Makapuku Forum

Makapuku Forum

Screenshot_20230519_065107_Opera%20Mini.jpg
Screenshot_20230519_065125_Opera%20Mini.jpg
 
Rais Mstaafu wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete kwa niaba ya Wastaafu amemshukuru Rais wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwaalika kushuhudia uzinduzi wa Ikulu mpya ya Chamwino Dodoma huku akisema leo historia leo historia mpya imeandikwa Tanzania “Historia imeandikwa tena imeandikwa kwa wino wa dhahabu”

Akiongea Ikulu Dodoma Dkt. Kikwete amesema “Hili ni jengo ambalo tumejenga wenyewe, Wataalamu wetu walichora wakasanifu, tumetoa pesa zetu wenyewe kujengwa na leo limekamilika”

“Tukio hili linahitimisha dhamira ya Baba wa Taifa ya kuhamishia Makao Makuu ya Dar es salaam kuyaleta Dodoma, uamuzi ulifanyika mwaka 1971 lakini leo Mama yetu Rais Samia umekamilisha maana kilele cha uamuzi ule ni Rais kuhamia Dodoma na kuwa na Ofisi yakeDodoma”

“Katika kila awamu kuna yaliyofanyika, maana Uongozi ni kazi ya kupokezana vijiti unafanya anakuja mwenzako anafanya mpaka mnafika mwisho wa safari, yapo yaliyofanywa na Mwl Nyerere, akaja Mzee Mwinyi, Mzee Mkapa na katika kipindi changu niliamua tujenge Chuo Kikuu kikubwa zaidi Dodoma pale Chimwaga, nikaelekeza Ofisi ya Rais na Makazi ya Rais yajengwe Chamwino na Ofisi za Mawaziri zijengwe karibu na hapo, kukawa na mjadala nikawaambia nendeni Malyasia mkajifunze walivyojenga unavuka Makazi ya Mawari mbele ndio kuna Ofisi za Viongozi Wakuu wa Kitaifa”

“Mh. Rais wa awamu ya tano Dr. Magufuli akaanza ujenzi na Rais Dkt. Samia kazi ile umeikamilisha na umeikamalisha kwa kiwango cha juu sana, nakupongeza sana Rais kwa Uongozi wako na nawapongeza wote walioshiriki ujenzi, Mh. Rais unafanya mambo mazuri katika Nchi yetu mwenye macho haambiwi tazama, mwenye masikio haambiwi sikia, umepokea miradi mikubwa ungeweza kusema unaanza ya kwako lakini umesema kila kilichoanzishwa na Mtangulizi wako unakikamilisha”
Screenshot_20230520_145032.jpg
 
Rais wa Zanzibar Dr. Hussein Mwinyi amemshukuru Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutenga Ofisi ya Rais wa Zanzibar ndani ya Ikulu mpya ya Rais Chamwino Dodoma iliyozinduliwa leo.

Dkt. Mwinyi akiongea Ikulu Dodoma leo amesema “Tunashukuru kwa kutupatia eneo Serikali ya Mapinduzi Zanzibar hapa Dodoma naahidi tutajenga Ofisi ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar hapa Dodoma ili kuwawezesha Watumishi wetu kupata eneo bora la kufanyia kazi”

“Lakini pia ndani ya Ikulu mpya kumetengwa Ofisi ya Rais wa Zanzibar tunashukuru sana”
Screenshot_20230520_145244.jpg
 
Hizi ni picha za matukio mbalimbali yaliyojiri wakati Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan akizindua rasmi Ikulu mpya ya Chamwino Mkoani Dodoma leo May 20,2023.. tazama LIVE kinachoendelea kwenye uzinduzi muda huu kupitia Youtube ya millardayo
Screenshot_20230520_150045.jpg
 
Baada ya Arsenal kufungwa 1-0 na Nottingham leo ni rasmi Man City Bingwa wa EPL 2022/2023 kwa mara ya tatu mfululizo akiwa na michezo mitatu mkononi.

Man City ana point 85 akiwa amecheza michezo 35 na amesalia na game 3, Arsenal wana alama 81 na mchezo mmoja hata Man City afungwe game zote na Arsenal ashinde hawezi kuifikia Man City
Screenshot_20230521_041925.jpg
 
Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan wakati wa uzinduzi wa Ikulu mpya ya Chamwino Dodoma leo amesema baada ya kukamilika kwa Ikulu sasa wanatarajia kujenga jengo la kisasa (Samia Complex) ndani ya eneo hilo kubwa la Ikulu lenye Ekari 8473 na tayari michoro ipo tayari ambapo kwa sasa wanahangaika kutafuta fedha ili ujenzi uanze.

Rais Dkt. Samia amesema “Eneo hili bado kuna kazi ya kufanya na hatua inayofuata ni ujenzi wa jengo la kisasa ambalo Wasaidizi wangu wameliita Samia Complex ambalo litakuwa na ukumbi wa mikutano wa Watu Elfu mbili mpaka Elfu tatu, nyumba za Viongozi hasa Majirani zetu wa EAC na SADC kutakuwa na Zanzibar Lounge, East Africa Lounge, uwanja wa golf, viwanja vya michezo, njia za ndege na sehemu za historia za Viongozi wa Nchi zetu”
Screenshot_20230521_042919.jpg
 
Rais Mstaafu wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete kwa niaba ya Wastaafu amemshukuru Rais wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwaalika kushuhudia uzinduzi wa Ikulu mpya ya Chamwino Dodoma huku akisema leo historia leo historia mpya imeandikwa Tanzania “Historia imeandikwa tena imeandikwa kwa wino wa dhahabu”

Akiongea Ikulu Dodoma Dkt. Kikwete amesema “Hili ni jengo ambalo tumejenga wenyewe, Wataalamu wetu walichora wakasanifu, tumetoa pesa zetu wenyewe kujengwa na leo limekamilika”

“Tukio hili linahitimisha dhamira ya Baba wa Taifa ya kuhamishia Makao Makuu ya Dar es salaam kuyaleta Dodoma, uamuzi ulifanyika mwaka 1971 lakini leo Mama yetu Rais Samia umekamilisha maana kilele cha uamuzi ule ni Rais kuhamia Dodoma na kuwa na Ofisi yakeDodoma”

“Katika kila awamu kuna yaliyofanyika, maana Uongozi ni kazi ya kupokezana vijiti unafanya anakuja mwenzako anafanya mpaka mnafika mwisho wa safari, yapo yaliyofanywa na Mwl Nyerere, akaja Mzee Mwinyi, Mzee Mkapa na katika kipindi changu niliamua tujenge Chuo Kikuu kikubwa zaidi Dodoma pale Chimwaga, nikaelekeza Ofisi ya Rais na Makazi ya Rais yajengwe Chamwino na Ofisi za Mawaziri zijengwe karibu na hapo, kukawa na mjadala nikawaambia nendeni Malyasia mkajifunze walivyojenga unavuka Makazi ya Mawari mbele ndio kuna Ofisi za Viongozi Wakuu wa Kitaifa”

“Mh. Rais wa awamu ya tano Dr. Magufuli akaanza ujenzi na Rais Dkt. Samia kazi ile umeikamilisha na umeikamalisha kwa kiwango cha juu sana, nakupongeza sana Rais kwa Uongozi wako na nawapongeza wote walioshiriki ujenzi, Mh. Rais unafanya mambo mazuri katika Nchi yetu mwenye macho haambiwi tazama, mwenye masikio haambiwi sikia, umepokea miradi mikubwa ungeweza kusema unaanza ya kwako lakini umesema kila kilichoanzishwa na Mtangulizi wako unakikamilisha”
Screenshot_20230521_043031.jpg
 
Rais wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema katika utekelezaji wa wazo la kuhamia Dodoma lililoasisiwa na Mwl Nyerere na katika msukumo wa ujenzi wa Ikulu ya Chamwino Dodoma, Hayati Dkt. Magufuli ameandika hadithi yake na mchango wake hauwezi kuacha kutajwa.

Akiongea wakati wa uzinduzi wa Ikulu mpya Dodoma leo, Rais Samia amesema “Nazipongeza awamu zote kwa uamuzi wa kuhamishia Makao Makuu Dodoma, ni katika kipindi cha awamu ya tano chini ya Hayati Magufuli msukumo wa kuhamia Dodoma ulichukuliwa”

“Mzee wetu Ally Hassan Mwinyi alituambia maisha ni hadithi na kututaka tujitahidi kuandika hadhithi njema za maisha yetu, katika utekelezaji wa wazo hili la kuhamishia Makao Makuu ya Serikali hapa Dodoma, hakika Ndugu yetu Hayati Magufuli ameandika hadithi yake”

“Hatutoweza kuandika historia ya shughuli hii ya uzinduzi wa Ikulu mpya Dodoma bila kuwepo kwa tahariri ya mchango wake mkubwa tuendeee kumuomba Mungu ampuzike kwa amani”
Screenshot_20230521_043118.jpg
 
Rais wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema kama alivyoahidi wakati anashika hatamu ya uongozi atahakikisha anaikamilisha miradi yote aliyoirithi kwa Mtangulizi wake Rais wa awamu ya tano, Hayati Dkt. Magufuli na miradi mipya aliyoianzisha na kusema hadi sasa ameshakamilisha Daraja la Tanzanite na Ikulu mpya ya Dodoma.

Akiongea wakati wa uzinduzi wa Ikulu mpya Ddooma leo, Rais Samia amesema “Kama nilivyoahidi wakati nakabidhiwa hatamu ya uongozi wa Nchi yetu kuwa nitaendeleza mema yaliyopo, nitaboresha inapobidi na nitaleta mema mapya kwa misingi ya kauli mbiu ya kazi iendelee, ujenzi wa Ikulu ilikuwa ni moja ya miradi niliyoirithi kutoka kwa Dkt. Magufuli”

“Mtakumbuka mradi wa kwanza kukamilisha ilikuwa Daraja la Tanzanite DSM, huu ni mradi wa pili na InshaAllah Mungu anipe uwezo nikamilishe yote, nashukuru Mungu kwa kunipa uwezo wa kuifanya kazi hii na leo tupo hapa tunashuhudia uzinduzi”
Screenshot_20230521_043208.jpg
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom