Makapuku Forum

Makapuku Forum

Mabosi wa Yanga wakiongozwa na Rais Hersi Said watafika kambini leo baada ya kushindwa kufika katika kwa wakati wote hapo kabla. Nabi aliwaomba viongozi wasionekane maranyingi kambini ili kutoa nafasi kwa wachezaji kutuliza akili na kufanya kazi yao badala ya kuwa na hamasa muda mwingi ambayo inaweza kuwatoa mchezoni na kuwapotezea malengo.
Screenshot_20230526_145740.jpg
 
WADADA HUYOO SINGIDA BS
.
Klabu ya Singida Big Stars imeendelea kujiimarisha kwenye eneo lake la ulinzi baada ya kukamilisha usajili wa beki wa kulia Nicolas Wadada anayecheza katika kikosi cha Ihefu.
.
Huu unatajwa kuwa usajili wa pili kwa baada ya kukamilisha usajili wa Yahya Mbegu ambaye waliipokonya Simba tonge mdomoni. Habari ambazo ninazo ni kwamba Wadada tayari ameshamalizana na mabosi wa Singida na kilichobaki anasubili dirisha la usajili lifunguliwe na atangazwe.
.
Inadaiwa mabosi wa Singida wanataka eneo la beki ya kulia kuwe na uzoefu kwani tayari ilishamtoa kwa mkopo Juma Abdul kwenda Kitayosce kabaki Paul Godfrey ambaye na yeye hapati nafasi ya kucheza mbele ya Nicolas Gyan.
Screenshot_20230526_145843.jpg
 
WINGA FUNDI ANUKIA MSIMBAZI
.
Simba imepania kurejesha ufalme baada ya kukosa mataji katika misimu miwili mfululizo, na katika kufanikisha hilo imeamua kuingia sokoni kusajili mastaa wapya ambapo kocha mkuu wa kikosi hicho, Roberto Oliveira anataka.
.
Uongozi wa Simba upo tayari kumtimizia kocha Mbrazili huyo mahitaji yake na sasa wameingia sokoni kumng’oa winga na staa katika Ligi Kuu ya Rwanda, Leandre Willy Essomba Onana (23)
.
Onana anayekipiga Rayon Sport kwa sasa ndiye kinara wa mabao Ligi Kuu ya Rwanda akifunga 15 na kuasisti 10. Anasifika kwa kasi, chenga na stamina akiwa na mpira lakini pia ni mtaalamu wa kufunga akitumia zaidi mguu wa kulia.
Screenshot_20230526_145948.jpg
 
UNITED YAKUBALIANA NA NAPOLI KUHUSU KIM MIN-JAE
.
Taarifa kutoka Napoli zinadai Klabu ya Manchester United imeshafanya makubaliano na mabosi wa Napoli juu ya uwezekano wa kumsajili beki kisiki wa timu hiyo, Kim Min-jae, 26.
.
Beki huyu wa kimataifa wa Korea Kusini alikuwa sehemu ya ukuta mgumu ulioiwezesha Napoli kutwaa taji la Ligi Kuu ya Italia, Serie A msimu huu, mkataba wake unamalizika mwaka 2025.
.
Man United ambayo imekuwa na upungufu kwenye eneo lao la ulinzii msimu huu kutokana na majeraha ya mara kwa mara ambayo yaliwakumba mabeki wake, inaamini ujio wa Kim utaongeza ufanisi kwa kuwa haitakuwa na presha pale Raphael Varane ama Lisandro Martinez mmoja wao akiumia.
Screenshot_20230526_150228.jpg
 
KAMA THIERRY HENRY
.
44—ASISTI ya Erling Haaland wa Man City katika sare ya 1-1 dhidi ya Brighton, imemfanya mwamba huyo kuhusika katika mabao 44 ya EPL msimu huu (kafunga 36, asisti 8) – rekodi kwa msimu wa EPL wa mechi 38 akimfikia Thierry Henry ambaye msimu wa 2002-03 (alifunga mabao 24, akatoa asisti 20).
Screenshot_20230526_150342.jpg
 
SAKO LA NYANI
.
20—BRIGHTON ilipiga mashuti 20 dhidi ya Man City juzi usiku; ni Wolves (21 vs Man City Disemba 2019) na Atletico Madrid (22 vs Barcelona Machi 2009) pekee ndizo zilizopiga mashuti mengi zaidi dhidi ya timu inayofundishwa na Pep Guardiola.
Screenshot_20230526_150445.jpg
 
Tangu kurudi kwa Frank Lampard Chelsea ameiongoza timu kama Kocha kwenye game 10 , wamepata ushindi kwenye mechi moja tu !

10 games
8 kipigo
1 ushindi
1 sare
0 clean sheets

Ukirudi nyuma kidogo mechi yake ya kwanza ugenini msimu wa 2019 Frank Lampard alipoteza kwa bao 4-0 OT mbele ya United na mechi yake ya mwisho ugenini msimu huu 2022/23 amepoteza kwa bao 4-1 OT .
Screenshot_20230526_152124.jpg
 
Klabu ya Simba imemtangaza Mels Daalder [@dauble.12] raia wa Uholanzi kuwa Skauti Mkuu wa klabu hiyo. Mels amewahi kushiriki kozi mbalimbali za skauti ikiwa ni pamoja na zile zilizoendeshwa na David Hobson, skauti wa zamani wa Manchester United.
Screenshot_20230526_152314.jpg
 
Farhan Jr

Mara Yanga waliingiziwa Million 100 na mishahara ya miezi mitatu na Feisal kutaka kuvunja mkataba, mara Feisal hana Million 56 ya kwenda CAS hivyo Watanzania tumchangie.

Mara unasikia Yanga wapo tayari kuachana nae sasa afike klabuni wamalizane, mara Feisal anapost anataka kwenda CAS ambapo lengo ni lile lile kuvunja mkataba.

Mara tunaoshauri wamalizane klabu na Mchezaji tunaonekana hatumtakii mema ila wanaotaka mchakato wa kuchangisha wanaonekana wapo sahihi.

Mara najaribu kuwaza YANGA wakafanya tafiti wakagundua kuna msukumo wa THIRD PARTY na wakafungua mashtaka rasmi, mara wakakutwa na hatia third party na Mchezaji nini kitatokea?

Hizi cinema za kuingiza Million 112 kisha ghafla huna pesa zinaacha maswali sana, hiyo 112 ilitoka wapi kama Feisal hana tu Million 56? Kama Feisal hana 56M, kwanini mishahara yake hataki kupokea? Ioneokane Mchezaji hana pesa? Wakati Yanga wana taarifa za muamala wake wa 112 Million?

Mara nimeamua tu kukaa kimya ila ni mchezo wa hesabu kwa hesabu! Kwenye hii game hakuna mjinga hata mmoja, ngoja tuone mwisho wake.

Mara nakumbuka kisa maarufu cha Mzee mmoja huko Kijijini kwetu aliwahi kusikika akimwambia Mgeni mmoja aliyemkuta Mwanae tu ukubwani tena mjini, Mzee alisema;

“Lengo lako sio kumsaidia Mwanangu, bali unataka kuaminisha watu sikuwa Baba bora na bahati mbaya unamtumia Mwanangu kama chambo bila yeye kujua”

Mara nimeamua kukaa kimya rasmi na kuwaza usajili wa chama langu Simba maana naitaka nusu msimu ujao na Chelsea nautaka ubingwa

Screenshot_20230526_152450.jpg
 
Mkuu wa Tawi la Utawala wa Jeshi la Kujenga Taifa
(JKT), Brigedia Jenerali Hassan Mabena amewaita Vijana wote waliohitimu kidato cha sita mwaka huu kutoka Shule zote za Tanzania Bara kujiunga na mafunzo ya Jeshi hilo kwa mujibu wa sheria.

Brigedia Jenerali Mabena ametoa wito huo Jijini Dodoma wakati akiongea na Waandishi wa Habari kuhusu mafunzo hayo kwa mwaka huu, akiwataka kuanza kuripoti kuanzia June 01 hadi June 11 2023 katika Makambi waliyopangiwa.
Screenshot_20230527_051719.jpg
 
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Daniel Chongolo amesema wao CCM wanahitaji Katiba mpya bora kuliko Mtu yeyote ndio mana wamempa dhamana Mwenyekiti wao ambaye pia ni Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kuanzisha mchakato wa mapitio ya Katiba ili kujua iandikweje na iweje?.

Ameyasema hayo akiwa katika ziara ya kikazi Mafinga Wilayani Mufindi Mkoani Iringa

“Tuna Katiba ya mwaka 1977 tumeipitia hapa imetufikisha leo hapa tuna amani na nchi inaenda sasa tunaijadili Katiba mpya kuna mambo yanahitaji kupitiwa upya tofauti na ile pendekezwa ya mwaka 2014 tunataka kuendana na mazingira ya sasa”
Screenshot_20230527_051858.jpg
 
Waziri ya Mambo ya Ndani ya Kenya mapema hii leo amesema Kiongozi wa Kanisa la Goodnews International Church Paul Mackenzie alitumia magenge ya Watu wenye silaha ili kuwaua baadhi ya Wafuasi wake ambao walichukua muda mrefu sana kufa na wale waliobadili mawazo yao wakati wa mfungo.

Polisi wanaamini kwamba miili mingi iliyogunduliwa kwenye makaburi ya halaiki ni ya Wafuasi wa Mchungaji Mackenzie ambaye anashutumiwa kuwaamuru wafe njaa ili waweze kukutana na Yesu.

Ingawa njaa inaonekana kuwa sababu kuu ya vifo vya Wafuasi hao waliozikwa kwenye shamba la Shakahola, baadhi ya Waathiriwa ikiwa ni pamoja na Watoto walinyongwa, kupigwa na kukosa hewa, kwa mujibu wa Daktari Mkuu wa Serikali, Johansen Oduor.

Nyaraka za Mahakama zilizowasilishwa mapema mwezi huu zilisema kuwa baadhi ya maiti zilitolewa viungo vyao, huku Polisi wakidai Washukiwa hao walikuwa wakijihusisha na uvunaji wa viungo vya mwili kwa lazima huku ripoti za uchunguzi wa maiti zikithibitisha viungo vilivyopotea katika baadhi ya miili ya Watu ambao wamefukuliwa.
Screenshot_20230527_052202.jpg
 
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Amos Makalla ameagiza kufunguliwa kwa Baa na Hoteli zote zilizofungiwa na Baraza la Taifa la Mazingira (NEMC) kwa kosa la kufungulia muziki mkubwa na kuweka utaratibu wa haraka wa kuelimisha makundi hayo.

“Baa na Hotel hizi zikisimama, ajira zitasimama, biashara zitasimama na uchumi utasimama na tujiulize watawezaje kulipa faini wanazodaiwa wakati biashara wamefunga hawafanyi tena”

Makalla pia amepiga marufuku ukamataji wa nguvu huku akisema kuwa Wafanyabiashara hao sio majambazi hivyo wanapaswa kuelimishwa wanapokosea kwa kuangalia uhalisia wa maisha kwani kuua biashara ni rahisi sana kuliko kuijenga.

Ameitaka NEMC na Wafanyabiashara waliopigwa faini kuketi pamoja na kuzungumza namna ya kumaliza matatizo hayo ili kuhakikisha biashara hazisimami kwa sasa na amewataka watulie na kuondoa hofu kutokana na tafrani za kamatakamata.
Screenshot_20230527_052338.jpg
 
Wanafunzi wanaokadiriwa kuwa 262 wanaosomea kozi ya teknolojia ya habari (Information Technology) katika Chuo Kikuu Iringa (UoI), wanatuhumiwa kughushi mfumo wa SAMIS na kujilipia ada huku chuo kikiingilia kati suala hilo.

Mkuu wa Chuo Kikuu Iringa (UoI), Profesa Ndelerio Urio alikiri juu ya tatizo hilo kutokea na kwamba uongozi ulichukua hatua kwa kuunda tume ya watu wanne ambao wanaendelea kufanya uchunguza wa tukio hilo ambapo limekikoseha chuo mamilioni ya fedha.

Mfumo wa SAMIS unaodaiwa kuingiliwa na wanafunzi hao unatumika na chuo hicho katika masuala ya malipo ya ada, kuweka kumbukumbu za wanafunzi na masomo.

“Wanafunzi waliingilia mfumo, waghushi malipo ya ada na hivyo kuonekana hawadaiwi. Hii imekikosesha UoI mamilioni ya shilingi. Pia wanadaiwa kughushi stakabadhi za malipo na mihuri ya benki ili kuridhisha kuwa hawadaiwi ada,” amesema Profesa huyo.

Kwa mujibu wa uchunguzi ulifanywa na Mwananchi na kuthibitishwa na uongozi wa chuo, imebainika wanafunzi waliofanya hujuma hiyo ni wale wanaosomea cheti na shahada ya awali (bachelor) hali ambayo imeleta taharuki chuoni hapo.

Taarifa zinatanabaisha kuwa ada wanayopaswa kulipa wanafunzi wanaosomea kwa mwaka katika ngazi za cheti (certificate) ni Sh840, 000 huku wale wanaosomea shahada kwanza wakitakiwa kulipa Sh1, 670,400 katika mwaka wao wa kwanza.

Huku Sh1, 610,400 na Sh1, 760,400 zikitakiwa kulipwa mwaka wa pili na wa tatu wa masomo chuoni hapo.

Hata hivyo Mkuu huyo wa UoI ameiambia Mwananchi Digital kuwa uchunguzi wa awali uliofanywa ulibaini wanafunzi 262 ndio walihusika katika kadhaa hiyo ambao baada ya kufanikiwa na ukaonyesha wamelipa ada, waliruhusiwa kufanya mitihani kabla chuo hakijashtukia hujuma hiyo.

"Baada ya kuwabaini wanafunzi waliofanya hujuma hiyo huku wakiwa tayari walishafanya mitihani, tumezuia matokeo yao hadi watakapolipa ada kamili wanayodaiwa," alisema Profesa Urio.
Screenshot_20230527_053018.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom