VIP A: Tsh 100,000/=
VIP B: Tsh 40,000/=
VIP C 1: Tsh 30,000/=
VIP C: 20,000/=
Mzunguuko: Tsh 10,000/=
Screenshot_20230713_145702_Instagram.jpg
 
OFFICIAL & CONFIRMED:
.
Klabu ya Yanga imethibitisha kukamilisha usajili wa winga kiberenge MAXI MPIA NZENGELI ( @maxi_mpia_nzengeli ) kutoka AS Maniema kwa Mkataba wa miaka miwili.
.
Nzengeli (23) anahesabika kuwa winga bora wa kulia pia na ubora wa kucheza kama kiungo mshambuliaji na kupiga pasi za mabao.
.
WANANCHI hapo vipi ..!!
Screenshot_20230714_045029_Instagram.jpg
 
Kiungo fundi wa zamani wa kimataifa wa Nigeria aliyewika katika klabu za PSG na Bolton, Augustine ‘Jay Jay’ Okocha (46) ameteuliwa kuwa Waziri wa Michezo, Vijana na Maendeleo nchini Nigeria.

Uteuzi huo umefanywa na Rais mpya wa Nigeria, Bola Tinubu.
Screenshot_20230714_050344_Instagram.jpg
 
.
CONFIRMED: Uongozi wa Yanga umefikia makubaliano ya kumtoa kwa mkopo beki wa kushoto David Bryson kwenda klabu ya JKT Tanzania hadi mwisho wa msimu wa 2023/24.

Bryson amebakiza mkataba wa mwaka mmoja ndani ya Yanga SC.
Screenshot_20230714_050458_Instagram.jpg
 
BEKI mkongwe wa pembeni nchini, Juma Abdul wa Singida Fountain Gate yupo mbioni kutua Namungo kwa mkopo baada ya kukosa namba ndani ya kikosi hicho msimu uliopita.
.
Abdul, aliyewahi kuwika na Mtibwa Sugar, Yanga na Taifa Stars ni miongoni mwa mabeki wazawa wenye uwezo mkubwa uwanjani, lakini hakuwa na msimu mzuri ndani ya Singida hivyo ataungana na wenzake wengine wenye mikataba kutolewa kwa mkopo katika timu nyingine.
Screenshot_20230714_050601_Instagram.jpg
 
Kama Kocha Miguel Gamondi ataridhia wiki hii mazoezini kama Djuma Shaban apigwe chini au la, kama itakuwa hivyo, viongozi watashusha chuma kingine beki wa kulia pale Asec Mimosas ya Ivory Coast Kouassi Yao Attohoula.
.
Yao ambaye pia anacheza kama winga, mabosi wa Yanga wanapiga hesabu ni mtu mwafaka wa kuongeza kasi upande wa kulia kwani hata kwenye ripoti ya Kocha Nabi alishawaambia kwamba wamchomoe Djuma walete mtu wa kazi.
.
Faili la Djuma pale Yanga halisomeki vizuri ikipiga hesabu za kumng’oa kwa kuangalia takwimu zake lakini pia anatajwa kuhusu nidhamu yake haiwaridhishi mabosi wake lakini uamuzi wa mwisho ameachiwa Kocha Miguel Gamondi.
Screenshot_20230714_050701_Instagram.jpg
 
ZANDANI: Viongozi wa Simba wameamua kupiga ‘stop’ kwa muda usajili wa golikipa Mbrazil Caique Luiz Santos baada ya kugundua kipa huyo anazungumza Kireno kwa sana lugha inaweza isiwe nzuri katika mawasiliano baina yake na mabeki wa Simba, jambo ambalo linaweza kuigharimu timu.
.
Beki Henock Inonga na Che Malone wanazungumza Kifaransa hivyo itakuwa vigumu kwa Caique kuwasiliana nao kwani hajui Kifaransa na Kiingereza chake ni cha kuunga unga.
.
Hata hivyo, huo sio mwisho wa Simba na Caique kwani wamesimamisha usajili huo kwa muda na kuingia sokoni tena kutafuta kipa ambaye atakuwa walau anaweza kuzungumza Kifaransa au Kiingereza na baadhi ya rada za Simba zimenasa Cameroon.
Screenshot_20230714_050806_Instagram.jpg
 
EVERTON inatarajia kuanza mazungumzo na wakala wa mshambuliaji wa Manchester United na Sweden Anthony Elanga ili kuipata saini yake katika dirisha hili.
.
Elanga ambaye hapati nafasi ya kutosha kwenye kikosi cha kwanza cha Man United hata yeye amekuwa akitamani kuondoka. Ikiwa watashindwa kulipa ada yake ya uhamisho Everton imepanga kumchukua staa huyu kwa mkopo.
Screenshot_20230714_050913_Instagram.jpg
 
Aaron Ramsey ameanza mazungumzo na Cardiff City juu ya uwezekano wa kujiunga na timu hiyo katika dirisha hili la usajili wa majira ya joto huko Ulaya baada ya kuachwa na Nice ya Ufaransa.

Cardiff ambayo ni timu ya utotoni ya supastaa huyu wa zamani wa Arsenal mwenye umri wa miaka 32, inaonekana kuwa na uhitaji wa kumsajili licha ya kufahamu kuwa amekuwa akisumbuliwa na majeraha ya mara kwa mara.
Screenshot_20230714_051033_Instagram.jpg
 
Jumla ya miili 12 imepatikana leo Alhamisi Julai 13, katika msitu wa Shakahola uliopo Kaunti ya Kilifi wenye ekari eneo 800 na kufanya idadi rasmi ya waliofariki kufikia 384.

Polisi wamekuwa wakifukua eneo la makaburi ya pamoja ambapo wafuasi wa muhubiri tata Paul Mackenzie walizikwa baada ya kudaiwa kushawishiwa kujiua kwa njaa na mchungaji huyo mwenye msimamo mkali.

Mkuu wa Mkoa wa Pwani Rhoda Onyancha amethibitisha kuwa hakuna mtu mpya aliyekamatwa kuhusiana na vifo hivyo, na kwamba idadi ya waliokamatwa bado ni ile ile ya 37.

Awali Shirika la Msalaba Mwekundu la nchini humo lilisema watu waliotoweka wakihusishwa na mahubiri ya Mackenzie ni zaidi ya 600.
Wakati huohuo, idadi ya waliookolewa wakiwa hai imefikia 95 huku sampuli za DNA 253 zimekusanywa na wapelelezi.

Taarifa zinasema ufukuaji wa makaburi hayo utaendelea.

Screenshot_20230714_051151_Instagram.jpg
 
Hofu imetanda baada ya watu wawili Faraji Ismail Rahisi (30) na mwingine ni mtoto wa miaka sita, kujeruhiwa na tembo ambaye alikuwa nje ya nyumba yao katika Wilaya ya Tandahimba.

Akizungumzia na Mwananchi Digital kwa njia ya simu, Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Kanal Patrick Sawalla amesema: “Kwakweli tembo hawajawahi kusikika katika wilaya yetu, yaani hata sisi tunashangaa; tunasubiri taarifa ya Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyapori Tanzania (Tawa) ili tuweze kujua wametokea wapi,” amesema na kuongeza;

“Lakini pia tumetoa rai kwa wananchi maana tumeambiwa na watalaamu kuwa tembo hawataki kelele hivyo tumewasihi wakae majumbani wasipige kelele wala wasiwarushie mawe. Pia mashirika mbalimbali yapo huko yanatoa elimu ili wananchi wanachukue tahadhari.”

Naye Diwani wa Kata ya Chingungwe Juma Hamisi Mdiliko amesema kuwa katika eneo lake, ni mtu mmoja aliyejuruhiwa ambaye anajulikana kwa jina la Faraji Ismail Rahisi (30) ambapo alikuwa shambani akiendelea na majukumu yake.

Screenshot_20230714_051254_Instagram.jpg
 
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imewataka wakazi wa mikoa ya Dar es Salaam, Lindi, Mtwara, Tanga, Pwani pamoja na wale wa Visiwa vya Pemba na Unguja kuchukua tahadhari na kujikinga na upepo mkali kwa siku tano mfululizo kuanzia leo.

Ushauri huo wa tahadhari umetolewa na leo Alhamisi ya Julai 13, 2023, huku ikitabiri kutokea upepo mkali usiozidi kilomita 40 kwa saa na mawimbi makubwa yasiyozidi mita mbili kwa baadhi ya maeneo ya ukanda wa bahari ya Hindi.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, TMA imetoa angalizo kwa mikoa mengine miwili ya Katavi na Rukwa kufuatia upepo mkali unaofikia kilomita 40 kwa saa kwa baadhi ya maeneo ya kusini mwa ukanda wa Ziwa Tanganyika.

“Athari zinazoweza kujitokeza ni pamoja na kuahirishwa kwa shughuli za baharini pamoja shughuli nyingine za bandari. Shughuli hizi ni pamoja na zile za uvuvi pamoja na usafirishaji baharini,” taarifa hiyo ya TMA imeeleza.

Tahadhari hiyo inafanana na ile iliyotolewa na mamlaka hiyo Jumapili Juni 25, mwaka huu, ambapo utabiri ulionyesha kuwa mikoa tajwa ingeathiriwa na uwepo wa upepo mkali na mawimbi makubwa katika pwani ya bahari ya Hindi.
Screenshot_20230714_051414_Instagram.jpg
 
Baada ya Shirikisho la Soka Barani Afrika(CAF) kubadilisha jina la mashindano yake mapya Super League na kuitwa African Football League

Rais wa CAF Patrice Motsepe amesema mashindano hayo yataanza Octoba 20, 2023 na mchezo wa ufunguzi utachezwa Tanzania.

Timu nane pekee zitashiriki mashindano hayo zikiwemo timu zilizofuzu kwa nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika 2023 Ahly ya Misri, Wydad Casablanca ya Morocco, Esperance ya Tunisia, na Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini.

Nyingine zitakazoshiriki ni TP Mazembe ya DR Congo, Enyimba ya Nigeria, Simba ya Tanzania na Petro Atletico ya Angola.

Screenshot_20230714_051530_Instagram.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom