Makapuku Forum

Makapuku Forum

Polisi Mkoani Mwanza wametoa ufafanuzi juu ya taarifa inayosambaa mitandaoni kumhusu Mbunge wa Jimbo la Nzega Vijijini na Mmiliki wa Kiwanda cha kuchakata Pamba kitwacho Mwalujo Ginery kilichopo Kijiji cha Mwalujo, Wilaya ya Kwimba, Hamisi Kingwangala kudaiwa kumpiga risasi Mlinzi wake Jumanne Omary Misango (66) katika mguu wa kulia, ambapo imebainika Jumanne hakupigwa risasi bali haliwaongopea Polisi.

RPC wa Mwanza, Wilbrod Mutafungwa amesema taarifa za awali zinaonesha kulitokea wizi wa mali kiwandani ikiwemo Gear Motor HP Radio made 02, Electrical Motor 05 na nyaya za umeme @ Armored Cable Mita 25 vyote vikiwa na thamani ya Tsh 28,525,000.

“Mei 22, 2023 saa 11:00 jioni Kigwangala alifika kiwandani kwake na kukatokea majibizano kati yake na Mlinzi wake, Mlinzi huyo alitoa taarifa Polisi kuwa alishambuliwa na kupigwa risasi mguu wa kulia, Askari walifika eneo la tukio na kufanya ukaguzi ambapo hakukuonekena viashiria vyovyote vya matumizi ya silaha ya moto”

“Hata hivyo Jumanne alipewa PF3 na kwenda Hospitali ya Wilaya ya kwimba kwa uchunguzi wa kitabibu, Hamisi Kigwangala alihojiwa na kufunguliwa kesi ya shambulio na yupo nje kwa dhamana”

“Uchunguzi umebaini kuwa hakuna jeraha wala mvunjiko wowote wa mfupa katika mwili wa Jumanne na hivyo amefunguliwa jalada la uchunguzi kwa kosa la kutoa taarifa za uongo kwa Afisa wa Polisi na kuzua taharuki kwa Jamii kuwa amepigwa risasi, upelelezi wa kesi hizo mbili unaendelea na utakapo kamilika Watuhumiwa wote wawili watafikishwa Mahakamani, Jeshi la Polisi linatoa rai kwa Wananchi kuacha kujichukulia sheria mkononi”
Screenshot_20230527_125131.jpg
 
Naibu Waziri Mambo ya Ndani ya Nchi na Mbunge wa Jimbo la Butiama, Jumanne Sagini leo May 27, 2023 ameongozana na Wanafamilia, Ndugu, Jamaa na Marafiki wa aliyewahi kuwa Mbunge wa Jimbo la Butiama Mkoani Mara Nimrod Mkono ambaye mwili wake umewasili leo katika Uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere kutokea Nchini Marekani ambapo alikuwa akipatiwa matibabu tangu mwaka 2018 na kufariki April 18, 2023.

Mara baada ya kupokelewa kwa mwili huo mapema leo katika Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere mwili huo ulipelekwa nyumbani kwake Masaki Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya ibada na kesho May 28, 2023 mwili wa marehemu Nimrod Mkono utaagwa katika Viwanja vya Karimjee na hatimaye kusafirishwa kwenda Kijijini kwao Busegwe Wilaya ya Butiama Mkoani Mara kwa ajili ya shughuli za mazishi siku ya Jumatatu.
Screenshot_20230527_125326.jpg
Screenshot_20230527_125351.jpg
Screenshot_20230527_125418.jpg
 
Shamrashamra za Makatibu Mahsusi pamoja na Watunza Kumbukumbu na Nyaraka wakati wa kilele cha mkutano wao wa Kitaaluma wa Chama cha Makatibu Mahsusi Tanzania (TAPSEA) pamoja na Menejimenti ya Watunza Kumbukumbu na Nyaraka (TRAMPA) unaofanyika Fumba Zanzibar leo Jumamosi Jumamosi Mei 27, 2023.
Ikulu
Screenshot_20230527_130525.jpg
 
KANE MADRID
.
Straika, Harry Kane ameripotiwa kutolewa kama ofa huko Real Madrid wakati Tottenham Hotspur wakijaribu kumzuia asiende kujiunga na Manchester United.
.
Kane, 29, amebakiza mwaka mmoja tu kwenye mkataba wake huko Spurs na kinachoelezwa ni kwamba huenda akabadili timu kwenye dirisha lijalo la uhamisho wa majira ya kiangazi litakapofunguliwa. Man United ni kati ya timu zinazopewa nafasi kubwa ya kumchukua Kane, lakini bosi wa Spurs hataki abaki ndani ya England.

Screenshot_20230527_130649.jpg
 
KWAHERI YA KUONANA
.
458—JORDI Alba amehusika katika mabao 118 kwenye mechi 458 za Barca katika michuano yote, akifunga 27 (kazidiwa na Pique (39) tu miongoni mwa mabeki waliofunga zaidi tangu msimu wa 12/13) na ametoa asisti 91 (kazidiwa na Messi (169) na Suarez (97) klabuni tangu wakati huo).
Screenshot_20230527_130751.jpg
 
United wameanza mazungumzo na mama na wakala wa kiungo wa Juventus na Ufaransa Adrien Rabiot, kwa nia ya kumsajili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 kwa uhamisho wa bure. (Nicolo Schira)

Screenshot_20230527_130923.jpg
 
Mshambulizi wa Argentina Angel di Maria anatazamiwa kuondoka Juventus kama mchezaji huru msimu huu wa joto, huku klabu kadhaa za MLS na Saudi Arabia zikitaka kumnunua mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 35. (90 Min)
Screenshot_20230527_131026.jpg
 
Paris St-Germain wamewasilisha ombi la kumnunua kiungo wa kati wa Sporting Lisbon na Uruguay Manuel Ugarte, huku Chelsea pia wakiwa katika kinyang'anyiro cha kumnunua mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22. (Fabrizio Romano)

Screenshot_20230527_131139.jpg
 
Kocha wa klabu tajiri zaidi duniani,Eddie Howe amekiri Newcastle "wamefanikiwa kupita kiasi" msimu huu na italazimika kutumia pesa nyingi msimu wa joto ikiwa wanataka kufikia Top 4 wakati ujao.

The Magpies walipata kurejea Ligi ya Mabingwa baada ya kukosekana kwa miaka 20 wakati ilipotoka sare ya 0-0 na Leicester City ili kufuzu katika nafasi ya nne-bora kabla ya safari ya siku ya Jumapili dhidi ya Chelsea.
Screenshot_20230527_131653.jpg
 
Farhan Jr

Kabla ya kulala nadhani Mwenyekiti wetu Mangungu tuna vitu vichache vya kukubaliana nawe kuelekea 2023/24 ili tusiwe na changamoto nyingi kama msimu huu unaomalizika.

Mwenyekiti suala la jezi rasmi za msimu mpya litazamwe kwa mapana sana, jezi zipatikane mapema kabla ya msimu kuanza, jezi zipatikane maeneo yote nchini ama tuwe na maduka ya kikanda, hili ni muhimu zaidi.

Kutangaza na kutoa jezi zetu mapema ni kuweka mazingira sahihi ya Mashabiki kujiandaa kiuchumi, ili waichangie klabu yao pale jezi zitakapotoka, hii itasaidia sana.

Mwenyekiti tuboreshe pia kwenye idadi ya jezi, tuna FA CUP, NBC PL na Champions League ni michuano Mama ambayo ni afya sana jezi zake zote zitoke pamoja mapema ili Mashabiki waenjoy na mitoko mapema.

Hii pia itatupa taswira nzuri kama timu, kuelekea SIMBA DAY mandhari yake yawe jezi mpya na kama kuna Wadhamini wapya basi wapate mileage yao vizuri sana, hili linawezekana.

Mwenyekiti pia nina ushauri huenda usiwe na maana sana ila tuone namna ya hii timu kucheza mechi angalau tatu kwenye mikoa ambayo soka halichezwi sana ili kuiuza hii timu na kuisogeza zaidi kwa watu.

Simba ni taasisi kubwa lakini marketing lazima iendelee, leo hii United, Madrid na timu kubwa zinazunguka duniani kucheza na kutambulisha wachezaji wao! Sisi tunaweza angalau mikoa mitatu nchini kabla ya kilele watu waione timu yao, hii sio ya Dar Es Salaam pekee.

La mwisho Mzee wangu Mangungu tupiganie hili suala la Wanachama wapya kama mchakato bado umekwama hapo FCC, ipo haja ya timu kuzalisha zaidi na kuingiza zaidi mapato kwakuwa lengo muscles basi hata mia mia zina nguvu yake.

Ni sahihi kufeli ila hatupaswi kufeli kwenye kila kitu! Muda tunao tena mwingi sana, em tujibane bane basi hapo tufurahi!

Ni hayo tu kwa leo!

Screenshot_20230527_132507.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom