Makapuku Forum

Makapuku Forum

Magazeti ya leo May, 2023
Screenshot_20230516_055855_Opera%20Mini.jpg
 
MKALI WA HIZI KAZI
.
11—Manchester City imeshinda mechi zote 11 mfululizo za Ligi Kuu England, huku mara tatu zilizopita kwa timu kushinda mechi nyingi kiasi hicho mfululizo kwenye ligi hiyo ikikuwa ni timu ya Pep Guardiola (mechi 12 Jan. 2022 na mechi 15 Machi 2021).
Screenshot_20230516_072735.jpg
 
DE ZERBI NOMA
3—VIPIGO vitatu kati ya vinne vilivyopita ambavyo Arsenal imevipata kwenye uwanja wake wa nyumbani katika michuano yote vimekuja kutoka kwa Brighton, huku pia Brighton wakiwa ni timu ya tano ya ugenini kushinda kwenye uwanja wa Arsenal mara mbili msimu mmoja baada ya N. Forest (87-88), Aston Villa (93-94), Man City (2021) na Liverpool (21-22).

Screenshot_20230516_072855.jpg
 
Mastaa wa Marumo leo asubuhi walikutana na kikao kizito kilichoandaliwa na uongozi wa timu hiyo katika kuwahamasisha kufanya vizuri katika mechi yao kesho kutwa Jumatano dhidi ya Yanga.

Rais wa Marumo Gallants, bilionea Abraham Sello ndiye aliongoza kikao hicho kilichotumia takribani dakika 30 na Licha ya yaliyozungumzwa kufanywa siri, inafahamika kuwa nyota wa Marumo waliahidiwa bonasi ya Rand Milioni 8 sawa na Sh Bilioni 1 kwa fedha za Kitanzania iwapo watafanikiwa kushinda na kutinga Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Je, Marumo wataweza kupindua meza mbele ya Wananchi ..!?

Screenshot_20230516_073000.jpg
 
Farhan Jr

Nakumbuka mengi kuhusu mpira, nakumbuka the rainy nights in Stoke wakati Stoke City wakiwa uwanjani ile Jumatatu ya mvua na baridi kali, leo hawapo tena na mitaa inasema “Bring back our rainy nights in Stoke” yes! Ryan Shwacross atapiga munda kama hajui kitu na Howard Webb atapeta kama hakijatokea kitu.

The Good old days! Usiku wa kelele nyingi kwenye jiji la mitindo Milano! At the heart of fashion there is football! Wanaliita tempo la mpira ndio San Siro! Pale Ricardo Kaka na Seedord juu yupo Philpo Pippo Inzaghi, touchline ni Don Carlo na ufundi wake.

Ziko wapi nyakati? Wakati Manchester United wanavaa AIG, Arsenal wana O2! Liverpool wana Carlsberg na Chelsea wana Samsung Mobile, kabla ya Nandy kuwa mainstream, Zuchu ni bikra huko Paje! Lulu Diva hajui wanaume na Gigy Money yupo Mbeya anashindia parachichi.

Gone are the days! Wakati Fergie anatafuna big G ya mamillion, Wenger na makoti ya bei mbaya! Fabregas mtoto hapo analelewa kwa Mama wa Kiingereza, Man City wana Mido Upara Stephen Ireland kabla ya Kipara Guardiola, utaniambia nini?

The days! Jay Jay Okocha anapiga goli anaenda kukatika kuliko Angel Nyigu! Kipindi hicho EPL ni TVT na Star TV, kabla ya Instagram na Matonya anaitwa Seif Shabaan, enzi hizo sisi ni Chawa halisi wa game kabla ya Mwijaku na GSM, kipindi hicho Mond anamtazama Baba Levo kama role model.

Zipo wapi nyakati? Bambo na Senga, Steven Gerrard na Alonso Xabi! Ray na Kanumba, Patrick Viera na Roy Keane! Zipo wapi nyakati? Au lipigwe goli nislide kama Didier Drogba kwenye DM ya Hamisa? Hapana Kaka Ali atanipiga

Zipo wapi nyakati?

Screenshot_20230516_073141.jpg
 
Mkuu wa Jeshi la Sudan, Jenerali Abdel Fattah al-Burhan ametoa agizo la kuzifungia akaunti zote za benki za jeshi la akiba (Rapid Support Forces) pamoja na kampuni tanzu zake zote.

Amri hiyo, imetolewa Jumapili, Mei 14 ambapo bado haijulikani ni athari zipi zitakazojitokeza kwa RSF na jinsi maagizo ya Burhan yatakavyotekelezwa.

Jenerali Burhan pia amewastaafisha maafisa wanne wa kijeshi wanaohusishwa na kundi hilo akiwemo Brigedia Jenerali Omar Hamdan Ahmed, kamanda wa RSF Jenerali Mohammed Hamdan Dagalo, na ambaye kwa sasa anaongoza ujumbe wa jeshi la wanamgambo kwa mazungumzo ya amani na jeshi la Sudan huko Jeddah, Saudi Arabia.

Jenerali Burhan pia amemfuta kazi Gavana wa Benki Kuu, Hussain Yahia Jankol na kumteua Borai El Siddiq badala yake. Mpaka sasa hajatangaza sababu za kumfuta kazi Jankol.
Screenshot_20230516_073319.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom