Shunie
JF-Expert Member
- Aug 14, 2016
- 157,077
- 464,004
Rais Mstaafu wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete ametuma salamu zake za rambirambi kwa Mke wa aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje, Mama Dorcas Membe akielezea alivyopokea taarifa za kifo cha Membe kwa mshtuko na huzuni kubwa.
Dr. Kikwete amesema “Nimemfahamu Membe miaka mingi, tumetoka nae mbali na tumesaidiana kwa mengi, Familia zetu, na mapito ya maisha yetu yamehusiana sana, Bernard KamilliusMembe alikuwa ni Mtu wa msaada mkubwa kwangu katika maisha yangu ya kikazi na kisiasa”
“Nilimuamini na kumtumainia katika nafasi zote alizohudumu kwenye Baraza langu la Mawaziri, aliwahi kuwa Naibu Waziri katika Wizara ya Mambo ya Ndani, na Wizara ya Nishati na Madini, aliwahi pia kuwa Waziri wangu wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kwa miaka 9 ambapo alifanya kazi kubwa na zuri ya kuendeleza maslahi ya Tanzania katika medani za Kimataifa”
“Nautambua mchango wake mkubwa alioutoa kwenye Chama Cha Mapinduzi alipokuwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa, Mjumbe wa Kamati Ku na Katibu wa Siasa na Uhusiano wa Kimataifa katika Sekretariati ya Halmashauri Kuu ya Taifa, katika nafasi zote hizo, alijitoa kwa moyo wake wote na kuacha alama za Kudumu”
“Nilimfahamu Mheshimiwa Membe kama Mwanadiplomasia Mbobezi, Mwanamikakati makini, Msomi mzuri, Mcha Mungu, Mzalendo,Mchapakazi hodari na Mtu jasiri ambaye hakuogopa kusema na kulisimamia analoliamini.
“Hakika Taifa limepoteza mmoja wa watu wake muhimu, natoa salaam za rambirambi na mkono wa pole kwako Shemeji yangu Dorcas Membe na Watoto wenu Cecilia, Richard na Dennis, pamoja na Wajukuu, Ndugu na Jamaa wa Marehemu Bernard Kamilius Membe, nawapeni pole kwa msiba mkubwa uliowakuta, lakini napenda kuwahakikishiakuwa hamko wapweke, Mimi pamoja na Mke wangu Salma na Wana Familia wetu wote, tuko pamoja nanyi katika majonzi na kuomboleza, tunawaombea kwa Mola awajalie moyo wa subira na ustahamilivu katika kipindi hiki kigumu mnachopitia, tukumbuke daima “Sisi sote ni Waja wake, na kwake tutarejea" Bwana ametoa, Bwana ametwaa, jina lake lihimidiwe, Tumuombee kwa mola marehemu mpendwa wetu, apumzike kwa amani na Roho yake aiweke Mahala Pema Peponi. Amina”

Kutoka ndani ya Ligi Kuu, Simba wameshamalizana na beki Yahya Mbegu na wapo kwenye mazungumzo na Kiungo Sospeter Bajana na fundi Bruno Gomes ambaye ni pendekezo la Kocha Robertinho.
mara moja kufuatia kipigo cha aibu cha mabao 3-0 wakiwa nyumbani dhidi ya Alahly mchezo wa mkondo wa kwanza wa Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.