BAADHI ya wachezaji wa Wigan wenye hasira wamepanga kufanya maandamano na waligoma kucheza mechi yao mwisho ya Ligi daraja la Kwanza dhidi ya Rotherham.
Wachezaji wa kikosi hicho cha Wigan waligoma kufanya mazoezi wikiendi iliyopita ikidaiwa kwamba mmiliki wao ameshindwa kuwapa mishahara yao yote.
Imeelezwa kuna Wachezaji ambao wamechelewa kulipwa mishahara yao, lakini wale ambao mkataba wao inamalizika mwisho wa msimu hawajalipwa mishahara yao.
Ingawa mishahara hiyo imechelewa kuingia kabla ya mechi yao dhidi ya Millers, wachezaji wa Wigan wangegoma kucheza mechi ya mwisho ya msimu huku Ligi daraja la Kwanza.
Mwenyekiti wa Wigan, Talal Al Hammad aliweka wazi mishahara haitawekwa hadi mechi itakapochezwa jambo ambalo limepingwa vikali na wachezaji wao.
View attachment 2616232