Makapuku Forum

Makapuku Forum

Screenshot_20230515_051148_Opera%20Mini.jpg
 
NOMA
20/38 — MANCHESTER United hadi sasa msimu huu imeshinda michezo 20 ya Ligi Kuu England na 38 kwenye mashindano yote wanayoshiriki ikiwa ni mingi katika msimu mmoja tangu ifanye hivyo mara ya mwisho msimu wa 2010-11 (39).
Screenshot_20230515_073207.jpg
 
CAMAVINGA AIPA PRESHA MADRID
.
Real Madrid imejawa na hofu baada ya kiungo wao Eduardo Camavinga kupata majeraha katika mechi ya Ligi Kuu Hispania ‘La Liga’ dhidi ya Getafe wikiendi iliyopita.
.
Madrid imehofia huenda Camavinga akakosa mchezo wa pili wa nusu fainali ya Kombe la Ligi ya Mabingwa dhidi ya Manchester City utakaochezwa Etihad kesho kutwa, Jumatano.
.
Camavinga alionekana akiwekewa barafu kwenye goti lake alipokuwa benchi na kuzua hofu kwa Kocha Carlo Ancelotti.
.
Kiungo huyo kinda alionyesha kiwango bora dhidi ya Man City katika Uwanja wa Santiago Bernabeu, akicheza kama beki wa pembeni huju akisaidia kupeleka mashambullizi eneo la hatari.
Screenshot_20230515_073423.jpg
 
Spika wa Bunge Dkt.Tulia Ackson amelazimika kuahirisha shughuli za Bunge za leo Jumatatu May 15,2023 mara baada ya kipindi cha maswali na majibu mpaka saa kumi jioni kufuatia hitilafu ya umeme iliyotokea mara mbili Bungeni.
Screenshot_20230515_125345.jpg
 
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa anatarajia kukutana na kamati ya Wafanyabiashara wa Soko la Kariakoo, Mawaziri wa Sekta husika na Mamlaka ya Mapato Tanzania ( TRA) Jumatano May 17,2023.

Mkutano huo unaotarajiwa kufanyika Saa 8 Mchana kwenye Ofisi ya Waziri Mkuu Magogoni-Ikulu Dar es salaam Jumatano May 17, 2023 kwa uratibu wa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Amos Makala.

Kwa sasa Serikali inaendelea kuwasihi Wafanyabiashara wa Kariakoo kuendelea na shughuli zao za biashara wakati Serikali inajiandaa kukutana nao kwa lengo la kuwasikiliza na kushughulikia kero zinazowakabili.
Screenshot_20230515_125514.jpg
 
Tayari mwili wa Mwanamtandao maarufu Nchini Tanzania William Malecela maarufu kama ‘LeMutuz’ ambaye pia ni Mmiliki wa Online TV ya LeMutuz aliyefariki dunia jana Jijini Dar es salaam, umefikishwa Karimjee kwa ajili kuagwa kabla ya kusafirishwa hadi Dodoma atakapopumzishwa kwenye makazi yake ya milele.

Hadi kufikia sasa Wasanii na Wadau mbalimbali wamejitokeza akiwemo Haji Manara, Mwigizaji Batuli, MC Gara B, Duma, Faiza Ally na wengine.
Screenshot_20230515_125642.jpg
 
Aliyekuwa mpenzi wa bingwa wa ndondi (UFC) uzito wa kati, Israel Adesanya anayeitwa Charlotte Powdrell amemburuta mahakamani bondia huyo akidai nusu ya mali kwa sababu ya kuwa kwenye mahusiano naye kwa muda mrefu.

Wawili hao hawakuwahi kufunga ndoa mpaka walipotengana na hawakufanikiwa kupata mtoto kipindi cha miaka minne ya mahusiano yao.

Screenshot_20230515_130000.jpg
 
Klabu ya Yanga imeendelea kupanda katika viwango vya soka barani Afrika ikishika nafasi ya 9 na pointi 118.5 na duniani ya 104 baada ya kuwa na msimu mzuri katika mashindano ya kimataifa na ligi ya ndani.

Kwa mujibu wa Shirikisho la Kimataifa la Historia na Takwimu za mpira wa Miguu (IFFHS) limetoa orodha ya viwango bora kwa kipindi cha Mei 1, 2022 hadi Aprili 30, 2023 ambapo timu mbili za Tanzania zimeingia 10 bora mabazo ni Yanga na Simba.

Yanga ambao ni mabingwa wa Ligi Kuu Bara wanashika nafasi ya 9 Afrika na 104 duniani huku Simba ikishika nafasi ya 10 na 105 duniani.

Nafasi ya kwanza Afrika inashikiliwa na Al Ahly ambaye kwenye nafasi ya duniani yupo namba 5.

Screenshot_20230515_130220.jpg
 
Takwa la Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla la wafanyabiashara kumfuata Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa mjini Dodoma limepingwa.

Wafanyabiashara hao walioitisha mkutano mwingine baada ya Makalla kuondoka wamesema wanalipa kodi hivyo Waziri Mkuu Kama anataka kuonana nao awafuate kariakoo na sio wafanyabiashara kumfuata.

Azimio la wafanyabiashara hao endapo mfanyabiashara atakayefungua duka leo ni halali yao.

"Mwenyekiti usiogope tupo nyuma yako usiogope chochote," ameeleza mmoja wa wafanyabiashara hao aliyepanda jukwaani na kutoa muongozo alioudai ni wa kisayansi.

Screenshot_20230515_130402.jpg
 
NABI: TUTACHEZA KAMA WANAJESHI
.
“Nitaendelea kuwakumbusha wachezaji wangu kwamba tunatakiwa kuipigania heshima ya klabu yetu kwa kucheza kama wanajeshi tunatakiwa kwenda kuipigania Yanga, tunatakiwa kwenda kuipigania Tanzania.”
.
“Natamani kuona kila mchezaji akicheza kwa jihadi na kujitolea nguvu zake zote kama anavyocheza beki wetu Bacca, napenda sana kumuona anavyojituma uwanjani, tunatakiwa kukaba kwa nguvu na kushambulia kwa nguvu lakini kikubwa tukipata nafasi tuzitumie.
.
“Wapinzani wetu watakuja kwa nguvu kubwa kutokana na matokeo ya mchezo uliopita, nasi tunatakiwa kuwa na nguvu ya kutoruhusu watufunge kuwathibitishia kwamba hatukubahatisha.”
Screenshot_20230515_130649.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom