Makapuku Forum

Makapuku Forum

Ripoti kutoka SA | Kuanzia hatua ya awali ya Mashindano (CAFCC) Marumo hawajapoteza wala kutoa sare katika mechi waliocheza uwanja wa nyumbani msimu huu 2022/23

Marumo Gallants 1-0 Elgeco Plus

Marumo Gallants 3-1 Al Ahli Tripoli

Marumo Gallants 4-1 Al Akhdar

Marumo Gallants 2-0 USM Alger

Marumo Gallants 3-2 FC Lupopo

Marumo Gallants 1-0 Pyramids

Je , Wananchi watatoboa ?
Screenshot_20230515_130909.jpg
 
Shabiki wa ‘kugalagala’ wa Simba @swalehmadjapa amesafiri kutoka Tanzania hadi nchini Afrika Kusini kwa ajili ya kushuhudia mechi ya pili [second leg] ya Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika kati ya Marumo Gallants dhidi ya Yanga!

Kwa zaidi ya miaka minne mfululizo Madjapa amekuwa akisafiri nchi tofauti za Afrika kwa ajili ya kushuhudia mechi za kimataifa za timu yake ya Simba lakini safari hii amesafiri kwa ajili ya Yanga.

Madjapa amesema mbali na kuipenda Simba kwa dhati, lakini anapena sana mpira wa miguu. Kwa hiyo anaumia kama mashabiki wengine wa Simba wanavyotambiwa na Wananchi kucheza Nusu Fainali ya mashindano ya CAF.

Amesafiri hadi Afrika Kusini ili kuwa sehemu ya historia endapo Yanga itafanikiwa kufuzu Fainali ya Kombe la Shirikisho anataka kuwa uwanjani akishuhudia.

“Mimi ni shabiki wa Simba lakini huku nimekuja kama mtanzania/mpenzi wa mpira wa miguu. Tangu nimefika hapa inatajwa Yanga na Tanzania. Yanga ikifanikiwa kufika Fainali itajizolea sifa kama klabu lakini pia Tanzania kama nchi.”

“Wakati Simba inafika Nusu Fainali ya mashindano ya CAF nilikuwa sijazaliwa, wakati inacheza Fainali ya mashindano ya CAF nilikuwa mdogo sikuona, sasa nataka kushuhudia mechi zote za timu kutoka Tanzania ikicheza Nusu Fainali na ikibidi Fainali.”

“Mafanikio ya Yanga yataleta chachu kwenye timu zetu nyingine kama Simba, Azam n.k. Klabu zikifanikiwa, timu yetu ya Taifa itafanikiwa pia. Tunataka kuiona Taifa Stars ikicheza AFCON au kufuzu kucheza Fainali za kombe la Dunia.”

Nipenda moyo wake, tunahitaji watanzania wengi wenye mtazamo kama @swalehmadjapa, tunashindana wenyewe kwa wenyewe ndani ya nchi lakini inapokuja kwenye masuala ya kimataifa tunasiamama pamoja kama nchi.
Screenshot_20230515_131007.jpg
 
Farhan Jr

PAPE OUSMANE SAKHO TRANSFER UPDATE

- Wawakilishi wa Mchezaji Pape Ousmane Sakho hawaridhishwi na kukosekana kwa muda wa kucheza kwa Mteja wao ndani ya Simba, wakiamini Msenegal huyo anastahili muda zaidi wa kucheza.

- Kutokana na hilo kwa mujibu wa taarifa nilizopata ni kuwa kuna baadhi ya ofa watazifikisha Msimbazi kumhusu Mteja wao ambazo zitakuwa na maslahi kwa Simba kiuchumi ili POS aweze kuondoka kusaka changamoto mpya.

- Tayari POS ameandika barua ya kuvunja mkataba baada ya mechi dhidi ya Ruvu huku mkataba wake ukitaka alipe mshahara wa miezi mitatu tu ili mkataba uvunjike, mkataba wake ulikuwa miaka mitatu tu na ameshacheza miwili.

- Wanaamini Kijana anastahili muda wa kucheza zaidi, ijapo mpaka sasa bado hakuna ofa mezani kwa Simba huku zikitarajiwa mwishoni mwa msimu.
Screenshot_20230515_131117.jpg
 
Rais wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya uhamisho wa baadhi ya Wakuu wa Mikoa ambapo amemuhamisha aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Amoss Makalla kwenda kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza akichukua nafasi ya Adam Malima aliyehamishiwa Morogoro.
Screenshot_20230516_050049.jpg
 
Rais wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya uhamisho wa baadhi ya Wakuu wa Mikoa ambapo aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Fatma Mwassa amehamishiwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera akichukua nafasi ya Albert Chalamila ambaye amehamishiwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam.
Screenshot_20230516_051333.jpg
 
Rais wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya uhamisho wa baadhi ya Wakuu wa Mikoa ambapo aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Adam Kighoma Malima amehamishiwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro akichukua nafasi ya Fatma Abubakar Mwassa ambaye amehamishiwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera.
Screenshot_20230516_051644.jpg
 
Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya uhamisho wa baadhi ya Wakuu wa Mikoa ambapo amemuhamisha aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera Albert John Chalamila kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam akichukua nafasi ya Amoss Makalla aliyehamishiwa Mkoani Mwanza.
Screenshot_20230516_051819.jpg
 
Tayari mwili wa Mwanamtandao maarufu Nchini Tanzania William Malecela maarufu kama ‘LeMutuz’ ambaye pia ni Mmiliki wa Online TV ya LeMutuz aliyefariki dunia jana Jijini Dar es salaam, umeagwa leo Karimjee kabla ya kusafirishwa hadi Dodoma atakapopumzishwa kwenye makazi yake ya milele.

Wasaniii, Wadau na Waombolezaji mbalimbali wakiongozwa na Baba wa Lemutuz, Mzee Malecela wamejitokeza kumuaga Lemutuz akiwemo aliyekuwa RC wa DSM, Paul Makonda, Mwigizaji Batuli, Mbunge Babu Tale, Mbunge Zungu, Doris Mollel, Kalito, Jembe ni Jembe na wengine.
Screenshot_20230516_052406.jpg
 
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameamua kukutana na kuongea na Wafanyabiashara wa Soko la Kariakoo leo ambapo tayari amefika Kariakoo muda huu badala ya Jumatano May 17,2023 ambayo ilitangazwa hapo wali hii ni kutokana na uzito wa suala hilo.

Awali mkutano kati ya Waziri Mkuu na Kamati ya Wafanyabiashara hao pamoja na TRA na Mawaziri wa Sekta husika ulitarajiwa kufanyika saa 8 Mchana kwenye Ofisi ya Waziri Mkuu Magogoni-Ikulu Dar es salaam Jumatano May 17, 2023 kwa uratibu wa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Amos Makala, lakini Waziri Mkuu ameamua aende leoleo Kariakoo.
Screenshot_20230516_053631.jpg
 
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa baada ya kusikiliza kero za Wafanyabiashara wa Kariakoo leo ameiagiza Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kufuta Vikosi Kazi (Task Forces) ambavyo amesema vinatumika kufanya kamatakamata na wakati mwingine kuchukua rushwa.

Waziri Mkuu Majaliwa akiwa Kariakoo jioni hii amesema “Tuna taarifa kuwa kuna kikosi kazi kimeundwa kinazunguka huko, Rais alikemea Vikosi Kazi (Task Forces) kwasababu vinatumika kuwasumbua Wafanyabishara na kuomba pia rushwa, naagiza hiyo Task Force isitishwe mara moja”

“Task force hii ndio inaendesha kamatakamata kila siku, Kamishna wa Mapato ya Ndani TRA naagiza isitishwe, kanuni zipo sheria zipo zinatuelekeza namna ya kulipa kodi, kamatakamata hii inafukuza Wafanyabiashara Kariakoo na mbaya zaidi mnawakamata hadi Wageni kutoka nje”
Screenshot_20230516_053814.jpg
 
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameshangazwa na Watumishi wa ngazi za chini wakiwemo wa TRA kukaidi maagizo ya Rais wa Tanzania Dkt. Samia, Makamu wa Rais na Waziri Mkuu, wakisema ni maagizo ya kisiasa tu ambapo amesema wakimbaini anayetoa majibu hayo atachukuliwa hatua.

Akiongea na Wafanyabiashara wa Kariako leo Waziri Mkuu ameshangazwa na wanaodharau kauli za Viongozi Wakuu wa Kitaifa “Akitokea Mtu anasema lazima ulete barua ya agizo lililotolewa na Rais, Makamu wa Rais au Waziri Mkuu, mtuletee huyo Mtu, Rais,Makamu wa Rais na Waziri Mkuu hawaandiki barua, wataandika barua ngapi?”

“Rais na Makamu wa Rais wanapoagiza sisi wa chini tunatekeleza, leo TRA Rais amesema kodi za miaka mitano mziache, nyie mnadai barua kwa Watu wa Kariakoo hivi Mfanyabiashara wa Kariakoo atapata wapi barua ya Rais? halafu unamwambia Mfanyabiashara hilo ni agizo tu la kisiasa, yaani agizo lililotolewa na Rais unasema ni la kisiasa hiyo ni dharau na natamani ningemjua aliyesema hivyo tumchukulie hatua”
Screenshot_20230516_053933.jpg
 
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewaomba Wafanyabiashara wa Kariakoo kusitisha mgomo na kufungua maduka yao huku akiagiza TRA kuacha kuwaonea Wafanyabiashara.

Akiongea na Wafanyabiashara wa Kariakoo leo, PM Majaliwa amesema “Nimeacha Bunge nimewafuata kuja kujua kuna nini!? Soko la Kariakoo tunalitegemea kutuingizia mapato ni lazima tulitulinze , nimesoma mabango yenu moja baada ya moja, kuna linalosema “TRA mmefukuza Wageni’ , mmeongelea EFD n.k, hakuna jambo mtalifanya tutalichukulia rahisirahisi”

“Tabia ya kuonea Wafanyabiashara ikome mara moja, hii ya kukusanya tu mnakusanya tu mpaka damu itoke hii sio sawa, wengine mnawazidishia kodi ili mkae nao chini muwaombe rushwa na hii rushwa inafanya Wafanyabiashara watoe hadi pesa zao za mauzo”

“Wafanyabiashara sikieni ombi la Serikali fungueni maduka yenu na matatizo yote keshokutwa tunayajadili keshokutwa, ningeweza kusema kesho lakini Mh.Rais amenituma kumwakilisha kwenye maziko ya Mh. Membe acha niende kesho asubuhi, ilitakiwa niende leo nimeghairi naenda asubuhi kesho nazika narudi tutatue matatizo”
Screenshot_20230516_054155.jpg
 
Hizi ni picha kutoka Kariakoo, Dar es salaam leo ambako Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alikutana na kuongea na Wafanyabiashara wa Soko hilo na kutangaza maagizo ya kuitaka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kufuta Vikosi Kazi (Task Forces) ambavyo amesema vinatumika kufanya kamatakamata na wakati mwingine kuchukua rushwa.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewaomba pia Wafanyabiashara wa Kariakoo kusitisha mgomo na kufungua maduka yao huku akiagiza pia TRA kuhakikisha haifanyi uonevu wowote kwa Wafanyabiashara.
Screenshot_20230516_055139.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom