Makapuku Forum

Makapuku Forum

Wale wa miaka yangu, naam miaka ile mwalimu anaheshimika kuliko waziri, viongozi tunawaita ndugu na hospitali sindano zilikuwa zinachemshwa maharage yanasubiri.
Naam nimekumbuka miaka hiyo leo kwa sababu dunia ya wapenda muziki wa nguvu (energetic music) imempoteza Tina Turner 1939-2023. Huyu ni malkia wa muziki wa Rock and Roll.

Kacheza vibao vingi vilivyopendwa duniani na tumboni kwake ni kama alikuwa na volkano, akiimba na kucheza bila kuchosha mashabiki wake.
Napenda muziki na ndiyo maana popote panapochezwa 'bakulutu' utanikuta ninamshukuru Mungu huku mkononi nimemkamata bata asiyefugwa. Ni maisha na nimeshare na wewe muda huu sababu dunia itammiss sana Tina Turner.
Bonus. Wimbo wake maarufu aliucheza baada ya kuamua kuachana na mume wake aliyekuwa akimpiga na kumnyanyasa na tangia hapo umaarufu ulikuwa ukimuulizia kila njia utasema Nemc wanahubiri kuwa na bar zisizopiga music. Pumzika legendary TT.

 
Wale wa miaka yangu, naam miaka ile mwalimu anaheshimika kuliko waziri, viongozi tunawaita ndugu na hospitali sindano zilikuwa zinachemshwa maharage yanasubiri.
Naam nimekumbuka miaka hiyo leo kwa sababu dunia ya wapenda muziki wa nguvu (energetic music) imempoteza Tina Turner 1939-2023. Huyu ni malkia wa muziki wa Rock and Roll.

Kacheza vibao vingi vilivyopendwa duniani na tumboni kwake ni kama alikuwa na volkano, akiimba na kucheza bila kuchosha mashabiki wake.
Napenda muziki na ndiyo maana popote panapochezwa 'bakulutu' utanikuta ninamshukuru Mungu huku mkononi nimemkamata bata asiyefugwa. Ni maisha na nimeshare na wewe muda huu sababu dunia itammiss sana Tina Turner.
Bonus. Wimbo wake maarufu aliucheza baada ya kuamua kuachana na mume wake aliyekuwa akimpiga na kumnyanyasa na tangia hapo umaarufu ulikuwa ukimuulizia kila njia utasema Nemc wanahubiri kuwa na bar zisizopiga music. Pumzika legendary TT.

Rip Tina
 
Magazeti ya leo may 25, 2023
Screenshot_20230525_064649_Opera%20Mini.jpg
 
Juma Msemwa (27) anashikiliwa na Polisi Njombe kwa tuhuma za kuwafungia ndani kwake kisha kuwabaka na kuwalawiti huku akiwa amewafunga kamba na kuwajaza vitambaa mdomoni Wanawake watatu katika Mtaa wa Kihesa Halmashauri ya Mji wa Njombe.

Prisca Mgaya ni Shuhuda aliyefika wakati wa kukamatwa kwa Kijana huyo na akiongea mbele ya DC wa Njombe, Kissa Kasongwa @kissagwakisakasongwa amesema alipata taarifa kwa Dada aliyetoroka kwenye nyumba waliyofungiwa kisha akaenda kuomba msaada dukani kwake akiwa na hali mbaya kwakuwa Juma alikuwa anafanya nao mapenzi siku nzima na alipochoka alizamisha gunzi au tango kwenye nyeti za Wanawake hao.

"Alipofika na kuniambia kuwa ametoroka kwenye nyumba waliyofungiwa na Juma ambaye alikuwa anawabaka, tukaondoka na wenzangu mpaka kwenye ile nyumba tukataka kuanza kuvunja mlango akatoka Kijana, tulipomuuliza yule Binti kama Kijana mwenyewe ni huyu akasema ndio lakini Kijana akaanza kukataa tukampiga kamba na kwenda kwenye vyumba vingine tukakuta vimefungwa tulipovunja chooni tukakuta Wamama wawili wakiwa uchi na huyu tuliyekuwa nae nje ni wa tatu"

DC Kissa Kasongwa amesema tayari Kijana huyo ameshikiliwa na Polisi huku akisikitishwa na kilichofanywa kwakuwa Mwanamke mmoja alikuwa amefungiwa kwa takribani wiki moja akiendelea kufanyiwa vitendo hivyo kila siku “Mmoja anasema kabakwa kwa saa 11 bila kupumzika”

"Niwashukuru Wananchi kwa kuwaokoa bila ya huyu mmoja kujinasua huenda leo tungeongea mengine nitoe rai kwa Wanawake kupunguza ujasiri wa kwenda kwa Mwanaume bila kumjua ni nani”
Screenshot_20230525_065707.jpg
 
Jeshi la Zimamoto na Uokoaji limesema hakuna madhara kwa Binadamu yaliyotokea kutokana na moto uliozuka Kiwanda cha kuzalisha plastiki cha Jambo 11 kilichopo Vingunguti Jijini Dar es salam lakini mashine na malighafi zimeungua na hadi sasa magari ya Zimamoto tisa yapo eneo la tukio kuendeleza mapambano ya kuuzima moto huo.

Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Ilala, Elisha Mugisha amenukuliwa akisema “Malighafi inayotumika kutengeneza plastiki na mashine zinazozalisha ndizo zinazoungua, tulichofanya ni kuzuia mashine ambazo hazijaathirika zisiungue na tumedhibiti moto usiende ghala jingine"

"Hapa tuna magari ya kuzimia moto tisa tunapokezana maji yakiisha wengine wanafuata Airport, tunapambana na kuzima moto kwanza, tukimaliza tutaanza uchunguzi kujua chanzo cha moto huu ni nini, kuna mashine kama saba zimeungua, hakuna Mtu aliyeumia au kupoteza maisha"
Screenshot_20230525_065808.jpg
 
Rais wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kushirikiana na Kenya na Uganda kupitia Pamoja Bid wamedhamiria kuwa Mwenyeji wa michuano ya Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika 2027.

Rais Samia amesema Nchi hizo zinawania nafasi hiyo kwa kutambua mafanikio makubwa ambayo Sekta ya Michezo imepata, hivyo kuwa Wenyeji wa AFCON 2027 kutaongeza hamasa zaidi kwa ukuaji wa michezo hususani soka na itachangia ukuaji wa utalii kwakuwa ni mashindano yanayotazamwa na zaidi ya Watu bilioni moja Afrika na maeneo mengi duniani.

Rais Samia pia amesema mashindano hayo yataleta Watu mashuhuri nchini wenye ushawishi duniani hivyo kuwezesha na kunufaisha sekta nyingi za uchumi na kuchangua ajira, mapato kwa Wafanyabiashara na Serikali.

Amesema Serikali imeshafanya utafiti na kuandaa mpango mkakati wa utekelezaji wa maandalizi ya kuwa Mwenyeji wa mashindano hayo ambayo yataweka rekodi kwa mara ya kwanza kufanyika katika Ukanda wa Afrika Mashariki tangu yalipoanzishwa rasmi mwaka 1957.

Katika hatua nyingine Rais Samia amepokea jezi alizokabidhiwa na Waziri wa Utamaduni, Sanaa, na Michezo Balozi Pindi Chana, na Naibu Waziri Hamis Mwinjuma maarufu @mwanafa wakati wa kukabidhi andiko la Ombi la Tanzania, Kenya na Uganda kuwa Mwenyeji wa AFCON mwaka 2027, kwenye Hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma leo tarehe 24 Mei 2023.
Screenshot_20230525_065928.jpg
 
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Innocent Bashungwa @innocentbash amewasilisha Bungeni Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 ambapo moja ya mambo aliyoyasema kwenye hotuba yake ni kutoa rai kwa Wabunge na Viongozi kuendelea kuwaelimisha Wananchi kuacha kuvamia maeneo ya Jeshi kwani ni hatari kwa maisha yao na mali zao.

“Wizara imeendelea kutekeleza Mkakati wa Uhakiki, Upimaji na Uthamini wa Maeneo ya Jeshi wa Miaka Mitatu (2020/21 – 2022/23) ili kuhakikisha maeneo yote ya Jeshi yanapimwa na kupatiwa Hati Miliki na hivyo kuondoa migogoro iliyopo, hadi sasa, Mkakati umetekelezwa kwa asilimia 71.48 kwa kuhakiki, kupima na kufanya uthamini wa maeneo mbalimbali ya Jeshi nchini”

“Katika Mwaka wa Fedha 2022/23, maeneo yaliyolipwa fidia ni pamoja na Gurungu, Mtipa, Mkiwa, Mkwese na Choda Mkoani Singida, Kisakasaka na Chukwani Mkoa wa Mjini Magharibi, Ras Nondwa Mkoani Kigoma, Itaga na Usule Mkoani Tabora, Funta Kihangaiko na Mkupuka Mkoani Pwani, Bulifani Misenyi Mkoani Kagera na Machenje Kongwa Mkoani Dodoma”
Screenshot_20230525_070053.jpg
 
Watu saba wamejeruhiwa na kupelekwa Hospitali ya Kairuki kwa ajili ya matibabu baada ya lifti kuporomoka kutoka ghorofa ya 10 katika jengo la Millenium Tower lililopo Kijitonyama Jijini Dar es salaam.

Jeshi la Zimamoto na Uokoaji limesema chanzo ni lifti hiyo iliyokuwa imebeba zaidi ya Watu kumi kuzidiwa uzito ——— “lifti ilizidiwa uzito na ilikuwa imefanyiwa matengenezo hivi karibuni ambapo leo ilikuwa inajaribiwa na kulikuwa na Fundi ndani”

Askari wa Zimamoto na Uokoaji Inspekta Msaidizi Mohammed kutoka Kinondoni amesema kilichofanywa na Uongozi wa jengo hilo lenye ghorofa 25 ni makosa kwa kuwa hawakupaswa kufanya majaribio ya lift kukiwa na Watu ndani bali walitakiwa kuweka kitu chochote chenye uzito ndani ya lifti ndio waifanyie marekebisho.
Screenshot_20230525_070207.jpg
 
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Innocent Bashungwa @innocentbash amewasilisha Bungeni Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 ambapo moja ya mambo aliyoyasema kwenye hotuba yake ni kutoa rai kwa Vijana wote wanaopata fursa za kupata mafunzo ya JKT, kuzitumia stadi za kazi na maisha walizozipata kujiajiri na kujitegemea.

“Wizara kupitia JKT imeendelea kuwapatia Vijana wa Kitanzania mafunzo ya ukakamavu, stadi za kazi, kuwajengea uzalendo na umoja wa kitaifa, katika mwaka wa fedha 2022/23, mafunzo yamefanyika kwenye kambi mbalimbali za JKT kupitia Operesheni Jenerali Venance Mabeyo, Vijana 24,458 kwa mujibu wa sheria wamepatiwa mafunzo, kati yao 17,942 wa kiume na 6,516 wa kike”

“Aidha, Vijana 11,358 wa Kujitolea wamepatiwa mafunzo, kati yao 7,483 ni wa kiume na 3,875 ni wa kike, dhumuni la mafunzo yanayotolewa kwa Vijana ni kuwapatia ukakamavu, stadi za kazi, kuwajengea uzalendo na umoja wa kitaifa ili baada ya kumaliza muda wa mafunzo na kutumikia JKT, waweze kurejea majumbani kwao wakiwa raia wema, wazalendo na wenye uwezo wa kujitegemea na kulilinda Taifa”
Screenshot_20230525_070305.jpg
 
Mwili wa MC Joel Misesemo Mkazi wa Mwananyamala ambaye alijirusha kutoka ghorofani kwenye jengo la Derm Plaza lililopo Makumbusho Kijitonyama na kufariki, umezikwa leo katika makaburi ya Kinondoni Jijini Dar es salaam.

Kwa mujibu wa Polisi Dar es salaam, uchunguzi wa awali unaonesha kuwa Marehemu alionekana katika jengo hilo tarehe 23, Mei 2023 majira ya saa kumi na moja alifajiri na alimwambia Mlinzi wa zamu kuwa anaenda kufanya ibada kwenye Msikiti uliopo ghorofa ya 15 ndani ya jengo hilo lakini muda mfupi baadaye alijirusha.

Taarifa ya Polisi imesema camera za jengo hilo zilimuonesha akijirusha kwa makusudi kutoka ghorofa ya saba kupitia dirishani na kufariki ambapo tayari mwili wake umepelekwa Hospitali ya Rufaa ya Mwananyamala kwa uchunguzi zaidi.

Jeshi la Polisi limesema limepata gari la Marehemu aina ya Suzuki rangi ya silver lenye namba za usajili T142 DRM lililokuwa limeegeshwa kwenye maegesho ya magari katika eneo hilo na sasa limehifadhiwa Kituo cha Polisi Oysterbay.
Screenshot_20230526_145246.jpg
 
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Innocent Bashungwa amewakabidhi magari mapya Wakuu wa Majeshi Wastaafu kwa maelekezo ya Rais na Amiri Jeshi Mkuu, Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Wakuu wa Majeshi Wastaafu waliokabidhiwa magari ni CDF Mstaafu George Waitara na Robert Mboma na makabidhiano hayo yamefanyika katika Ofisi za Wizara ya Ulinzi Mtumba Jijini Dodoma

Akikabidhi Magari hayo, Waziri Bashungwa amesema kuwapatia Wastaafu hao magari ni sehemu ya maelekezo ya Rais na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. Samia Suluhu Hassan kwamba wapatiwe magari mapya ambayo yanatengenezeka na spea zake zinapatikana kwa urahisi.

“Wakuu hawa wa Majeshi Wastaafu walifanya kazi kubwa na iliyotukuka kipindi cha utumishi wao kwa Nchi yetu, Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. Samia Suluhu Hassan imewapatia magari na kuwatakia kheri na maisha marefu Majenerali Wastaafu hawa”
Screenshot_20230526_145403.jpg
 
Isaka Rafael (27), Baba wa Watoto mapacha waliozaliwa kabla ya wakati na mmoja wao kunyofolewa jicho na ngozi ya paji la uso wakiwa Kituo cha Afya Kaliua, amesema tayari miili ya Watoto wake imezikwa lakini ameiomba Serikali kusimamia haki ya Watoto wake Mahakamani na kuhakikisha kila aliyehusika anapata adhabu inayostahili.

Isaka ameishukuru pia Serikali, Wadau na Wananachi wote kwa ushirikiano alioupata tangu sakata hilo lilipoibuliwa.

Miili ya Watoto hao mapacha waliozaliwa kabla ya wakati imezikwa kimila nyumbani kwao (ndani ya nyumba) katika Kijiji cha Kalemela Wilaya ya Urambo Mkoani Tabora.

Kwa upande wake RC Tabora ameendelea kusisitiza kuwa Wauguzi wanne wa Kituo cha Afya Kaliua watafikishwa Mahakamani kujibu tuhuma zinazowakabili wakati wowote kuanzia sasa kuhusiana na sakata hilo.
Screenshot_20230526_145531.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom