Makapuku Forum

Makapuku Forum

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni amesema Serikali imetenga Tsh. trilioni 1.2 katika bajeti yake ya mwaka 2023/2024 huku kukiwa na ongezeko ukilinganisha na bajeti ya mwaka 2022/2023 lengo likiwa ni kudhibiti matukio ya uhalifu kwa kuboresha vitendea kazi ikiwemo pikipiki maalumu za kuongoza misafara ya Viongozi.

Masauni amesema hayo leo Jijini Dar es salaam baada ya kushuhudia makabidhiano ya pikipiki maalumu ya kuongoza misafara ya Viongozi iliyotolewa na Mdau wa maendeleo, Mohammed Ibrahim ambaye amesema hiyo ni pikipiki ya tatu kuikabidhi kwa Polisi na anao mpango wa kuwakabidhi magari pia Polisi ili kusaidia jukumu la ulinzi wa mali na Wananchi.

Waziri Masauni pia amesema Serikali ina mpango wa kujenga wa Vituo vya Polisi katika Kata na Shehia zote nchini huku akitoa wito kwa Wadau kujitokeza kuiunga mkono Serikali katika adhma yake ya kuhakikisha huduma za ulinzi wa mali na Wananchi inafika katika ngazi zote ili kuweza kudhibiti Wahalifu na matukio mbalimbali ya uhalifu.

Kwa upande wake Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Muliro Jumanne ameishukuru Wizara kwa kuwaunganisha na Wadau na ameahidi msaada huo kutumika katika dhamira iliyokusudiwa.
Screenshot_20230609_074311.jpg
 
Mbunge wa zamani wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ ameitaka Serikali iangalie namna ya kubana matumizi katika ununuzi wa magari ya Viongozi na kupendekeza Mawaziri watumie Toyota Hilux 'pick up’ na sio V8.

Sugu ameyasema haya katika mkutano wa hadhara wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) uliofanyika katika Mji wa Mlowo Wilayani Mbozi mkoani Songwe.

"Hakuna sababu ya Viongozi kutumia magari ya gharama kubwa ya zaidi ya Milioni 400 wakati wanaweza kufanya kazi katika magari ya kawaida, wanunue magari kulingana na mazingira, mfano Waziri wa Kilimo piga pickup, Waziri wa Ujenzi pickup, Waziri wa Kilimo unaenda kukagua mashamba V8 la nini?”

Kwa upande mwingine aliyekuwa Mbunge wa Mbozi (CHADEMA), Paschal Haonga ameitaka Serikali iruhusu soko huria la mazao ili Wananchi waweze kuwa na uhuru wa kuuza mazao yao badala ya kutegemea kuuza AMCOS.

“Sisi sera yetu ni soko huria, kuwa na kampuni nyingi za kununua mazao ili kuwe na ushindani wa bei hali hiyo itawapa Wananchi uhuru wa kuchagua wauze wapi mazao yao" —— Haonga.

Mkutano huo ambao umehudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa CHADEMA wa Wilaya, Mkoa na Kanda ulihamasisha pia Wananchi kudai katiba mpya na Tume huru ya uchaguzi.
Screenshot_20230609_074445.jpg
 
Wakati wengine wakisema utakula kwa urefu wa kamba yako, wengine wanasema utateseka kulingana na maamuzi ya chaguo lako, wakati wengine wakisema 'cheap is expensive' kwamba 'cha nafuu ni ghali" wengine wanasema kinga ni bora kuliko tiba... misemo yote hii inafanya kazi kwenye kesi nyingi sana hata pale unapojikuta gereji na Toyota yako.

Kwa sisi wenye magari ya Toyota ukikutana na Fundi Mwaminifu gereji anaweza kukupa machaguo matatu ya spea ambapo ya kwanza ni ya Mchina ambayo ni bei rahisi kuliko mwingine lakini haitodumu na utarudi gereji soon tu, vilevile atakwambia kuna iliyotumika 'used' ambayo mara nyingi hutolewa kwenye gari jingine ambayo bei yake ni ya kati alafu kama hautaki maumivu ya kichwa na akili kuna mpya ORIGINAL zile zinazouzwa kwenye maduka ya Toyota Tanzania hivyo chaguo mwenyewe.

Pamoja na hayo yote pia wengi wetu hatuna uwezo wa kutofautisha kwa macho ni ipi spea feki na ipi original na wakati mwingine tunajikuta tumeuziwa feki kwa bei ya original na baada ya muda mfupi tunajikuta tena gereji tukitibu ugonjwa zaidi ya mmoja kwasababu wanasema spea mbovu inaweza kukusababishia ugonjwa mwingine kwenye gari.

Sasa wakati Kampuni ya Toyota Tanzania (1965) inatimiza miaka 58 Nchini Tanzania tangu ianze kuuza magari na spea 'original' za Toyota aina zote zikiwa zimehakikiwa na Mainjinia wa Toyota na kuwekewa waranti, imewakumbusha Watanzania kuzingatia ubora wa vipuri kwanza kabla ya kingine na kuwakaribisha kutembelea Maduka yao katika Mikoa mbalimbali Tanzania, jiunge nao kwenye @Toyota.Tanzania

Kabla hujamalizana na hii post chek slide uone feki na original zilivyofanana..... alafu baada ya hapo niambie experience yako ya kutumia spea feki, je imeshawahi kukutokea ? matokeo yalikuaje ? nini ungependa Watanzania wengine wafahamu na waepuke kufanya ?
Screenshot_20230609_074656.jpg
 
Kampuni maarufu ya usafirishaji Abiria ya Abood Bus Service imetangaza kuanza kutumia Mabasi yake mapya ya VIP kwenye safari zake za Dar - Mwanza kuanzia kesho June 9 2023.

Taarifa rasmi kutoka kwenye Kampuni hiyo imesema ni furaha yake kuendelea kutoa huduma bora kwenye usafirishaji abiria Nchini Tanzania kwa miaka 37 sasa ambapo Mabasi haya ukiachia mbali kuwa na siti nzuri za 'luxury', yana AC, TV, Wifi, choo, Wahudumu waliobobea, vinywaji pamoja na vitafunwa.

"Tunazindua ruti hii baada ya kupata maombi mengi ya Wateja wetu na tunawakaribisha Wasafiri wote wafenye booking kupitia namba yetu ya huduma kwa Wateja 0748771551 lakini pia wanaweza kufanya booking kupitia tovuti yetu ya www.aboodbus.co.tz au wakapakua APP yetu ya Abood Bus kupitia playstore au APP STORE" - imeeleza taarifa hiyo.

Abood Bus Service Limited @aboodbustz ilianza kazi ya usafirishaji wa Abiria Nchini Tanzania mwaka 1986 hadi sasa inasafirisha Abiria kutoka Dar kwenda Mikoa 11 ya Tanzania.
Screenshot_20230609_075324.jpg
 
Chama cha Mawakili Tanzania (TLS) kimesema inatambua uwepo wa mijadala inayoendelea nchini kuhusu makubaliano kati ya Serikali ya Tanzania na Serikali ya Dubai kuhusu uendeshaji wa Bandari ya Tanzania na kampuni ya DP World ya Falme ya Dubai.

TLS imesema Kutokana na unyeti wa suala hili Baraza la Uongozi la TLS likiongozwa na Rais, Wakili Harold Sungusia limeunda kamati ya Wataalamu kuchambua makubaliano hayo.

Baraza hili litaongozwa na Makamu wa Raisi wa TLS, Wakili Aisha Sinda, likiwa na Wajumbe Dkt Hawa Sinare (Makamu Mwenyekiti), Wakili Mpale Mpoki (Mjumbe), Wakili Stephen Mwakibolwa (Mjumbe), Wakili Mackphason Mshana (Katibu).

Kamati itatoa ripoti yake na mapendekezo yake kwa Baraza la Uongozi tarehe 12/06/2023 ili TLS iweze kutoa maoni na kwa hatua zaidi.
Screenshot_20230609_075528.jpg
 
Wakati Club ya Yanga SC ikitangaza kupokea ofa ya Azam FC na kuthibitisha kumuuza Mchezaji huyo baada ya makubaliano ya pande zote mbili, Feisal tayari amesaini mkataba na Azam FC.

Feisal ameonekana akisaini mkataba wake mpya mbele ya Viongozi wa Club hiyo katika tukio ambalo limerushwa LIVE kupitia AzamTV.
Screenshot_20230609_075631.jpg
 
Baada ya mvutano wa kimakataba wa muda mrefu kati ya Yanga SC na Mchezaji Feisal Salum hatimaye leo suala hilo limefikia tamati baada ya Yanga kumuuza Mchezaji huyo kwa Azam FC.

Taarifa rasmi ya Yanga SC imesema wamepokea ofa kutoka Azam FC na kuamua kumuuza Mchezaji huyo baada ya makubaliano ya pande zote mbili.

Feisal anaenda Azam FC kwa ada ya uhamisho ambayo hata hivyo bado haijatajwa ambapo amekuwa nje ya uwanja takribani kwa miezi sita… toka 24/12/2022 alipoandika barua ya kuomba kuvunja mkataba na Yanga.
Screenshot_20230609_075753.jpg
 
Mfanyabiashara maarufu wa Zanzibar na Mwanasiasa ambaye aliwahi kuwa Mwakilishi Jimbo la Uzini Mkoa wa Kusini Unguja, Mohamed Raza amefariki dunia leo wakati alipokuwa akipatiwa matibabu Hospitalini Jijini Dar es Salaam.

Taarifa za msiba huo zimethibitishwa na mmoja wa Wanafamilia aitwae Mohammed Ibrahim Raza ambapo maziko yatafanyika leo Kisutu Dar es salaam.

Itakumbukwa May 09,2023 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali alimtembelea Mohamed Raza baada ya kulazwa Hospitalini Jijini Dar es salaam.
Screenshot_20230609_075934.jpg
 
Mfanyabiashara maarufu wa Zanzibar na Mwanasiasa ambaye aliwahi kuwa Mwakilishi Jimbo la Uzini Mkoa wa Kusini Unguja, Mohamed Raza amefariki dunia leo wakati alipokuwa akipatiwa matibabu Hospitalini Jijini Dar es Salaam.

Taarifa za msiba huo zimethibitishwa na mmoja wa Wanafamilia aitwae Mohammed Ibrahim Raza ambapo maziko yatafanyika leo Kisutu Dar es salaam.

Itakumbukwa May 09,2023 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali alimtembelea Mohamed Raza baada ya kulazwa Hospitalini Jijini Dar es salaam. View attachment 2650702

R.I.P classmate
 
Baada ya mvutano wa kimakataba wa muda mrefu kati ya Yanga SC na Mchezaji Feisal Salum hatimaye leo suala hilo limefikia tamati baada ya Yanga kumuuza Mchezaji huyo kwa Azam FC.

Taarifa rasmi ya Yanga SC imesema wamepokea ofa kutoka Azam FC na kuamua kumuuza Mchezaji huyo baada ya makubaliano ya pande zote mbili.

Feisal anaenda Azam FC kwa ada ya uhamisho ambayo hata hivyo bado haijatajwa ambapo amekuwa nje ya uwanja takribani kwa miezi sita… toka 24/12/2022 alipoandika barua ya kuomba kuvunja mkataba na Yanga. View attachment 2650701

Kiko wapi UTO
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom