Makapuku Forum

Makapuku Forum

Kituo hicho cha kisasa cha biashara Afrika Mashariki, kinajengwa wilayani Ubungo, jijini Dar es Salaam sehemu ambayo awali kulikuwa na Kituo Kikuu cha Mabasi yaendayo mikoani.

Mkurugenzi Mkuu wa kituo hicho Cathy Wang, amesema kuwa kituo hicho kinatarajiwa kufunguliwa mwezi wa sita mwakani baada ya ujenzi wake kukamilika.

Cathy ameyabainisha hayo leo Julai 8, 2023; kwenye maonesho ya 47 ya biashara ya kimataifa (Sabasaba) yanayofanyika katika viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Screenshot_20230709_054452_Instagram.jpg
 
Mkurugenzi wa Kinga wa Taasisi ya Saratani Ocean Road (ORCI) Dk Crisprin Kahesa amesema, Watanzania wengi wanaogopa na hawapo tayari kupokea majibu ya vipimo vya saratani, jambo ambalo ni hatari kwa taifa.

Changamoto hiyo inakuja wakati ambapo takwimu za taasisi hiyo zinaonyesha, asilimia 75 ya wanawake wanaofika ORCI kwa ajili ya uchunguzi wa saratani ya matiti na mlango wa kizazi, wanakutwa na ugonjwa huo katika hatua za mwisho.

Kufuatia hali hiyo, ORCI imetangaza huduma za uchunguzi wa saratani bure katika maonyesho ya Kimataifa ya 47 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam (DITF).
Screenshot_20230709_054544_Instagram.jpg
 
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dk Angeline Mabula, ametaka wananchi wa Wilaya ya Longido mkoani Arusha kutumia fursa ya mradi wa uboreshaji usalama wa milki za ardhi nchini, kutatua migogoro ya ardhi iliyodumu kwa muda mrefu katika halmashauri hiyo.

Waziri Mabula ametoa kauli hiyo tarehe 8 Julai 2023 wilayani Longido mkoa wa Arusha wakati akifungua mkutano wa wadau kujadili mpango wa matumzi ya ardhi wilaya hiyo uliobeba kauli mbiu ya uboreshaji milki kwa maendeleo endelevu.

Amesema, halmashauri ya Wilaya ya Longido inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo muingiliano wa aina za ardhi.

Screenshot_20230709_054723_Instagram.jpg
 
Watu nane wamefariki dunia wakiwemo watoto wawili, wenye umri wa miaka mitano na nane, kufuatia kuanguka kwa jengo moja katika mji wa Recife Kaskazini Mashariki mwa Brazil jana Ijumaa.

Sababu za kuanguka kwa jengo hilo bado hazijafahamika lakini mji huo ulikumbwa na mvua kubwa katika siku za hivi karibuni.

Maafisa wa Serikali wamesema jengo hilo liliporomoka majira ya saa 06:35 usiku kwa saa za Brazil wakati wakazi wengi wakiwa wamelala.
Screenshot_20230709_055005_Instagram.jpg
 
Iran imewanyonga wanaume wawili mapema leo kufuatia shambulio dhidi ya Washia na kusababisha vifo vya takribani watu 13 mwezi Oktoba mwaka jana, vyombo vya habari vya Serikali ya Iran vimeripoti.

Shirika rasmi la habari la IRNA limesema wawili hao walinyongwa alfajiri katika mji wa kusini wa Shira.

Wakati wa kesi yao wanaume hao walisema kwamba walikuwa wakiwasiliana na kundi la Islamic State la nchini Afghanistan na kusaidia kupanga shambulio la madhabahu ya Shah Cheragh huko Shiraz.
Screenshot_20230709_055058_Instagram.jpg
 
Serikali iko mbioni kuanzisha mnada wa kitaifa na kimataifa kwa ajili ya madini ya Tanzanite, ikiwa na lengo la kuyaongezea thamani.

Hayo yamebainishwa leo na Waziri wa Madini, Dotto Biteko baada ya kufanya ziara ya siku moja Mji Mdogo wa Mirerani ambako madini hayo huchimbwa.

Amesema mnada wa kwanza utaanza katika mji huo mara tu jengo la soko la madini hayo kukamilika.

Screenshot_20230709_055516_Instagram.jpg
 
Askari wa kikosi cha Jeshi la Zimamoto na uokoaji mkoani Kagera wamefanikiwa kudhibiti moto usiendelee kuteketeza majengo mengine katika shule ya sekondari ya Istiqama Manispaa ya Bukoba.

Moto huo umetokea jana Ijumaa Julai 7, 2023 saa 12 kamili jioni. Kamanda wa Jeshi la Zima Moto na Uokoaji mkoani hapa, Zabron Muhumha amesema baada ya jeshi hilo kupata taarifa askari wa jeshi hilo waliwahi eneo la tukio kwa ajili ya kuudhibiti.

"Baada ya kupata taarifa ya moto huo askari wangu wamewahi eneo la tukio wakiwa na gari letu na baadae wameongeza nguvu kwa kutumia gari la uwanja wa ndege na kufanikiwa kuudhibiti moto huo ili usiendelee kusambaa na kuleta madhara zaidi" amesema Muhumha

Kwa upande wake Mkurugenzi wa shule hiyo Farid Said amesema, bweni lililoungua lilikuwa la wavulana, huku mpaka Sasa hakuna madhara yoyote kwa binadamu (majeruhi) yaliyosababishwa na moto huo.
Screenshot_20230709_060430_Instagram.jpg
 
Simba SC imetangaza kukamilisha usajili wa mlinzi wa kati Che Fondoh Malone raia wa Cameroon (24) aliyekuwa akicheza Coton Sport FC de Goroua .

Che Malone anamudu kucheza nafasi mbili uwanjani , beki wa kati au beki wa kulia amekuwa tegemezi kwenye Kikosi cha Cotom Sports hata timu ya taifa ya Cameroon ameitwa mara kadhaa.

Vipi hali ya bahari huko ..!
Screenshot_20230709_131528_Instagram.jpg
 
Simba SC imetangaza kukamilisha usajili wa mlinzi wa kati Che Fondoh Malone raia wa Cameroon (24) aliyekuwa akicheza Coton Sport FC de Goroua .

Che Malone anamudu kucheza nafasi mbili uwanjani , beki wa kati au beki wa kulia amekuwa tegemezi kwenye Kikosi cha Cotom Sports hata timu ya taifa ya Cameroon ameitwa mara kadhaa.

Vipi hali ya bahari huko ..! View attachment 2682853

Anakaba mpka umbeya huyu beki
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom