Makapuku Forum

Makapuku Forum

KEVIN DE BRUYNE — MAN OF THE MATCH.
Screenshot_20230510_053808.jpg
 
"Jana nilikuwa kwenye Kikao na Shirikisho la Soka Afrika CAF pamoja na timu nyingine saba tutakazoshiriki nazo kwenye mashindano ya Africa Super League yatakayofanyika kuanzia mwezi October hadi November kwa mfumo Nyumbani na Ugenini, ambapo sisi Simba SC tunaimani kubwa ya kufanya vizuri kwasababu ligi yetu ipo ukingoni kwamaana hiyo tutakuwa na muda wa kufanya maboresho ya kikosi pamoja na maandalizi bora"

"Na timu ambazo tutashiri nazo Super League ambazo zote jana nilishiriki nazo kwenye Kikao ni Enyimba, Al Ahly, TP Mazembe , Wydad Casablanca, Mamelod Sundowns, Petro Athletico pamoja na sisi Simba SC wenyewe"- Imani Kajula Mtendaji Mkuu wa Simba SC.

Screenshot_20230510_055342.jpg
 
"Timu yetu imeshatoa Bonus zaidi ya Billion 1.1 na kiasi kilichobaki ni milioni 20 pekee tena ni Bonus ya Ligi ya ndani, wewe vuta picha Klabu inalipa zaidi ya Billion 1.1 inashindwaje kulipa milioni 20 haingii akilini hilo ni jambo linalopitia mchakato wa kitaasisi na lipo ndani ya uwezo wetu.

Vuta picha wachezaji wanalipwa mshahara kiasi gani na ukilinganisha na milioni 20 ambayo watagawana watu zaidi ya 30 kila mmoja atapata kiasi gani, ambapo kukosekana kwake ije iathiri matokeo kwenye mechi.”"- Imani Kajula Mtendaji Mkuu Simba SC.

Pia Mtendaji Mkuu Iman Kajula, amesema kwenye mikataba yao hakuna sehemu ambayo imesema itawalipa Bonus ila huwa wanatoa kwa ajili ya kuwahamasisha wapandane zaidi kwenye kile wanachokipambania.
Screenshot_20230510_055454.jpg
 
Shaffih Dauda

Kama wanabaki na Robertinho wampe nafasi ya kuja na wasaidizi wake , Kocha hawezi kuja na begi tu hii sio Simba ile , Kocha anatakiwa kuja na Watu wake ambao watashirikiana kama timu sio anakuja anakuta Meneja , Kocha msaidizi wanatofautiana mitazamo

Unajua hawa Waswahili wanakuwa na mambo yao ukimleta huyu anashindwa kuwa huru , ndio maana inashauriwa mara zote Klabu kama Simba ambayo inaenda kwenye Professionalism Kocha aje na watu wake ili baadae uweze kum-judge

DIGALA
Screenshot_20230510_055542.jpg
 
Shaffih Dauda

Simba wamesajili lakini hawaamini baadhi ya Wachezaji wao , mwanzoni Moses Phiri hakuanza alivyopata nafasi akafunga magoli ya kutosha bahati mbaya akaumia, Dirisha dogo akaja Baleke na yeye hakupata nafasi alivyopata nafasi akafunga akajihakiikishia nafasi .

Ni fikra kwamba ukicheza vizuri lazima mchezo unaokuja ucheze wanatakiwa kucheza kwa mpango kazi , wakati mwingine uswahili hizi timu unachukua nafasi sana mfano Aish na Beno .

Mara nyingi Aish akipata matatizo Beno anacheza na hajawahi kuonekana ni Kipa wa akiba , huna sababu ya kulitetea benchi la ufundi la Simba una Makipa wawili wote ni wa timu ya Taifa.

Swali, Benchi la ufundi kwanini hawamchezeshi Beno ?

#DIGALA
Screenshot_20230510_060008.jpg
 
Farhan Jr

MATUSI MENGINE KWENYE MPIRA WA MIGUU.

Simple logic ni kuwa Watu wanasema Clatous Chama anacheza chini ya kiwango kwenye big games, niwaulize swali kuna mechi ambayo Simba wamecheza vizuri then Chama hajaperform? Timu kama imeshikwa unatarajia afanye nini?

Game ya Simba vs Yanga ya 4-1, mechi ilikuwa nzuri akaonesha uwezo, mechi dhidi ya Yanga ya 2-0 akaonesha uwezo wake! Game ya Wydad home na hata away alicheza mpira kwakuwa timu inaflow vizuri na huduma zinafika kwake, ni mfano tu wa game ambazo Simba alicheza mpira.

Chama cant perform kama timu imeshikwa ila ataperform kama timu inacheza, vs Azam hata huduma kwao haifiki watu wanakata umeme katikati ulitarajia nini? Football ni collective sio Chama peke yake, Azam walihakikisha hawi huru na mpira, nafasi zilikuwa finyu.

Watu wanasahau hata game ambazo kuna muda uwezo wake binafsi unaamua game, thats football! Brilliance ipo lakini not every day na ndio maana timu zina Messi na Ronaldo na bado wanafungwa, uwezo binafsi upo ila timu lazima iwe katika level flani.

Its true ni ushindani wa Chama vs Chama, lakini lazima tutazame Simba kachezaje na Mpinzani amechezaje, mwisho wa siku thats football and Chama is the best!

Unfair kwa MVP! Top assist kwenye Premier League, moja kati ya Top scorers pale CAF na assists pia yupo miongoni mwao, tuheshimu mpira na tumheshimu Mchezaji Bora kuwahi kutokea, form is temporary but class is permanent.

Respect the GOAT @realclatouschama
Screenshot_20230510_060318.jpg
 
Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amesema Serikali inatarajia kubadilisha jina la Hospitali ya Taifa ya Afya ya Akili Mirembe na kuitwa National Instititue for Mental Health.

Amesema hayo leo katika semina maalum iliyoandaliwa kwa Wabunge wa Bunge la Tanzania kupata elimu ya masuala ya afya ya akili, Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) pamoja na Bohari ya Dawa (MSD).

“Tunakwenda kubadili jina la Hospitali ya Mirembe ili kujenga taswira mpya ndani ya jamii kwenye huduma zinazotolewa pale, mtu anaweza kwenda pale kutibiwa hata Malaria, lakini jamii inamuita ‘chizi’. Tunataka Mirembe iitwe National Instititue for Mental Health,” amesema

Ameongeza kuwa “Tunataka Hospitali ya Mirembe ifanye kampeni za hamasa na kuelimisha jamii kuhusu masuala ya afya ya akili, matibabu, tafiti mbalimbali za masuala ya afya ya akili pamoja na kufanya mafunzo.
Screenshot_20230510_060518.jpg
 
Afisa Habari wa Simba SC, Ahmed Ally amesema kuchelewa kwa madai ya posho za wachezaji katika michezo kadhaa si sababu ya timu hiyo kutokufanya vizuri hususani katika mechi dhidi ya Azam FC iliyochezwa Mei 07, mwaka huu.

Akizungumza katika mahojiano na E-FM, Ahmed amesema ni jambo la kawaida kwa taasisi kuchelewa kutoa posho kwa wachezaji, na kwamba si mara ya kwanza kwa klabu ya Simba kufungwa na Azam.

“Ni kweli kwamba wachezaji wanadai bonus [posho] zao za mechi kadhaa, na hilo ni jambo la kawaida, kuna wakati taasisi inakuwa na fedha inalipa madeni yote, na kuna wakati taasisi inakuwa haina fedha inalimbikiza madeni, mzigo ukipatikana watu wanalipwa. Na hata wachezaji wa Simba wanafahamu kwamba mzigo ukipatikana kila mmoja analipwa haki yake,” amesema Ahmed.
Screenshot_20230510_060745.jpg
 
Uganda imekanusha madai kuwa Virusi vya Corona ndio kichocheo cha wimbi la kikohozi na mafua yaliyowakumbua watu wengi nchini humo na kupelekea baadhi kuwekewa mashine za kupumua.

Idara ya Kudhibiti Magonjwa Yanayoambukiza imesema wimbi hilo ni mafua ya kawaida, na si ongezeko la visa vya UVIKO-19.
Screenshot_20230510_060953.jpg
 
Watu waliofariki kutokana na mafuriko na mmomonyoko wa ardhi Mashariki mwa DR Congo imefikia 400, huku kazi ya kutafuta wengine ikiendelea.

Ajali hiyo ilivikumba vijiji viwili juma lililopita, hivyo kuwaacha mamia ya wananchi bila makazi na chakula.
Screenshot_20230510_061046.jpg
 
Rais wa Urusi, Vladimir Putin amesema anataka kuona amani ikitawala lakini nchi za Magharibi zinapandikiza mbegu ya chuki dhidi ya nchi hiyo.

Akihutubia katika siku ya mashujaa amewapongeza wanajeshi wanaoshiriki kwenye alichokiita operesheni maalum ya kijeshi nchini Ukraine na kuwa hatma ya dola ya Urusi inawategemea wao.
Screenshot_20230510_061137.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom